Kikao cha mazungumzo kikiwa ns kichwa (Juhudi Za Jeshi La Misri katika kuunda makada wa kitaifa) miongoni mwa shughuli za siku ya 11

Kikao cha mazungumzo kikiwa ns kichwa (Juhudi Za Jeshi La Misri katika kuunda makada wa kitaifa) miongoni mwa shughuli za siku ya 11
Kikao cha mazungumzo kikiwa ns kichwa (Juhudi Za Jeshi La Misri katika kuunda makada wa kitaifa) miongoni mwa shughuli za siku ya 11
Kikao cha mazungumzo kikiwa ns kichwa (Juhudi Za Jeshi La Misri katika kuunda makada wa kitaifa) miongoni mwa shughuli za siku ya 11

Shughuli za siku ya 11 ya Udhamini zilihitimishwa na kikao cha mazungumzo kwa kichwa “juhudi za Jeshi la Misri katika kuunda makada wa kitaifa” na hivyo kwa mahudhurio ya Jenerali Dkt Khaled Fahmy, mshauri katika Kituo cha Mafunzo ya mkakati cha jeshi, kikao hicho kilisimamishwa na Esraa Akkad, mmoja wa washiriki katika Udhamini huo.

Jenerali Dkt. Khaled Fahmy alionesha juhudi za Jeshi la Misri kuunda makada katika nyanja mbalimbali, akiongeza Kuwa Misri ikiwa na Uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi ina jukumu alilopewa katika ngazi ya kikanda, inayoonekana wazi katika misaada inayoitoa katika nyanja mbalimbali kwa nchi za Afrika ndani ya bara,

 "Fahmy"alisifu jukumu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi  wa Kimataifa katika mafunzo na ukarabati wa vijana na kuhakikisha ushirikiano wa vijana wa pamoja kati ya mabara matatu ya Afrika, Asia na Amerika ya kusini, haswa mnamo kipindi cha hivi karibuni ambapo Misri imekuwa mahali pa kimataifa kuandaa matukio mengi ya kimataifa ya vijana.

"Fahmy" alionesha juhudi za vikosi vya jeshi katika maandalizi ya makada, ambapo alizungumzia  juhudi za taasisi za Uongozi mkuu wa jeshi, miongoni mwake jukumu la mamlaka ya Tafiti za kijeshi na Chuo cha juu cha kijeshi cha Nasser katika kuandaa makada kupitia mazoezi pamoja na kuonesha jukumu vikosi vya ukinzani na vya jeshi, Akisisitiza Kuwa Jeshi la Misri lina vifaa vingi vinavyohakikisha lengo rasmi la Misri linalohusiana na ujenzi na ukarabati wa makada wa binadamu katika nyanja mbalimbali na vitengo, ikiwa ni pamoja na kitivo cha Kijeshi Kiufundi, Chuo cha  juu cha kijeshi cha Nasser na Vyuo vya lugha na ufasiri.

"Fahmy" alisisitizia Uangalifu wa vikosi vya jeshi la Misri la kuandaa makada na kujenga na kuendeleza uwezo wao wa kisayansi na kiteknolojia kulingana na mikakati sahihi na kwa kutumia wenye maarifa kupitia ukarabati wa makada wa binadamu wana uwezo wa uvumbuzi, maendeleo, ubunifu na kushughulika na vifaa vya kisasa na mwelekeo wa kudumu kuelekea maendeleo ya kuboresha uwezo wa kupigana kwa silaha na vifaa kwa kiasi kinachohakikisha uwezo wa kuhakikisha kufanikiwa na usawajiko na teknolojia ya ulinzi wa kimataifa na kuhakikisha matakwa ya kuhifadhi na kulinda nguzo za usalama wa kitaifa wa Misri kwenye viwango na pande zote pia alipongeza uzoefu wa ushirikiano kati ya nchi katika uwanja wa kiuchumi, linalomfanya raia ahisi uzoefu na matokeo ya maendeleo ya kiuchumi ambayo hufanyika kati ya nchi na nyingine, na alisisitizia umuhimu wa jukumu la Umoja wa Afrika kupambana na mashambulizi ya kigaidi kupitia Baraza la Amani na Usalama la Afrika pamoja na ushirikiano na mshikamano kati ya nchi kupambana na mashambulizi ya kigaidi.

 Washiriki wa Udhamini walitoa  maswali, maulizo na majadiliano kwa Jenerali Dkt. Khaled Fahmy na kikao kimehitimishwa kwa kupiga picha za kumbukumbu na washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  ikifuatiwa na aya ya kiufundi huku kukiwa na ushirikiano mkubwa na furaha kutoka kwa washiriki.