Kituo cha Mafunzo ya Kiarabu-Eurasia 

Kituo cha Mafunzo ya Kiarabu-Eurasia 

Taasisi huru ya wasomi inayobobea katika masuala ya Eurasia, inayomaanisha Urusi, "Jamhuri za Umoja wa Kisovieti wa zamani" na mikanda inayoizunguka (Uchina, Uturuki, Iran, Afghanistan, Pakistan, Uhindi) na mahusiano yake na Marekani na Umoja  wa Ulaya. 

Kituo kinatafutia  kuchapisha karatasi za utafiti kuhusu Eurasia kuwa chanzo cha kuaminika kwa watoa maamuzi, waandishi wa habari, watafiti na wengine wanaopenda kusoma na kujua uwanja huo muhimu, na kuchunguza mambo ya ushawishi wa pande zote na eneo la Mashariki ya Kati, ili kusaidia waelewe vizuri zaidi kile kinachoendelea Duniani mnamo wakati muhimu, ambapo nidhamu mpya ya kilemwengu inaundwa, wakati unajitokeza - wakati huo huo - chaguzi za sera za kigeni zinazokabili ulimwengu wa Kiarabu. Kituo pia kinataka kujenga daraja la mawasiliano kati ya Waarabu na Eurasia ili kupata uelewa wa pamoja wa masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kihistoria. 

Kituo hicho pia kinajali na masomo ya "Geopolitics" ili kupata ufahamu wa kiini zaidi wa ushawishi wa Jiografia kwenye siasa, na kusoma mikondo mipya ya kisiasa "ya kihafidhi" inayoshuhudia kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo, na vile vile kutoa maudhui mbalimbali ya maoni na mitazamo yote inayohusiana na eneo la utafiti lililotajwa hapo juu bila kupitisha mtazamo fulani, itikadi fulani ya kisiasa, au kukuza taasisi fulani, wakitamani  kutoa vyanzo vinavyowezesha wale wanaovisoma kuelewa kwa misingi ya ukweli. 

Wakati huo huo, Kituo cha Mafunzo ya Kiarabu-Eurasia (CAES) hutoa kipaumbele maalum kwa masomo ya kijamii, ya kiutamaduni na ya kihistoria, pamoja na muundo wa kidini na kikabila na masuala yanayohusiana katika nchi za Eurasia, na athari zao kwa sera zao na mahusiano ya watu wao wenyewe, na mafungamano yanayowaleta pamoja na mazingira yao na ulimwengu wa Kiarabu. 

Katika suala hili, Kituo huanzisha uhusiano mkubwa na wasomi wengi, wanasiasa na viongozi wa juu wa serikali katika kambi ya Eurasia, ili kuelewa na kuwasilisha maoni yao na kuchambua utaratibu wa kufanya maamuzi ya kisiasa na nia zake. 

Pia, Kituo cha Mafunzo ya Kiarabu-Eurasia (CAES) huchapisha, kati ya machapisho yake mengine mbalimbali, gazeti la "Masuala ya Kiarabu-Eurasia" kila baada ya miezi mitatu, chapisho zake zinapatikana kwenye tovuti bure, ili kutoa maudhui ya kina kwa kuchambua matukio yanayozunguka eneo la Eurasia na uhusiano wake na ulimwengu kupitia maandishi ya viongozi maarufu wa fikra na wa kisiasa na maafisa, ambao wanalipa gazeti hilo makala za kipekee, ambazo Kituo kitayafasiri na kutayachapisha, na litasaidia yawe katika mikono ya watoa maamuzi na wale wanaopenda, nyenzo za uchambuzi zinazoendana na matukio ya mara kwa mara.

Marejeleo: 

Tovuti ya Kituo cha Mafunzo ya Kiarabu - Eurasia.