Maandishi ya "Abu shanab" Mhitimu wa Udhamini wa Nasser katika maonesho ya Kitabu ya Kairo ya kimataifa 2021
Harakati ya Nasser kwa Vijana inatangaza kuchapishwa kwa Maandishi ya Mtafiti na mwandishi wa habari "Mohammed Abu Shanab", mwandishi wa Habari katika Gazeti la Al-Jumhuriya, na Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na mshindi wa Tuzo ya kuhamasisha ya serikali kwa moja ya vitabu vyake "tunboura stringed machine" kwa mwaka wa 2021.
Ambapo “Abushanab " anashiriki mwaka huu katika maonesho ya Kitabu Kairo ya kimataifa , na vingi vya vitabu vyake maalumu katika uwanja wa Urithi wa Utamaduni, iliyotolewa na nyumba ya utambulisho wa utamaduni na taasisi ya Rawaee kwa kwa Utamaduni, Sanaa na Urithi.
Maandishi hayo yanajumuisha kitabu kinazungumzia tabia na desturi za watu zinazohusiana na kipindi cha kuzaliwa, ndoa na kifo, kitabu kingine kuhusu maelezo ya ala ua tunbora ya nyuzi, kama vile kitabu kuhusu "kukusanya vyanzo vya Urithi wa kienyeji kutoka vitabu vya wasafiri na wenye elimu ya nchi za mashariki Katika Misri Nubia".
Ikumbukwe kwamba mnaweza kununua vitabu hivyo na kuvisoma kwa kutembelea Hall Na. (2)C41 Katika maonesho ya Kitabu ya kairo ya kimataifa, yanayofanyika kituo cha Misri cha maonesho ya kimataifa, Fifth Settlement, ambapo maonyesho yalianza tangu Juni 30 iliyopita na yaliendelea hadi Alhamisi, Julai 15.