Taarifa ya Mshikamano wa Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa watu jasiri wa Algeria

Taarifa ya Mshikamano wa Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa watu jasiri wa Algeria

Leo,Tunaomba Mwenyezi Mungu  kwa ajili ya Algeria na raia wake, tukitamani Mwenyezi Mungu kuwanusuru Algeria kutoka moto kali uliyefikia majimbo 16 ya majimbo ya Algeria pamoja na moto mkubwa uliyezuka katika mji mkuu Algeria, tunaomboleza kwa masikitiko makubwa wahanga wa moto mkali, tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu awabariki kwa rehema zake kubwa na kuwasaidia familia zao na kuwapa subira katika msiba, na kupona jeraha za waliojerehewa  haraka,, na kuhifadhi Algeria na kusitisha moto uliyemiminika kila pahali pa nchi katika siku mbili zilizopita tangu Jumatatu jioni.

Tunathamini juhudi za nchi ndugu kuhusu misaada ziliyatoa kwa Algeria, zilizoisaidia kushinda msiba huo,  pia tunatangaza mshikamano wetu na watu wa Algeria katika hali hiyo ngumu, ambapo timu za kuzima moto ziko bado tukijitahidi kuuzuia moto huo, tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu awarehemu, awaongoze na Mungu alipe fidia kwa waliopotea familia, fedha na watoto, na Algeria kurudi kuwa na  Usalama na Amani.