Mshikamano wa Kimataifa wajadili Jukumu la Vituo vya Kitamaduni kwenye Kufufua Urithi wa Lugha
Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa umeandaa kipindi cha nne cha mfululizo wa vipindi vya Programu ya Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa (toleo la Kiswahili), chini ya kichwa: "Nadharia za Chimbuko la lugha ya Kiswahili tangu mwanzo wa kuanzishwa kwake hadi siku hizi: Jukumu la Bakita kwenye Ufufuo wa Urithi wa Kiisimu".
Kipindi hicho kilishuhudia uwepo wa kundi la watafiti katika lugha za Kiafrika, kati ya Misri na Tanzania, na kwa kuhudhuria ya Dkt. Hamisi Aly Matembelea, Mwalimu wa Kiswahili kwa wazungumzaji wasio wa asili, ameyeidhinishwa na Kituo cha Kimataifa cha Kiswahili Bakita na Mtaalamu wa Lugha katika Balozi za nchi kadhaa, Bi. Edelfrida, Mtaalamu wa Kiswahili, Idara ya Lugha kwenye Tume ya Taifa ya UNESCO nchini Tanzania, na Dkt. Mohamed Abdel Rahman Attia, Mhadhiri wa Lugha ya Kiswahili kwenye Idara ya lugha za Kiafrika, Kitivo cha Lugha na Ufasiri, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na Msimamizi wa Lugha za Kiarabu, Kituo cha Al-Azhar kwa kupambana na fikra potofu.
Kipindi hicho kilifunguliwa na Dkt. Hamisi Matembelea akihutubia hadhira kwa kurejelea umuhimu wa lugha ya Kiswahili ambapo kikao hicho kilishuhudia mjadala wa kina kuhusu chimbuko la lugha ya Kiswahili na nadharia zake.
Dkt. Mohamed Abdul Rahman aliongeza maelezo hayo kwa mifano ya kanuni za lugha kuonyesha ushahidi na hoja kuhusu lugha hiyo na kwa kauli moja wamekubaliana kuwa Kiswahili kimechukua na kukopa maneno mengi kutoka lugha nyingine hasa lugha za kikoloni kama vile Kiingereza, Kijerumani, Kihindi na nyinginezo, huku lugha ya kiarabu ikiwa na sehemu ya simba ya kukopa hiyo, kutokana na kuanza kuandika Kiswahili kwa herufi za Kiarabu, na kurudi nyuma kwa ukweli kwamba sayansi ya asili ya uandishi ni Waarabu, pamoja na jukumu la dini ya Kiislamu katika jambo hilo.
Katika muktadha unaohusiana, Hamisi Matembelea alielezea jukumu muhimu lililotekelezwa na Kituo cha Lugha cha Bakita kwenye kuhifadhi Urithi wa Lugha kupitia machapisho yake ya vitabu na kamusi nyingi ambazo hutumika kama kumbukumbu ya Kiswahili, akieleza kuwa baadhi ya matoleo pia huhifadhi asili ya maneno ikiwa ni lugha iliyokopwa au la, na kumbuka kuhusu lugha gani neno hilo lilichukuliwa.
Mwanaisimu Bi. Edelfrida alitoa maoni yake katika hatua muhimu iliyokatiza utata huo akisema: "Lugha ya Kiswahili imepata maneno mengi kutoka kwa Kiarabu, na sifa hiyo inatokana na Kiarabu kuchukua maneno mengi.
Kwa upande wake, Mwanaanthropolojia na Mwanaharakati wa kimataifa Hassan Ghazaly, Mwanzilishi na Mkuu wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, alisisitiza haja ya taasisi na watu binafsi kusaidia vituo vya kitamaduni kama vihifadhi vya urithi na kuongeza juhudi zao za kuhifadhi urithi wa lugha, kuimarisha utambulisho wa kitamaduni wa mataifa, na kuhamasisha jamii kusherehekea Urithi wao wa Kipekee, akibainisha kuwa juhudi hizi ni sehemu muhimu ya maono ya Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa ili kukuza uelewa na utofauti wa kitamaduni wa watu duniani kote. Kupitia ushirikiano kwenye miradi ya mipango ya kitamaduni inayoheshimu wingi wa kitamaduni na lugha.
Kikao hicho kilisimamiwa na Mfasiri na Mtafiti Nourhan Khaled, Mratibu wa toleo la Kiswahili la Programu ya Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa, na Mhariri Mkuu wa Lango la Makala na Maoni ya Kiswahili, kwenye Tovuti Rasmi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana.
Mwishoni, wageni na washiriki walisifu jukumu la ufanisi lililochezwa na Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa ulimwenguni, na athari zilizopatikana na Mpango wa Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa, katika kuleta pamoja maoni ya wageni, akionesha kuwa mpango huo ni kiungo kilicholeta pamoja mataifa mengi duniani kote katika sehemu moja ya kuingiliana na kila mmoja katika mazungumzo ya pamoja. Pia walipongeza juhudi za Harakati ya Nasser ya Kimataifa kwa Vijana katika kutoa fursa nyingi kwa wanafunzi na watafiti, na uwezo wake wa kujenga makada wa vijana wenye uwezo wa kuendana na mahitaji ya soko la ajira, na kujua changamoto za kimataifa.