Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa uko na Ufadhili wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uandishi wa Habari
Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, ambao uko na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa mwaka wa tatu mfululizo, ulipata Udhamini wa kimaandishi kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Uandishi wa Habari, ambapo Mamlaka hiyo itashughulikia yote yanayohusu Udhamini mnamo kipindi kijacho kama maandalizi ya kuzinduliwa kwake Juni 2023, pamoja na kauli mbiu isemayo "Vijana wasiofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini".
Udhamini huo hapo awali ulikuwa umepata vingi sana vya uandishi wa habari kitaifa na kimataifa pia kwa lugha kadhaa kama ; Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili,,Kihispania, na Kiarabu, pamoja na majadiliano ya washiriki na kupanuka habari zake kupitia mitandao ya kijamii.
Na kwa upande wake, Hassan Ghazali, Mwanzilishi na Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa aliashiria kuwa Udhamini huo kwa matoleo yake yote umepata maandishi ya habari yafikapo Tovuti 112 za Kihabari za ndani, pamoja na zaidi ya Tovuti 27 kwa lugha za kigeni,na maandishi mengi sana katika Magazeti ya kimaandishi kutoka magazeti ya kitaifa ya kimisri maarufu zaidi kama Al Ahram,Al Masri Al Youm, Al Jomhuria, Al Watan, Akhbar Al Youm,Rose Al Yusuf,Al Masaa, Al Wafd, Al Destoor, Al Youm Al Sabe,pamoja na nakala ya kimaandishi ya Gazeti la Egyptian Gazet litamkalo kwa Kiingereza.