Harakati ya Nasser kwa Vijana ni Mkuu wa Muungano wa wanafunzi wa kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Sohag
Kiongozi mwanafunzi mwanaharakati "Mahmoud Labib", Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na katibu mkuu wa uratibu wa mkoa wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alishinda baada kushindana sana kwa uchaguzi wa nafasi ya Mkuu wa Muungano wa Kitivo cha Tiba ya binadamu, Chuo kikuu cha Sohag, uliofanyika kutoka Novemba 24 hadi Desemba 7 hii mwaka wa 2022.

Wasifu wa mwanafunzi kiongozi mwanaharakati wa Vijana "Mahmoud Labib" tangu utotoni mwake, ingawa umri wake mdogo lakini wasifu wake unajaa kwa mafanikio yenye athari kubwa kati ya jamii ya wanafunzi, na hatupitia kiasi tukisema kuwa ulianza kutoka vipindi vya kwanza vya darasa, ni miongoni mwao: kupata nafasi ya nne katika mashindano ya mwanafunzi bora katika ngazi ya Jamhuri ya 2015, na kisha kumteua kama katibu wa Muungano wa Wanafunzi wa shule za wanafunzi bora za Sayansi na teknolojia, mkoa wa Sohag mwaka wa 2016, kisha katika ngazi ya mkoa wa Assiut, mwaka wa 2017, pamoja na kujitolea kama mwezeshaji msaidizi katika kambi ya Elimu kwanza kwa viongozi wa vijana kutoka Microsoft, na"B-Tech" katika mwaka wa 2018, kisha kuchaguliwa kwake kama Rais wa kamati ya mahusiano ya umma, umoja wa wanafunzi, “Tahia Misr” mkoa wa Giza 2021, kisha katibu msaidizi wa kamati ya sayansi, Muungano wa wanafunzi wa Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Sohag cha 2022, kama alipata nafasi ya tatu kama mwanafunzi bora, Kitivo cha Tiba, Chuo Kikuu cha Sohag, mnamo mwaka huo huo, na mnamo Februari 2022 alihitimu katika mpango wa kitaifa "Mimi ni Mmisri ...Mimi ni Mwafrika" kujenga kada za wanafunzi katika masuala ya Afrika ndani ya mpango wa Afromedia, pamoja na usimamizi wa taasisi ya Afrika ya maendeleo na kujenga uwezo, na mnamo Machi, 2022 alipewa nafasi ya mratibu wa eneo la Afrika Kusini wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, pamoja na kushikilia cheo cha naibu mratibu wa kambi ya utafiti wa kisayansi na EBM, na pia alishiriki katika mkutano wa pili wa wanafunzi kwa ajili ya Misri katika vyuo vikuu vya Misri Huko Alexandria 2022.

Hayo ni pamoja na uanachama wake katika taasisi nyingi za ndani na za kimataifa za kisayansi, ikiwa ni pamoja na kuwa mwanachama wa Jumuiya ya kisayansi ya wanafunzi katika Kitivo cha Tiba katika Sohag "SMSA", na mwanachama anayeonesha katika timu ya Anactus katika Chuo Kikuu cha Sohag, basi mwanachama wa Bunge la vijana wa Misri ,2021 pamoja na uanachama wake katika ofisi ya mabadiliko ya Utamaduni na ushirikiano wa kimataifa katika taasisi ya vijana wa eneo la kati.
Kwa upande wake, Hassan Ghazali, Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, alielezea fahari yake kwa imani ambayo Labib anafurahia kati ya duru za wanafunzi, akisema, "tangu wakati wa kwanza, nilihisi kwa ukaribu sifa za kiongozi mwenye kuahidi, msomi, mwenye maoni wazi, Kijana mwanzoni mwa maisha ambaye hataki kuonekana wakati wote, hubeba hangaiko la wanafunzi wenzake akijaribu kuwasaidia kama kiungo kati yao na watoa maamuzi katika chuo kikuu, pamoja na upeo wake mpana wakati wa majadiliano mengi kwamba yeye alishiriki katika Harakati ya Nasser kwa Vijana, lililonihamasisha mimi kumteua katibu wa uratibu wa mkoa Harakati ya Nasser kwa Vijana, inayokadiriwa kwa mikoa 9 katika mabara 5 inayofikia nchi 65 Duniani kote," akisisitiza imani yake katika uwezo wake wa kufanya mabadiliko ya kweli ndani ya shirikisho ili kuamsha jukumu la umoja wa wanafunzi katika kufanya maamuzi ndani ya Chuo Kikuu.

Inatajwa kwamba "Labib" amehitimu katika kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, uliofanyika mnamo Juni 2021, pamoja na ushiriki wa viongozi vijana 110 kutoka nchi 53 kutoka mabara ya Asia, Afrika na Marekani ya Kusini, na kupitia kwake alishiriki kama msimamizi wa kikao kwa mahudhurio ya Balozi Sherif Issa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Balozi Amal Abdel Kader, msaadizi wa Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Asia, pamoja na usimamizi wa mheshimiwa Rais Abdel Fattah El Sisi, na katika mfumo wa kuwekeza katika nguvu za wahitimu wengi wenye ushawishi mkubwa na wanaojulikana kutoka kwa wahitimu wa Udhamini, alichaguliwa miongoni mwa timu ya Udhamini wa Nasser katika toleo lake la tatu, pamoja na Ufadhili wa mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi kwa mara ya pili mfululizo, ukiwa na kauli mbiu “Vijana wa kutofungamana kwa upande wowote na ushirikiano wa Kusini Kusini”.
