Kumbukumbu ya Kifo cha Shahidi mtoto mpalestina Muhammad Al- Durrah

Septemba 30, 2000 mtaa wa Salah Elden katika ukanda wa Gaza, Palestina
Muhammed aliambatana na babake kutoka katika mahali pa kazi yake kwa maandamano yaliyoanzwa na wapalestina dhidi ya Vikosi vya uvamizi, katika siku ya pili ya Mapinduzi ya msikiti wa Al-Aqsa yaliyoanzwa na raia wa Palestina, mnamo Septemba 28, mwaka wa 2000 .
Ili kupinga kuvamiwa na Arael Sharon Waziri mkuu huyo wa zamani wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, pia kukataa Mashambulizi endelevu dhidi ya Maeneo matakatifu ya Yerusalemu, na katika maeneo ya Palestina, ambapo mtoto huyo Muhammad Al-Durrah na babake Walijikuta walizingiriwa na Vikosi vya uvamizi vya Israel waliofyatua risasi nyingi Kwa mtoto na babake , hadi mtoto akianguka shahidi.
Na leo ni maadhimisho ya 22 ya Shahidi Muhammad Al-Durrah, aliyeaga Dunia wakati wa umri wa kumi na mbili.
Ulimwenguni unazingatia Muhammad Al- Durrah kama alama ijulikanayo katika harakati za Mapambano ya raia wa Palestina dhidi ya Uvamizi wa Israel, ambapo picha ya baba na Shahidi iliwekwa Stempu za posta na zatolewa kwa ulimwengu wa Kiarabu , na Mitaa mahsusi ilipewa jina lake
Mtoto huyo bado ni ishara haikusahaliwi kwa uhalifu wa vikosi vya uvamizi vya Israel, ambavyo bado vinafyatua risasi kwa watoto wapalestina hadi leo.