Muungano wa Waandishi wa Misri wapokea Viongozi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana 

Muungano wa Waandishi wa Misri wapokea Viongozi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana 

Juzi, Jumatano, Septemba 14, 2022, Dkt Alaa Abd El hadi,Mwenyekiti wa  Chama kikuu cha Ushirika  cha Muungano wa Waandishi wa Misri, aliwapokea viongozi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana. wakiwakilishwa na Hassan Ghazaly, Mwanzilishi na Mratibu mkuu wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, na Mwandishi Ahmed Al-Juwaily, Mhariri mkuu wa tovuti ya Makala na Maoni, tovuti rasmi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana, na mwanachama wa Chama kikuu cha Ushirika cha Muungano wa Waandishi wa Misri.

Mkutano huo ulishughulikia mazungumzo yenye tija pamoja na Mwenyekiti huyo, Dkt. Alaa Abdel-Hadi, ambyo yalijumuisha kurudisha kwa kazi muhimu za viongozi wa kihistoria katika uwanja wa Kiafrika na mahusiano ya kihistoria ya kiafrika,kama  Waziri Mohamed Fayek, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Afrika wakati wa enzi za Marehemu kiongozi Gamal Abdel Nasser, na baadaye mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Haki za Kibinadamu,Pamoja na Mwanafikra na Mwanaanthropolojia, Bw. Helmy Shaarawy, mkurugenzi wa Kituo cha Tafiti za Kiarabu na Kiafrika,

 Mwanahistoria mkuu Profesa El-Sayed Fleifel, Mkuu wa zamani sana wa Kitivo cha Mafunzo ya juu ya Kiafrika. 

Katika mazungumzo hayo, kwa upande wake, Dkt Abdul-Hadi alisifu umuhimu wa jukumu la vijana la Harakati ya Nasser  kwa Vijana lenye ushawishi mkubwa katika miduru ya vijana kwenye kiwango cha   utamaduni na uwanja. akisisitiza  utayari wa Chama kikuu cha Ushirika kutoa njia zote zinazowezekana za msaada ili kuongeza  ushiriki wa vijana wa Misri, pamoja na vijana wa Kiarabu na Kiafrika katika shughuli ya kiutamaduni, na pia kutoa nafasi ya kujieleza,  na kuwasilisha miradi yao ya kiutamaduni na kujenga. uwezo wao. 

Katika muktadha unaohusika , Ghazaly, Mwanzilishi wa Harakati  ya Nasser kwa Vijana , alielezea furaha yake kukutana na Mwenyekiti  wa Chama kikuu cha Ushirika cha Muungano wa Waandishi wa Misri, akibainisha kuwa anatarajia ushirikiano wenye tija kati ya Harakati na Chama hicho ili kutoa fursa kwa michango zaidi na shughuli za kiutamaduni na kiakili zinazohudumia vijana wabunifu na wenye vipaji, katika nyanja za uandishi, hadithi, riwaya na fasihi. ili kupanua wigo wa kuenea na kuboresha ujuzi wa vijana zaidi wa fasihi na kiakili. 

Inafaa kutaja kwamba Chama kikuu cha Ushirika cha Muungano wa Waandishi wa Misri kilianzishwa na Mwandishi mkuu Youssef El-Sibai mnamo miaka ya sabini,na kilijumuisha kundi la watu wabunifu, wakiwemo;  Naguib Mahfouz, mwandishi Muhammad Abdel Halim Abdullah, mwandishi Ihsan Abdel Quddous, mshairi Ahmed Ramy, mkosoaji Raja al-Naqash, mwandishi Tharwat Abaza, mwandishi Fikri Abaza, mwandishi Ahmed Ali Bakathir, mwandishi Abdel Hamid Joudeh al-Sahar, mwandishi Amin Youssef Ghorab, na waandishi wengine wakuu mashuhuri katika historia ya kiutamaduni na  fasihi ya Misri na Kiarabu.