Udhamini wa Nasser kwa Uongozi katika toleo lake la tatu, washughulikia kuziwezesha nchi zinazoendelea

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi  katika toleo lake la tatu, washughulikia  kuziwezesha nchi zinazoendelea

 Kwa kukaribia kuanza kwa shughuli za kwanza za toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, uko kwa kichwa cha"Ushirikiano wa Kusini na Vijana wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote", hiyo ndiyo ni moja ya malengo ya Maendeleo Endelevu kwa 2030.

 Malengo ya kozi hiyo ya Ushirikiano ni kama ifuatavyo, kuongeza na kuboresha mawasiliano kati ya nchi zinazoendelea; inayosababisha kupatikana ufahamu zaidi wa matatizo ya pamoja na kuongeza upatikanaji wa ujuzi na uzoefu, pamoja na kuunda ujuzi mpya kuhusu kukabiliana na matatizo ya Maendeleo.

 Pia,toleo la tatu la Udhamini huo linashughulikia kuziwezesha nchi zinazoendelea kufikia kiwango kikubwa cha ushiriki katika shughuli za kimataifa za kiuchumi na kupanua ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya Maendeleo.
 Pamoja na kukuza uwezo wa kiteknolojia uliopo sasa katika nchi zinazoendelea, na kuhimiza kuhamisha teknolojia na ujuzi unaoendana nazo.
 Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa umepangwa kuanza  Mei 30 ijayo, na utaendelea kwa siku 15.