Wizara ya Vijana na Michezo yajiandaa kuzindua toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Imefasiriwa na / Mervat Sakr
Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri inajiandaa kuzindua Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, linalotarajiwa kufanyika Juni ijayo pamoja na kauli mbiu ya "Vijana Wasiofungamana kwa Upande wowote, Ushirikiano wa Kusini - Kusini", kwa ushiriki wa Vijana 150 wa kiume na wa kike Duniani kote.
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi ni mojawapo ya mifumo ya utendaji wa mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa kukuza wenye ufanisi wa Vijana waafrika, kuwawezesha kuunda maoni kamili na muhimu yanayohusiana na masuala ya kimataifa na mipango ya maendeleo endelevu, na kusaidia fursa za kukuza jukumu la Misri Duniani, na inakuja ndani ya mfumo wa kutekeleza maoni ya Misri ya malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda ya Afrika 2063, na Mkakati wa Ushirikiano kwa ajili ya Kusini- Kusini.
Ikumbukwe kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi lilitekelezwa mnamo Juni 2019 pamoja na uangalifu wa Mheshimiwa Waziri Mkuu Dkt. Mustafa Madbouly, kukamilisha juhudi za serikali ya Misri katika kuimarisha jukumu la Vijana wa Afrika kupitia mafunzo, ukarabati na uwezeshaji katika nafasi mbalimbali za uongozi, na jukumu la serikali ya Misri katika kufikisha na kuwawezesha vijana waafrika, na ndani ya muktadha wa wito wa Rais El-Sisi wa kutekeleza Mpango wa Umoja wa Afrika 2021 wa kuandaa Vijana milioni moja kwa ajili ya uongozi, uliozinduliwa wakati wa shughuli za Jukwaa la Vijana Duniani katika toleo lake la pili 2018 na toleo lake la tatu 2019; ambapo Toleo la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi lilitekelezwa mnamo Juni 2021 na kupanuliwa kujumuisha viongozi wa vijana kutoka Asia, Amerika ya Kusini na Afrika.
Baada ya sifa pana za kimataifa na mafanikio makubwa ya Toleo la pili, Toleo la tatu lilifanyikwa Juni 2022, na fomu ya usajili imepangwa kuzinduliwa kwa Vijana wanaotaka kuomba Udhamini katika Toleo lake la nne mnamo kipindi kijacho.