Mapinduzi ya Julai 23 na Athari Zake kwa Harakati za Kijamii

Mapinduzi ya Julai 23 na Athari Zake kwa Harakati za Kijamii

Imetafsiriwa na/ Abdelrahman Muhammad 
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed

Mapinduzi ya Julai 1952 chini ya uongozi wa kiongozi Jamal Abdul Nasser yalikuwa na lengo la kufanya elimu kuwa nguvu inayoongoza katika harakati za kijamii, ambayo kwa upande wake itaathiri maendeleo ya kijamii kutoka msingi wa piramidi ya jamii.

Hivyo tunakuta katika miaka kumi ya kwanza (1952-1962) ya harakati ya jeshi ambayo itageuka kuwa mapinduzi ya kijamii ambapo mapinduzi yalitumia fedha nyingi kwa elimu (kama nguzo ya msingi katika mradi wa taifa wa maendeleo) kiasi cha mara mbili ya kile kilichotumiwa katika miaka sabini iliyopita tangu utawala wa Waarabu na Misri ilipokuwa chini ya utawala wa ukoloni na wafuasi wake wa familia ya muuzaji wa tumbaku (1882 - 1952).

Inasemekana kuwa takwimu zinaonyesha kwamba jumla ya pauni milioni 200 zilitumika kati ya mwaka 1882 na 1952, yaani kwa kipindi cha miaka 70.

Kwa upande mwingine, Mapinduzi ya Julai yalitumia pauni milioni 400 kati ya mwaka 1952 na 1962, yaani kwa kipindi cha miaka 10.

Ingawa takwimu zinaeleza ukweli, ni muhimu kutambua matukio na maafa makubwa ambayo nchi ya Misri ilikabiliana nayo katika kipindi hicho, kama vile:

1. Kitaifaishaji wa Mfereji wa Suez na uvamizi wa Tatu.
2. Umoja na Syria, kisha kujitenga.
3. Kuunga mkono mapinduzi ya ukombozi katika ulimwengu wa Tatu.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy