Mhitimu wa Udhamini wa Nasser yuko kwenye mkutano maalum na Jumuiya ya Afrika huko Kairo
Leo Jumatatu, Juni 21, 2021, Kijana wa Tunisia, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi na kwa kauli mbiu " Ushirikiano wa Kusini Kusini" na pia ni mkufunzi wa kimataifa katika elimu ya kitaifa na mratibu mmoja wa harakati ya Vijana ya Nasser nchini Tunisia " Yasser Fathly" anashiriki kama mkurugenzi wa kikao kilichoandaliwa kwa shirika la " Jusoor " la vijana la ofisi ya Misri kwa kushirikiana na Umoja mkuu wa wanafunzi wa Afrika nchini Misri kwa anwani ya " kuimarisha uwezo wa jamii ya Misri na Afrika katika kuunda miradi ya jamii na nafasi yake katika kuhakikisha malengo ya Maendeleo Endelevu " .
Ni vyema kuashiria kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unawalenga viongozi vijana ambao wana taaluma ya utendaji mbalimbali na vijana hai na wenye ushawishi katika jamii ya kiraia, pamoja na ni moja ya njia ya kutekeleza Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu kuwekeza katika Vijana, na pia kutekeleza ushiriki kwa ajili ya Kusini _ Kusini katika mabara matatu: Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.