Umoja wa Afrika | Siku ya Kimataifa ya  Viwanda Barani  Afrika 

Umoja wa Afrika | Siku ya Kimataifa ya  Viwanda Barani  Afrika 

Umoja wa Afrika | Siku ya Kimataifa ya  Viwanda Barani  Afrika 

Pamoja na kauli mbiu ya  "Kuifanya Afrika kuwa na Viwanda: Kuimarisha  Ahadi kwa ajili ya  Viwanda na  mseto wa Uchumi  wa Kina na Endelevu", sambamba na  Siku ya Kimataifa ya  Viwanda Barani Afrika, Niamey, mji mkuu wa Niger, wakaribisha  Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda na Mseto wa Kiuchumi, na hivyo mnamo mwaka huu, kuanzia 20 hadi 25 Novemba 2022.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilikuwa limeweka  tarehe 29 ,Novemba kila mwaka tangu Julai 1989 kuwa Siku ya Kimataifa ya Viwanda  ya Afrika, kwa mujibu wa Azimio (A/RES/44/237), na hiyo ilikuja ndani ya mfumo wa kuzindua Muongo wa Pili wa  Maendeleo ya viwanda Barani Afrika kati ya miaka (1991-2000), iliyopitishwa na kongamano la marais wa Nchi na Serikali za  Shirika la Umoja wa Nchi huru za Afrika, na imeshaanza kuadhimishwa tangu mwaka 2018 kwa tukio hilo  kwa wiki nzima ili kuongeza ufahamu kwa umuhimu wa ukuaji wa viwanda Barani  Afrika, na jukumu la mabadiliko ya kiuchumi katika kufikia malengo ya Ajenda ya Afrika ya 2063. 

Kwa mfumo huo , mkutano huo unalenga kuangazia azma ya Afrika na wajibu wake unaoendelezwa  kwa ajili ya kukuza viwanda  inayozingatiwa kuwa  mojawapo ya vichocheo vya kimkakati ili kufikia malengo ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara , kulingana na kile kilichoelezwa katika Ajenda ya Afrika 2063, na  kile kilichotiliwa mkazo na  Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu .

Ambapo mkutano huo wa kilele utajadili vipengele  kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na "njia za kutekeleza Mkataba wa Biashara Huria wa Bara la Afrika" kutokana na mahusiano wa kimsingi na wa kimkakati kati yake na ukuaji wa viwanda; na kipengele kingine   kilichohusiana na "Virusi vya Corona na njia mpya katika muktadha wa ukuaji wa haraka kwa viwanda"; Pamoja na kujadili "Mkataba wa Tatu wa Maendeleo ya Kiuchumi na Mpango wa Maendeleo ya Viwanda Afrika"; Pamoja na kujadili kipengele cha “Viwanda kwa Maendeleo Endelevu Barani Afrika”, hivyo  inakuja kwa lengo la kuongeza   ufahamu  wa mabadiliko ya kisiasa , rasilimali, makampuni na ushirikiano unaohitajika  kwa ajili ya maendeleo ya viwanda Barani Afrika,  jambo ambalo lingewawezesha wananchi kukidhi mahitaji yao ya kimsingi pamoja na  kukuza ukuaji  sekta ya  binafsi ya ndani, haswa katika nyanja za viwanda vya bidhaa nyepesi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alitoa wito kutokana na maadhimisho  ya siku ya viwanda Barani Afrika  kwa ajili ya juhudi  za  kujenga Afrika ziwe yenye ustawi zaidi, akisisitiza kuwa licha ya changamoto zinazolikabili Bara la Afrika, ikiwemo migogoro , majanga  na ukosefu wa   kiwango cha kifedha, ila  ina baadhi ya uchumi unaokuzwa kwa  haraka zaidi ulimwenguni . pamoja na uwezo wa kudhibitisha uhamisho wa nishati ulimwenguni . vilevile , alipendekeza kukuza ujasiriamali, kutumia uwezo wa teknolojia mpya, kupanuza fursa kwa vijana, wanawake na wasichana, kujenga uwezo wa kukabiliana na hali ya hewa na kuimarisha uwezo wa  ushindani na biashara, akiashiria umuhimu wa kufanya kazi  kwa pamoja ili kufikia malengo ya  kanda la Biashara Huria ya Bara la Afrika.