Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 

Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 
Mji wa Nasr.. Mahali pa Ndoto 

Fikra ya kuanzisha mji wa Nasr ilianza baada ya mapinduzi ya Julai 23, mwaka1952, kiasi kwamba Rais Gamal Abd El Nasser alitoa uamuzi mnamo 1958 AD kupanua na kujenga miji katika eneo la Jangwa kaskazini mashariki mwa Kairo, haswa mashariki mwa mtaa wa Abbasia  mbali na nafasi za kilimo, akatoa ishara ya kuanza kwa kujenga mji kamili kwa njia ya kiustaarabu, kisasa na yenye mvuto na ameuita "Nasr City", ambao wahandisi waliuzingatia kama ardhi ya ndoto, kiasi kwamba eneo lake ni  zaidi ya kilomita mraba 250 katika  mashariki ya  barabara ya Kairo-Suez hadi kilo 51 na Barabara ya Kattameya, magharibi mwa nje Salah Salem na katika mtaa wa kaskazini ya Heliopolis na kusini, mtaa wa Mokattam.

Fikra hiyo ni ya mhandisi mmisri Sayed Karim tangu 1953, wakati alikuwa na ndoto ya kuacha "msongamano wa Kairo" na kuenda "upana wa Jangwa."mnamo mwaka huo huo akatoa pendekezo kwa serikali ili kuanzisha mji mpya, ila ilikataa , kwa sababu ikiona kuwa pendekezo hilo limepambana na maadili za Ujamaa.

Baadaye, Karim aliweza kuwasilisha wazo hilo kwa Afisa Anwar al-Sadat, aliyevutiwa nalo na muundo wake wa usanifu.Mhandisi huyo aliendelea na juhudi zake za kuwasilisha wazo lake kwa kila mtu, hadi alipoliwasilisha kwa Abd El Nasser, ambaye alipendekeza awasilishe mradi huo kama mji mkuu mpya wenye makao makuu ya serikali, uwanja wa michezo, na ukumbi wa mikutano.

Mhandisi Sayed Karim alichukua majukumu ya upangaji wa jiji kwenye eneo la ekari 6000. Mahali pake pana sifa ya kuunganishwa moja kwa moja kwa viingilio vyote vya jiji la Kairo.. Mipango yake inachanganya uwekaji serikali kuu na ugatuaji. Linachukuliwa kuwa jiji linalojitegemea kulingana na eneo lake la hali ya hewa, eneo na idadi ya watu, na inahusiana katika uhusiano wake na jiji la Kairo. Mpango wa jumla wa jiji una maeneo makuu kadhaa , idadi ya hoteli, klabu za michezo, maktaba, mbuga, masoko makubwa ya kibiashara, maeneo ya uwekezaji na burudani, na vitongoji vingine vingi vya Makazi, hospitali za umma na za kibinafsi.

Eneo la Michezo 

Liko katikati ya jiji na lilipangwa kwa njia ya mzunguko uliofungwa, na katikati yake ni Uwanja wa Kimataifa wa Kairo, uwanja mkubwa wa michezo na wa kisasa zaidi katika Mashariki ya Kati mnamo miaka ya hamsini,  uliofunguliwa mwaka wa 1960. . Unaweza kuchukua watazamaji takriban  85,000 - kwa wakati huu - na eneo hilo pia linajumuisha viwanja vingi, kumbi wazi na zilizofunikwa, bwawa la kuogelea, uwanja wa mbio, majengo ya usimamizi, na malazi ya wanariadha. Na makao makuu mengi ya mashirikisho ya michezo, kama vile: makao makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Nguvu, Shirikisho la Mashirikisho ya Michezo ya Afrika "OXA", Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri, Shirikisho la Misri la Michezo ya Nguvu, Shirikisho la Mpira wa Mikono la Misri, Shirikisho la Misri kwa Kujenga mwili, Shirikisho la Boga la Misri, Shirikisho la Bowling la Misri.

Eneo la Maonesho ya kimataifa 

Eneo hili linajumuisha soko la kimataifa na Ardhi ya Maonesho, na iliyokuwa moja ya misingi mikuu ya kuchagua eneo la soko la kimataifa la Kairo ilikuwa kuwasiliana moja kwa moja na jiji la Olimpiki ili wazo la uhusiano wa moja kwa moja na njia mbalimbali za usafiri wa jiji na vitongoji vyake mbalimbali vitapatikana.

Eneo la Vyuo Vikuu na Elimu

Kwa sababu ya umuhimu wa eneo la Mji wa Nasr, lilichaguliwa kuwa upanuzi wa Chuo kikuu kikubwa zaidi katika historia.Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilipanuka katika kujenga vitivo vya Sayansi, vitendo na sheria, na kuanzisha tawi la Chuo Kikuu cha Wanawake, makazi ya wanafunzi, na idara za taasisi za Al-Azhar. Taasisi ya Kitaifa ya Utawala na Maendeleo Endelevu, Chuo Kikuu cha Wafanyakazi, na Chuo Kikuu Huria cha Kiarabu.

Eneo la idara na majengo ya serikali 

  Iko kwenye mlango wa mji, ambako inaunganishwa moja kwa moja na jiji la Kairo na usafiri wake wa sasa, wakati huo huo haupingani na harakati za ndani za jiji. Hapo awali, sio wizara zote zilizopangwa zilihamia eneo la serikali, badala yake, suala lilianza kwa wizara mpya ambazo hazikuwa na makao  makuu huko Kairo, na kufuatiwa na baadhi ya wizara kama makao makuu ya Wizara ya Ulinzi, Fedha, Upangaji na Maendeleo ya Kiuchumi, Wizara ya Nguvu Kazi, Taasisi kuu ya Habari ya Serikali, Shirika Kuu la Ukaguzi na Wakala Kuu ya shirika na utawala, Wakala Kuu ya Uhamasishaji wa Umma na Takwimu, Mamlaka ya Mitambo ya Nyuklia ya Uzalishaji wa Umeme na mashirika mengine ya serikali na masilahi, na vifaa vya kitaifa.

Eneo la kijeshi 

Eneo hili liko karibu na Mji wa Michezo na kwenye mhimili mkuu wa mlango wa uwanja, ambapo uwanja wa gwaride la kijeshi na eneo lake ziko, na baadhi ya vifaa vya kijeshi.baada ya Ushindi wa Oktoba 6, 1973, Vikosi vya Kijeshi vilianzisha kumbukumbu ya Askari asiyejulikana kwenye barabara ya Al Nasr, inayozingatiwa ya muhimu zaidi jijini, na hivyo kama kumbukumbu kuu ya Mashahidi wa Vita vya Oktoba 6,1973, jukwaa na Panorama ya  Oktoba.

Eneo la viwanda 

Iko kusini mwa jiji kwenye barabara ya Autostrad inayohusiana na jiji la Helwan, ili eneo lake la utawala na biashara liko moja kwa moja kwenye barabara, na viwanda vya mwanga vimejilimbikizia ndani yake. Ilifunguliwa mwaka wa 1961 AD.