Wanawake na tasnia ya Vyombo vya Habari huko nchini Tanzania wakiwa kwenye meza ya “Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa”

Wanawake na tasnia ya Vyombo vya Habari huko nchini Tanzania wakiwa kwenye meza ya “Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa”

Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa (Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa kwa Kiswahili) umeandaa kikao chake cha saba kwa anwani ya “Baada ya  Kesho ya Tanzania: Jukumu la Vyombo vya Habari na Wanawake katika Kuunda Kesho ”,  haya yamekuja sambamba na Sikukuu ya Kitaifa ya Tanzania, ambapo mnamo Desemba pamoja na kuhudhuria Wanafunzi, Watafiti, na Wanataaluma wa Vyombo vya Habari wanaohusika na masuala ya kiafrika.

Mgeni wa kikao hicho alikuwa Meneja wa Mawasiliano wa TAMWA Bi. Sophia Ngalapi ambaye alizungumzia jukumu la vyombo vya habari katika kuunda maoni ya wananchi na kuelimisha jamii akisisitiza kuwa vyombo vya habari vina jukumu kuu katika kufungua Tanzania na dunia. Pia akidokeza athari za kiteknolojia ya kisasa na vyombo vya habari vya kidijitali katika kuwasilisha sauti ya watu na kufuatilia masuala ya kijamii.

Vilevile Bi.Ngalabi amesisitiza jukumu la vyombo vya habari katika kuzuia kusambaza habari ghushi kwa njia ya  kuhakikisha vyanzo vya habari na kutoa uchambuzi wa kina, pia akipongeza juhudi za taasisi za Tanzania katika nyanja hii. Alieleza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuongeza uelewa wa kitaifa na kukumbusha matukio muhimu kama vile: Maadhimisho ya Miaka ya Uhuru wa Tanzania.

Kwa upande mwingine, Bi.Sophia ameelezea uzoefu wake kama Mwandishi wa Habari na Mwanaharakati wa Masuala ya Wanawake, akiashiria mabadiliko chanya yanayoshuhudiwa katika haki za wanawake wa Kiafrika, ambayo yalimwezesha kushiriki kikamilifu katika nyanja zote za maisha, sawa ya  kitaaluma ama kifamilia, akilisisitizia jukumu lake muhimu katika kujenga jamii.

Kwa upande wake Dkt. Edelfrida Tibaji, Afisa wa Programu za Utamaduni na Lugha katika Tume ya Taifa ya UNESCO huko nchini Tanzania, alisema  akisisitiza jukumu la vyombo vya habari katika kujenga uelewa wa wananchi watanzania katika masuala ya Uhuru wa Kitaifa, na vilevile akipongeza jukumu la vyombo vya habari katika kuandika historia na kuhamasisha uungwaji mkono kwa masuala ya kitaifa.

Mtafiti Mwanthropolojia, Bw. Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, aliongeza kusisitiza jukumu la vyombo vya habari kuwa nyenzo kuu katika kuhifadhi turathi za kitamaduni na kiisimu na kuimarisha utambulisho wa kitaifa, akieleza kuwa vyombo vya habari si njia ya kusambaza habari tu, bali pia ni kama daraja la mawasiliano kati ya wanajamii. Akiongeza kuwa nafasi ya wanawake katika vyombo vya habari vya Tanzania inachukuliwa kama mfano wa kuheshimika wa kuangazia maadili na mila za kitamaduni zinazochangia kujenga jamii yenye mshikamano, akieleza kuwa kusaidia na kuwawezesha wanahabari wa kike kuongezea uwezo wa vyombo vya habari kwenye kuendana na changamoto za kimataifa, sambamba na kuhifadhi utambulisho wa ndani,  pia Bw. Ghazaly alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya vyombo vya habari na taasisi za kitamaduni ili kutoa maudhui ambayo yanaakisi utofauti wa kitamaduni na kuangazia nafasi ya wanawake kama  mhusika mkuu kwenye kujenga mustakabali.

Mtafiti, Mfasiri na Mratibu wa Toleo la Kiswahili la programu hiyo, Bi. Nourhan Khaled aliyeongoza kikao hicho, amesisitiza jukumu kuu la Programu ya “Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa”  katika kuimarisha mwingiliano wa kitamaduni na vyombo vya habari kati ya Misri na watu wanaozungumza Kiswahili,  kuimarisha Uelewa wa Kitamaduni kati ya watu, na kufungua nafasi za mazungumzo kuhusu masuala yanayoathiri mustakabali wa jamii Katika nchi za Ulimwengu Kusini. Washiriki walisisitiza kuwa mpango huo unajumuisha maono ya Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa na juhudi zake za kujenga madaraja ya mawasiliano na ushirikiano kati ya tamaduni kadhaa, na kuongeza nafasi ya vyombo vya habari katika kukuza maadili ya mshikamano na maendeleo endelevu.

Wahudhuriaji pia walipongeza juhudi za Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa katika kusaidia vijana na wanataaluma ya habari ili kukuza ujuzi wao na kuwawezesha kuwa hai katika kuunda maisha yajayo, na kubainisha umuhimu wa vikao hivyo kuendelea kujadili masuala ya kimsingi yanayozifunga jamii za Kiafrika katika maisha ya baadaye moyo wa mshikamano na kazi ya pamoja.