VIDEO| Utaratibu wa Kiafrika wa Kutathmini Rika (APRM) waadhimisha miaka minne tangu kuanzishwa kwa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana

 Katika mazingira yaliyojaa uchangamfu na shauku kwa ushindi mtawalia kwa wanachama wa African Peer Review Mechanism, ambao ni viongozi wa vijana Barani Afrika, Bw.Lennon Monyae, Afisa wa Masuala ya Vijana katika APRM, alitoa pongezi kubwa kwa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana kwa kupita miaka minne tangu kuanzishwa kwake, ambapo hayo yalitokea pembezoni mwa kongamano la kwanza la mashauriano kwa vijana waafrika, lililofanyika katika Ufalme wa Morocco, likienda sambamba na sherehe za watu huru wa miaka sabini ya Mapinduzi matukufu ya Julai. 

 Katika muktadha unaohusiana, Bw.Lennon Monyae alisisitiza kwamba Harakati ya Nasser kwa Vijana ina jukumu muhimu katika kukuza ukamilifu wa kikanda na bara, haswa katika kiwango cha sekta ya vijana, akiashiria kile ambacho Harakati  ya Nasser kwa Vijana imekuwa ikifanya kazi katika kuunganisha kanuni za Muungano wa kiafrika, pamoja na nafasi yake kubwa ya kuwaunganisha vijana wa Dunia kupitia matukio, semina, mikutano na makongamano inaozinduliwa nayo, pamoja na programu za mafunzo kwa kutumia njia za kiteknolojia, kisha akamaliza akisema :" Idumu Afrika...Idumu Afrika kuelekea Ushirikiano wa kikanda."

 Kwa upande wake, Bw.Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Harakati ya Kimataifa  ya Nasser kwa Vijana, na kiongozi wa timu ya mawasiliano na vyombo vya habari katika African Peer Review Mechanism akiwakilisha ukanda wa Afrika Kaskazini, alielezea furaha yake na majibu ya bara kutoka kwa watoa maamuzi na wanadiplomasia kuhusu athari hai za Harakati hiyo kati ya  vijana, haswa viongozi wa vijana katika Mfumo wa Kupitia rika la Kiafrika, akionesha nia ya APRM ya kuwaunganisha vijana kutoka bara zima katika mifumo yake ya kazi, akisisitiza kwamba ni hatua ya karibu ya kuunganisha dhana na utamaduni wa uongozi wa mabadiliko Barani Afrika, akionesha nia ya Harakati ya Nasser kuimarisha utawala na kueneza kanuni za utawala bora, kama moja ya Misingi muhimu zaidi katika kufikia Maendeleo Endelevu.

Ghazaly pia alielezea furaha yake na Shukrani zake za dhati kwa Profesa Eddie Maluka, Mkurugenzi Mtendaji wa African Peer Review Mechanism, kwa kumchagua katika nafasi hii kama kiongozi wa timu ya kimataifa ya mawasiliano na vyombo vya habari, akiwakilisha ukanda wa Afrika Kaskazini, akiwa na kina la " APRM Regional Communication Champion", akieleza msaada wa APRM, na ushiriki wake katika Matukio na shughuli nyingi anazozizindua.

 Katika muktadha unaohusiana, "Ghazaly" alieleza kuwa katika nafasi yake kama kiongozi wa timu ya kimataifa ya vyombo vya habari, alishiriki kama mzungumzaji katika Mkutano wa Wakuu wa Ushirikiano wa Afrika wenye uwakilishi wa hali ya juu wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, pamoja na  kauli mbiu "Kujenga Jamii Imara na thabiti Barani Afrika na Global South", Desemba 2021, pamoja na ushiriki wake katika kuzingatia vyombo vya habari kwa matukio na mikutano mingi iliyofanywa na Mechanism, ikiwa ni pamoja na Jukwaa la Vijana la Bara la Kujadili Utawala wa Kidijitali, Biashara ya Kidijitali, Usalama na Haki za Kidijitali, Desemba 2021, na Jukwaa la Amani na Kuzuia Migogoro Barani Afrika, kwa ushirikiano na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Desemba 2021, pamoja na Jukwaa la 31 la Mataifa na Serikali, ambalo lilifanyika Februari 2022.

 Mwishoni mwa hotuba yake, Ghazaly alisisitiza kazi ya utaratibu wa kuunganisha maadili ya demokrasia, utawala bora, na heshima ya haki za binadamu Barani Afrika, akiashiria kukaribishwa na msaada kamili wa Misri kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya hatua za pamoja za Afrika. na ari ya Misri ya kujitolea kutekeleza malengo ya maendeleo ya Afrika, akionesha kwamba Misri imefikia karibu 45% ya matarajio ya Agenda 2063, na hilo ndilo lililothibitishwa na Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi alipokutana na ujumbe wa African Peer Review Mechanism, Februari jana 2022.