Dola elfu tano za kimarekani kama tuzo kwa mhitimu wa Udhamini wa Nasser kutokana na Uadilifu na kupambana na Ufisadi

Dola elfu tano za kimarekani kama tuzo kwa mhitimu wa Udhamini wa Nasser kutokana na Uadilifu na kupambana na Ufisadi

Wahamiaji wa Chad nchini Marekani wanamheshimu Ahmat Larry, mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Jumuiya ya wahamiaji wa Chad nchini Marekani ilimheshimu mwanaharakati wa Chad, Ahmat Haroun Larry katika kituo cha utamaduni cha Alumni  kwa kumpa Sanamu ya Uhuru ambayo thamani yake inafikia dola elfu tano za kimarekani kama tuzo ya Uadilifu na kukabiliana na Ufisadi nchini Chad, tuzo hiyo  inayopewa kwa mara ya kwanza kwa mwanaharakati mtaani nchini Chad.

Larry ni mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili, ambayo kupitia kwake aliangalia uzoefu wa Misri wa ujenzi, maendeleo, uimarishaji wa taasisi za kitaifa na jukumu la vijana kupambana na Ufisadi, ndiye pia mmoja miongoni mwa Wachad Watano tu waliochaguliwa na chuo cha Umoja wa Mataifa kwa mafunzo na tafiti kupitia Ufadhili wa serikali ya Japan ili kufanya mafunzo katika sekta ya kukabiliana na Ufisadi.

Na kwa upande wake, kupitia maneno yake, Larry alionesha furaha na Shukrani yake kwa tuzo hiyo, akishukuru waliompa, akionesha kwamba anaitoa kwa wanaharakati wote wa vyama vya kiraia(wasio wanasiasa) kama alivyosema, na hatimaye aliwashukuru wote kwa uaminifu huo akiahidi Hadhira kuwa atafanya juhudi zaidi, akiwaomba kushirikiana kwa ajili ya Maendeleo na Ustawi wa Nchi .