Siku ya Hisani Duniani

Siku ya Hisani Duniani

Tunaishi kwa kile tunachopata, lakini tunatengeneza maisha kupitia kile tunachotoa. 

Tarehe tano mwezi wa Septemba ni siku ya Hisani Duniani, iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kufahamisha na kuongeza uelewa wa watu binafsi, taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali Duniani kote kusaidia na kuwahudumia wengine kupitia kazi za kujitolea na shughuli mbalimbali za hisani. 

Tarehe 5 Septemba ilichaguliwa kuadhimisha kifo cha Mama Teresa, mfano wa utoaji, aliyepata Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1979, kama heshima ya juhudi zake za hisani na kibinadamu, ambapo alijitolea maisha yake kusaidia na kuwahudumia watu wasioweza na watu maskini, pia  kueneza Heri na Amani.