Chini ya Kauli Mbiu "Lugha za Alama Tuungane!" Umoja wa Mataifa Waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Alama Mwaka Huu
Imetafsiriwa na/ Habiba Mohammed
Imeharirwa na/ Mervat Sakr
Lugha za Alama ni lugha za asili zimezooneshwa kikamilifu ingawa kimuundo ni tofauti na lugha za hotuba zinazoishi pamoja, Kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Viziwi Duniani (World Federation of the Deaf Associations) zinazojumuisha takribani vyama 135 vya viziwi vya kitaifa, kuna viziwi wapatao milioni 72 duniani kote, wakitumia lugha zaidi ya 300 za ishara, na asilimia 80 kati yao wanaishi katika nchi zinazoendelea.
Wiki ya kwanza ya Kimataifa ya Viziwi iliadhimishwa Septemba 1958, na tangu wakati huo imegeuka kuwa harakati ya kimataifa yenye lengo la kuunganisha viziwi na kuongeza Ufahamu mkubwa wa masuala yao na changamoto za kila siku wanazokabiliana nazo, kuongeza Ufahamu wa umuhimu wa kulinda na kutekeleza haki za viziwi, kuheshimu Utambulisho wa lugha na Utofauti wa kitamaduni wa watumiaji wote wa lugha ya alama ulimwenguni, na kukuza Utambuzi wa haki yao ya kuitumia katika maeneo yote ya maisha, na mwaka 2018, Siku ya Kimataifa ya Lugha za Alama iliadhimishwa kwa mara ya kwanza chini ya azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 72/161, lililopitishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 2017 ndani ya muktadha wa shughuli za Wiki ya Kimataifa ya Viziwi.
Inashangaza kwamba kila nchi ina lugha yake ya alama inayotofautiana na nchi zingine, na kunaweza kuwa na lugha zaidi ya moja katika nchi moja. Lugha ya alama inatofautiana na nyingine kulingana na historia, Utamaduni na desturi za jamii na mazingira viziwi wanayoishi, lakini wale ambao wana Ufasaha katika kutumia lugha ya alama katika nchi moja wanaweza kuwasiliana kwa urahisi na watumiaji wa lugha ya alama katika nchi nyingine, tofauti na watumiaji wa lugha zinazozungumzwa. Pia kuna lugha ya alama ya kimataifa inayotambulika, ambayo hutumiwa na viziwi katika mikutano ya kimataifa na wakati wa kusafiri.
Hatimaye, na ili kupitisha kanuni ya "maoni yetu ni muhimu katika jambo lolote linalotuhusu", Umoja wa Mataifa ulisisitiza haja ya kutumia lugha ya alama katika kutoa huduma za msingi kwa kikundi hiki, ikiwa ni pamoja na elimu na mafunzo katika lugha ya ishara, kuchangia kwa Umakini, kwa nguvu na kwa Ufanisi katika maendeleo ya Ujuzi wa kundi hili la viziwi, ambalo lina athari wazi kuhusiana na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 Ulimwenguni.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy