Dkt. Said Al-Batouti aandika: Utalii wa Milimani

Dkt. Said Al-Batouti aandika: Utalii wa Milimani

Imetafsiriwa na: Saga Ashraf
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Utalii wa milimani ni aina ya “shughuli ya utalii inayofanyika katika eneo maalumu la kijiografia lenye miundo ya kijiolojia kama vile vilima au milima yenye sifa na tabia za kipekee zinazoonekana katika mandhari ya asili, miinuko ya ardhi, tabianchi, utofauti wa viumbe hai (mimea na wanyama), pamoja na jamii ya wenyeji. Utalii huu unajumuisha shughuli mbalimbali za burudani na michezo ya nje ya nyumba.”

Utalii wa milimani una uwezo mkubwa wa kuchochea ukuaji wa uchumi wa ndani na mabadiliko ya kijamii kutokana na uhusiano wake na shughuli nyingine za kiuchumi, mchango wake katika pato halisi la taifa, na uwezo wake wa kuunda fursa za ajira. Aidha, utalii wa milimani una uwezo wa kuimarisha usambazaji wa mahitaji (kupambana na msimu) kwa wakati unaofaa katika kiwango cha kanda.

Ingawa utalii wa milimani ni kichocheo muhimu cha usafiri, data kuhusu ukubwa wake na athari zake bado ni nadra. Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Utalii la Dunia (UNWTO), utalii wa milimani unakadiriwa kuwakilisha kati ya 9% na 16% ya jumla ya watalii wa kimataifa wanaofika duniani kote, jambo linalotafsiriwa kuwa watalii milioni 195 hadi milioni 375 kwa mwaka 2019 pekee. Hata hivyo, uhaba wa data za kitaifa zinazohusiana na utalii wa milimani unafanya iwe vigumu au hata haiwezekani kutathmini athari za kiuchumi, kijamii, na kimazingira za aina hii muhimu ya utalii. 

Idadi ya watu wanaoishi katika milimani inakadiriwa kuwa bilioni 1.1, baadhi yao wakiwa miongoni mwa watu maskini zaidi na waliotengwa zaidi duniani. Wakati huo huo, milima imekuwa kivutio cha watalii wanaopenda asili, maeneo ya nje, na shughuli za nje kama vile kutembea, kupanda milima, na michezo ya msimu wa baridi. Pia, inavutia wageni kutokana na utofauti wake wa kibaolojia na tamaduni zake za kienyeji zenye shamrashamra. Hata hivyo, mwaka 2019, mwaka pekee ambapo takwimu zinapatikana, nchi kumi zenye milima mingi zaidi (kwa wastani wa urefu juu ya usawa wa bahari) zilipokea asilimia 8% tu ya watalii wa kimataifa wanaofika duniani kote."

Ingawa utalii wa milimani, ukifanywa kwa njia endelevu, utachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa mapato ya jamii za wenyeji na kusaidia kuhifadhi rasilimali zao za asili na utamaduni.

Kwa kutumia data sahihi, tunaweza kudhibiti vyema usambazaji wa mtiririko wa wageni, kusaidia mipango ifaayo, kuboresha ufahamu wa watalii, kuunga mkono mipango inayofaa, kuboresha uelewa wa mienendo ya watalii kwa kujenga bidhaa endelevu zinazolingana na mahitaji ya watumiaji, na kuweka sera zinazofaa ambazo zitaimarisha maendeleo endelevu na kuhakikisha shughuli za utalii zinafaidi jamii za wenyeji.

Kuzalisha manufaa ya kiuchumi na kuunda fursa kwa jamii za wenyeji, pamoja na kukuza bidhaa endelevu, ni vichocheo vikuu vya kukuza utalii wa milimani kwa njia endelevu ili uwe njia ya kusaidia kusambaza mtiririko wa watalii, kushughulikia msimu, na kukamilisha ofa za utalii zilizopo. Hakuna budi kuwa na juhudi za pamoja, zinazojumuisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi kutoka kote kwenye mfululizo wa thamani, ili kuboresha ukusanyaji wa data na kuziweka pamoja kwa njia bora ili kupata tathmini pana zaidi ya utalii wa milimani kuhusiana na ukubwa na athari zake, na ili kueleweka na kuendelezwa vyema kwa kuendana na malengo ya maendeleo endelevu. Hii itasaidia kuwa na ufanisi zaidi katika kusaidia jamii za wenyeji, kuunda fursa za ajira, kuunga mkono biashara ndogo na za kati, kuvutia uwekezaji wa kijani katika miundombinu, pamoja na kusaidia kuunga mkono matumizi na uzalishaji endelevu na kuhifadhi rasilimali asili.