Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watangaza awamu ya Tatu na ya Kabla ya Mwisho ya Fainali za Washiriki wa Misri

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watangaza awamu ya Tatu na ya Kabla ya Mwisho ya Fainali za Washiriki wa Misri


  Leo, Jumapili asubuhi, Mei 22, 2022, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa umetangaza  orodha za awamu ya tatu na ya kabla ya mwisho ya Fainali za  washiriki wa Misri katika Udhamini huo, unaopangwa kuanzia Juni ijayo, kwa kushirikisha 
viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote, na nchi  rafiki, pamoja na Ufadhili wa Rais wa Jamhuri, Abdel Fattah El-Sisi.

  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , katika toleo lake la tatu mwaka huu, unachukua marejeleo kadhaa, kama vile Maoni  ya Misri ya 2030, Ajenda ya Afrika ya 2063, Mkataba wa Vijana wa Afrika, pamoja na ramani ya Umoja wa Afrika ya uwekezaji wa vijana, pamoja na Kanuni za Bandung, Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, kama hati za marejeleo ambazo Udhamini unategemea.

 Ikumbukwe kwamba Udhamini huo katika toleo lake la tatu, uliopangwa kuzinduliwa Juni ijayo 2022, unalenga kuangazia jukumu la vijana wasiofungamana kwa upande wowote katika kuamsha ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kutafuta njia za kuendeleza ushirikiano huo kupitia vijana kama nguvu yenye ushawishi na endelevu, pamoja na  kuzingatia jukumu la wanawake; Kwa hivyo, kauli mbiu ya Udhamini mwaka huu iko na "Vijana Wasiofungamana kwa Upande Wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini."

 Huu ni mwendelezo wa juhudi za Misri katika kutekeleza jukumu lake lililohusisha kuimarisha jukumu la vijana ndani, kikanda, bara na kimataifa.