Wasichana wa Harakati ya Nasser kwa Vijana wako na mafanikio Barani sambamba na Mwezi wa Wanawake
Menna Yasser na Zapora Moriba, Viongozi wasichana maarufu sana wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, wameshinda "Tuzo ya wanawake Wa Afrika kwa Uongozi" katika nyanja za Elimu, Utetezi wa haki za wasichana na uwezeshaji wa wanawake.
Mmisri Menna Yasser anafanya kazi kama Mratibu mkuu na mhariri wa Idara ya lugha ya Kiswahili ya Harakati ya Nasser kwa Vijana, Mtangazaji wa Redio ya mtandaoni na Mkalimani wa mashirika kadhaa ya kimataifa, pamoja na kazi yake kama Mkurugenzi wa sekta ya matibabu huko Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayo yote mbali na yeye ni mmisri wa kwanza anayeandikia kitabu cha Kiswahili kiitwacho NJIANI, katika uwanja wa kujiendeleza na Maendeleo ya Binadamu, pamoja na Kitabu chake cha pili kiitwacho Karatasi Na Kalamu ndicho ni Hadithi Fupi, hiyo ndiyo iliyomfikisha kushinda tuzo hiyo katika uwanja wa Elimu.

Wakati ambapo Zapora Moriba, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na Mratibu wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Sierra Leone, anafanya kazi ya kuwawezesha wanawake na kutetea wasichana na bila starehe yoyote anatetea maoni yake ya kupatikana Dunia sawa, yenye haki, iwe na ustahimilivu na uendelevu, ambapo wasichana na wanawake vijana huwezeshwa kufurahia haki zao za kimsingi na kuwekeza katika nguvu zao ili kuchangia mabadiliko chanya katika ulimwengu wetu huu.

Ikumbukwe kuwa tuzo ya "Wanawake wa Afrika kwa Uongozi" huzinduliwa na Mpango wa Viongozi Vijana wa Afrika, mnamo mwezi wa Machi kila mwaka, sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kwa kutoa tuzo kwa wasichana 50 wenye ushawishi Barani Afrika katika nyanja takribani 10, kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35, na miongoni mwa maeneo yanayolengwa na tuzo hiyo ni : Afya, Elimu, Shughuli za Hali ya hewa, Maendeleo ya Mazingira, Kilimo, Vyombo vya Habari na Michezo, na miradi inayohusiana na kuilinda Jamii.