Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili jukumu la jamii ya kiraia

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wajadili jukumu la jamii ya kiraia


Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  ulimkaribisha Anba Joseph, Askofu Mkuu wa Afrika na anayehusika na nchi za Malawi, Namibia, Zimbabwe na Botswana, katika kikao cha majadiliano, kilichofanyika mchana wa siku ya kumi, chenye kichwa cha "Jukumu la Jamii ya Kiraia", ambapo Anba Joseph, Askofu Mkuu wa Afrika, alizungumza kwa mahudhurio ya Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa,Ahmed Al- Sabbagh, mwakilishi wa kikanda wa utawala, Amani na Usalama katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Kikundi Kikuu cha Vijana cha Umoja wa Mataifa,Dkt. Sameh Kamel, Mkuu wa Kundi Kuu la Umoja wa Mataifa la Watoto na Vijana, na kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, wanataaluma wa habari na waandishi.

Anba Joseph, Askofu Mkuu wa Afrika, alianza hotuba yake kwa maneno ya Papa Tawadros II, Papa wa Aleksandria na Patriaki wa Kanisa la Kiothodoksi la Kikoptiki, kwamba “nchi bila makanisa ni bora kuliko makanisa bila nchi, na kwamba Misri sio nchi tunayoishi lakini ni nchi inayoishi ndani yetu" "Askofu Mkuu wa Afrika" alidai Vijana washiriki Katika Udhamini huo kwamba ni muhimu kuacha vitu vidogo ili kuhakikisha malengo ya juu na kushinda vikwazo vinavyozuia Umoja wa  jamii.


Pia "Joseph" alionesha jukumu la Kanisa la Kikoptiki la Misri katika nchi mbalimbali za kiafrika, na linalochukuliwa kuwa mojawapo ya Balozi za Misri nje ya nchi, na lina jukumu muhimu la maendeleo katika nyanja zote za maendeleo ya jumla, pia lina  jukumu kubwa katika uamsho wa jamii kupitia kuanzisha hospitali, nyumba za utunzaji na ukarabati katika baadhi ya maeneo, maeneo ya maji na nishati ya jua, pamoja na kile inachofanya kwa kutoa Programu za kuwawezesha wanawake akielezea matumaini yake ya kuanzisha shule za ufundi na viwanja vya michezo vinavyohudumia vijana na kukuza ujuzi wao.

Viongozi vijana washiriki waliuliza maswali kadhaa kwa Anba Joseph, Askofu Mkuu wa Afrika, halafu washiriki wakapiga picha za kumbukumbu wakati wa mwingiliano na  uchangamfu mkubwa  kutoka kwa kila mtu kwa kikao hicho muhimu cha majadiliano kilichofanyika miongoni mwa shughuli za Udhamini.