Rasmi.. Mjumbe wa Harakati ya Vijana ya Nasser apatia idhini ya BAKITA huko Tanzania kama mfasiri wa lugha ya Kiswahili

Rasmi.. Mjumbe wa Harakati ya Vijana ya Nasser apatia idhini ya BAKITA huko Tanzania kama mfasiri wa lugha ya Kiswahili
Rasmi.. Mjumbe wa Harakati ya Vijana ya Nasser apatia idhini ya BAKITA huko Tanzania kama mfasiri wa lugha ya Kiswahili

Mjumbe wa Harakati ya Vijana ya Nasser katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na mtafiti wa masuala ya Afrika, Shaima Tarek Jaber, amepatia ruhusa rasmi kama mfasiri na mkalimani wa Kiswahili kutoka kwa Kituo cha Kitaifa cha «BAKITA» huko Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hicho ndicho ni moja ya vituo vikubwa na maarufu vilivyoidhinishwa katika lugha za Kiafrika, na kinachohusika haswa katika lugha ya Kiswahili, inayoenea zaidi mashariki Barani Afrika.

Mhitimu wa Kitivo cha Al-Alsun, Chuo Kikuu cha Ain Shams, na mtafiti katika Idara ya Isimu ya Kiswahili, ShaimaTarek ni mfano mzuri wa kike, licha ya umri wake mdogo, ila aliweza kupiga hatua kubwa katika taaluma yake, amethibitisha ufanisi wake kama mfasiri wa  Kiswahili katika taasisi nyingi za vijana zinazohusika na masuala ya Afrika, na miongoni mwao: uanachama wake kama mfasiri wa lugha ya Kiswahili katika Harakati ya Vijana ya Kimataifa ya Nasser, mbali za kazi yake ya kufundisha na kufasiri Kiswahili katika vituo kadhaa vya utafiti, mbali na kazi yake inayojulikana katika nyanja ya vyombo vya habari kupitia kazi yake ya kujitolea katika gazeti la taifa la "Mwananchi" nchini Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Kituo cha Taifa cha Lugha ya Kiswahili «BAKITA» kilianzishwa mwaka 1967 kwa lengo la kusaidia, kuendeleza na kupanua uenezaji wa lugha ya Kiswahili, haswa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mbali na kuunga mkono matumizi yake katika hati rasmi za serikali, kwa kuhimiza taasisi za sekta ya umma na asasi za kiraia kutumia lugha ya Kiswahili katika kazi za maandishi na picha, Kituo hiki kimefanya kazi kwa miaka mingi kuratibu tafsiri na ukalimani katika lugha ya Kiswahili katika mikutano na makongamano ya kitaifa, na mnamo 1983  shughuli za Kituo hicho zilipanuka katika Barani Afrika, likikusudia kusaidia na kufuatilia ukuaji na kuenea kwa lugha sahihi ya Kiswahili, ndani na nje ya nchi.