Rasmi.. Chini ya Ufadhili wa Rais wa Jamhuri, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watangaza matokeo ya mwisho ya waombaji wa Misri kwa Ushiriki katika toleo lake la tatu 2022
Imetafsiriwa na: Saga Ashraf
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri, chini ya Ufadhili ya Dkt. Ashraf Sobhy, ilitangaza matokeo ya mwisho ya waombaji wa Misri kushiriki katika Udhamini wa Nasser katika toleo lake la tatu, unaokuja chini ya kauli mbiu "Vijana wasiofungamana na Upande Wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini", na ushiriki wa viongozi wa vijana wa 150 kutoka nchi zisizofungamana na upande wawote na za rafiki, umeopangwa kufanyika kutoka Mei 31 hadi Juni 17, 2022 huko Kairo.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unategemea marejeo na nyaraka kadhaa za kikanda na za bara, zikiwemo Hati ya Vijana wa Afrika, Ajenda ya Afrika 2063, pamoja na Kanuni za Bandung, Ramani ya Njia ya Umoja wa Afrika ya Uwekezaji kwa Vijana, pamoja na Maono ya Misri 2030, Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030.
Ni vyema kutajwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa toleo lake la tatu inakuja na ushiriki wa viongozi wa vijana wanaowakilisha nchi za 73 duniani kote, pamoja na ujumbe wa Misri ambao wanawakilisha sehemu kadhaa za jamii zinazolengwa na udhamini mwaka huu, ikiwa ni pamoja na matawi ya kitaifa ya Mtandao wa Vijana wa Harakati ya Kutofungamana na Upande Wowote, wakuu wa mabaraza ya vijana wa kitaifa, wajumbe wa halmashauri za mitaa, watafiti katika utafiti wa kimkakati na mizinga ya kufikiri, pamoja na wanachama wa vyama vya kitaaluma, Pamoja na wataalamu wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na wajasiriamali wa kijamii, pia uko chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi kwa mara ya pili mfululizo.