Maadhimisho ya Miaka 54 ya Uhuru wa Swaziland

Maadhimisho ya Miaka 54 ya Uhuru wa Swaziland

Imetafsiriwa na/ Dalia Hassan 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Mnamo tarehe Septemba 6, 1968, Swaziland ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza. Tangu miaka ya themanini ya karne ya kumi na tisa, matarajio ya Waingereza na Uholanzi kudhibiti Swaziland na hamu yao ya kupata madini na dhahabu nchini ilikuwa imeanza. Mnamo Mwaka 1902, vita vilizuka kati ya Waingereza na Waholanzi, ambapo Waingereza walishinda na kuchukua udhibiti wa Swaziland peke yao.

Hatua ya Swaziland kuelekea uhuru ilianza kwa kupitishwa kwa katiba ya kwanza ya nchi hiyo mwaka 1964, ambapo Uingereza ilikabidhi madaraka kwa Swazis mwaka 1967 na Swaziland kupata Uhuru mnamo Septemba 6, 1968.

Ikumbukwe kwamba Mfalme wa Swaziland Miswati III aliamua mwaka 2018 kubadili jina la nchi yake kuwa "Eswatini" kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya hamsini, pia inayoambatana na Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Swaziland.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy