Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika wapokea Kipaumbele Maalumu kwa Serikali

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika wapokea Kipaumbele Maalumu kwa Serikali

Imetafsiriwa na:Toka Mosaad Yusef
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Wizara ya Vijana na Michezo - inayoongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy - inathibitisha maslahi ya serikali na msaada kwa faili ya Afrika, katika utekelezaji wa kile Rais wa Jamhuri alitangaza wakati wa shughuli za Jukwaa la Vijana Duniani, lililoshuhudia uwakilishi wa heshima wa vijana wa nchi za Afrika, ambapo udhamini wa "Udhamini wa Nasser kwa Mabadiliko" uliotolewa na Utawala Mkuu wa Bunge na Elimu ya Uraia - Ofisi ya Vijana wa Afrika ilikuja wakati wa kipindi cha 8 hadi 22 Juni; ili kuonesha maslahi ambayo Serikali inashikilia, kuamini katika jukumu la vijana wa Kiafrika na umuhimu wa kuwapa aina zote za msaada, ukarabati na mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika nafasi za uongozi na kufaidika na uwezo na mawazo yao.

Katika muktadha huu, Mamlaka kuu kwa Habari ilipitisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika, kupitia bandari ya elektroniki iliyozinduliwa wakati wa urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, inayojumuisha tovuti nane kwa Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kichina, Kiswahili, Amharic na Hausa http://africa.sis.gov.eg/, Ilizinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo - inayoongozwa na Dkt. Ashraf Sobhi - katika utekelezaji wa mpango huo (1Million by 2021) kuhitimu vijana milioni moja wa Afrika na 2021, iliyozinduliwa na Tume ya Sayansi, Teknolojia na Rasilimali Watu ya Umoja wa Afrika hivi karibuni katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Mamlaka kuu kwa Habari pia ilichapisha udhamini kwenye tovuti yake rasmi http://www.sis.gov.eg katika lugha tatu: Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa, kupitia dirisha la elektroniki kwa udhamini unaojumuisha masharti ya uandikishaji na fomu yake ya usajili.

Ni muhimu kutambua kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kuwa udhamini unalenga viongozi wa vijana wa 100 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, watoa maamuzi katika sekta ya serikali, viongozi wa watendaji katika sekta binafsi, vijana wa asasi za kiraia, wakuu wa mabaraza ya vijana wa kitaifa, wanachama wa kitivo katika vyuo vikuu, watafiti katika utafiti wa kimkakati na vituo vya mawazo, wanachama wa vyama vya kitaaluma, wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, na wengine.

Udhamini huo unalenga kuhamisha uzoefu wa zamani wa Misri katika kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi wa mabadiliko ya vijana wa Afrika na maono, kulingana na maelekezo ya urais wa Misri wa Umoja wa Afrika na kuamini katika kutumikia malengo ya Umoja wa Afrika kupitia ushirikiano, pamoja na kuanzisha mkusanyiko wa viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa wa Afrika barani, na mafunzo muhimu, ujuzi na maono ya kimkakati.

Nasser pia ni udhamini ya kwanza (Afrika-Afrika) inayolenga viongozi wa vijana wa Afrika wenye taaluma tofauti ndani ya jamii zao, na ni mmoja wa wawezeshaji muhimu wa mabadiliko ya Afrika, yaliyoidhinishwa na maandiko ya Ajenda ya Afrika 2063.