New Valley ni mkoa wa ustawi daima

New Valley ni mkoa wa ustawi daima

Imefasiriwa na / Nourhan Khaled Eid

Kwa eneo la 440098 km2 kusini-magharibi mwa nchini Misri katika Jangwa la Magharibi, na ni mkoa mkubwa zaidi nchini Misri kwa ukubwa, ambapo unawakilisha 44% ya eneo lote la Jamhuri ya kiarabu ya Misri,  katika upande wa mashariki kuna mikoa mitano ya Misri ya Juu: Minya, Assiut, Sohag, na Aswan, na katika upande ea kaskazini kuna mkoa wa Matrouh. AL-Wahat albahria  upande wa magharibi Libya ,
na Sudan upande wa kusini.

Binadamu alikuwepo ndani yake kabla ya kuandika historia, kwa hivyo unawakilisha logi na kumbukumbu ambayo ina hadithi ya ustaarabu kwenye ardhi ya Misri , ni mpito kwa kabila lolote la kiarabu lililokuja kutika jangwa kubwa katika mipango ya uhamiaji jumuishi, ya mwisho ambayo ilikuwa katika karne ya kumi na nane na mapema karne ya kumi na tisa.

 
Jina lake linatokana na tangazo la marehemu Rais Gamal Abdel Nasser mnamo 1958 ,alipoanza kuanzisha bonde sanjari na Bonde la Nile lilikatika jangwa la Magharibi ili Kuijenga upya na kuikuza kwenye maji ya chemchemi na visima, kwa lengo la kupunguza msongamano wa binadamu katika bonde la Nile, ambalo hapo awali liliitwa Jimbo la Kusini .
vifaa na huduma zilizokuwa zikifanya kazi mnamo kipindi hiki .

Idara ya ndani haingii Oases tangu 1961, Gavana wa kwanza, Jenerali Anwer Abdelhaleem , alipofikisha ili kutekeleza majukumu yake kama Gavana wa Al-wadi Algdeed, baada ya mkoa huu ulikuwa mkoa wa mipaka unafuatilia na Wizara ya Vita na Navy, unasimamiwa na Jeshi la Mipaka la Misri, linaloongozwa na gavana mwenye cheo cha wakili wa wilaya, unajumuisha vituo viwili vya usimamizi, vituo vya Kharga na Dakhla , na kila kituo kiliongozwa na Afisa wa jeshi mwenye cheo cha yuzbashi na pamoja naye kundi la askari ambao idadi yao katika kila kituo haizidi ishirini.Kundi la askari linahusishwa na makao makuu ya gavana, likiongozwa na mtu binafsi mwenye cheo cha (sol), pamoja na kampeni ya magari ya Ford saluni kwa gavana na gari la jeshi kwa mkoa .

Shule iliyopo katika kipindi hicho ilikuwa shule ya bure, inayoitwa leo, shule ya kibinafsi,  ni shule ya sheikh Bahr, elimu inayofupishwa katika shule hii juu ya alfabeti , na hisabati inafungwa baada ya 1959, shule ya msingi ambao jina lake lilikuwa shule ya serikali iliyopatikana katika uwanja unaoitwa Al-Sholaa leo, iliyogawanyika shule mbili:  shule kwa wavulana,  na shule kwa wasichana katka Al-Kharga iliyotoa huduma kwa kila mtu katika Algharga, na shule ya msingi katika Mot katika Aldakhla ilitoa huduma katika vijiji vyote katikati kituo cha Aldakhla ,na shule ya upili (Shule ya upili  ya Al-Kharga ) mwishoni mwake awamu ya upili , ilitoa huduma kwa Kharga na Dakhla na walikuwa na uhusiano na Eneo la Elimu la Qena .

Shule hizo zote zilianzishwa na Kikosi cha Mipaka (shughuli za Kijeshi), na baada ya hapo, mtu yeyote aliyetaka kuendelea masomo yake alikwenda Assiut, na shule ya sekondari iliyojitolea kusomesha wana wa Oasis ilikuwa Shule ya Sekondari ya Sahel Selim, na ilikuwa na sehemu ya ndani kwa ajili ya wana wa oasisi na pia hawa wale wanaotoka Sudan na Somalia. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kuhusu elimu hadi mwanzoni mwa miaka ya sitini na kuingia kwa usimamizi wa kitaifa na kuanzishwa kwa kurugenzi ya elimu huko New Valley.


Tangu mwaka 1924 , Jeshi la Mipakani la Misri lilichukua usimamizi wa mkoa na kuanza kuanzisha hospitali, moja Kharga na ya pili Dakhla, na zinashirikiana na Idara ya Madawa ya Mipaka.Katika kila hospitali kuna daktari mmoja anayetibu wagonjwa. katika taaluma zote, na katika kila hospitali kuna duka la dawa.Kuanzia daktari hadi kurudi kwake, na katika kila hospitali nje na ndani, gari hufanya kazi na daktari katika trafiki ya mara kwa mara hadi vijiji vya kila kituo. 
 
Na hali ya mkoa huu ulikuwa kama ilivyo hadi mwanzo wa kazi katika usimamizi wa kitaifa na kuanza kuanzisha hospitali ya serikali na kuu na pia vituo vya kiafya , na vituo hivyo vilikuwa Ofisi ya Usalama wa Jamii tu, katika oasisi, kulikuwa na ofisi ya hifadhi ya jamii tu yenye uhusiano na mkoa wa Qena, na kulikuwa na mfanyakazi mmoja akifanya kazi ya kutoa hifadhi ya jamii kwa wale ambao walikuwa na sifa hadi kuanzishwa kwa Kurugenzi ya mambo ya kijamii huko Alwadi Algadeed, na pamoja na kupokea uongozi wa mkoa kwa usimamizi. 


Usalama katika oasisi uliongozwa na Mameya  katika miji na vijiji vikubwa, na Masheikh katika nyumba za vijiji.Kila meya anafuatwa na ghufra kadhaa, ambao wanawajibika kwa kudhibiti kwa usalama ndani ya mikusanyiko hiyo.
 Umeme haukuingia kwenye nyumba za raia hadi baada ya kuanzishwa kwa kituo cha kwanza cha umeme katikati ya miaka ya sitini katika jiji la Kharga na Dakhla miaka mitano baadaye. na umeme katika mkoa wa alkharga ulikuwa katika barabara tu kwa njia Nguzo zake zimetundikwa na globu ambayo huwashwa usiku kwa kupita juu ya nguzo kwa chombo  katika kuipatia mafuta ya Keroxine na kuwasha.

Barabara na njia ni miongoni mwa changamoto kubwa zilizokumba maeneo hayo wakati wa nyuma .hadi mwaka 1961 mkoa huu  ulikuwa umetengwa kabisa na Misri na hapakuwa na barabara za lami  zilizokuwa zikiunganisha na magavana wa Misri na nyinginezo na zilizo karibu zaidi. Assiut, ambayo ilifanywa na kampuni ya Kiingereza ili kutafuta madini katika oases, na hiyo ilikuwa mwaka wa 1910  na ilifikia mstari huu wa chuma hadi kijiji cha kampuni (55), na jina hili ni Pamoja naye katika kupanua njia ya reli kutoka wilaya ya Qena, kuanzia kaskazini mwa Farshout, mali ya Nagaa Hammadi, hadi Al-Kharga, kisha kuipanua hadi kilo 30 kwenye Barabara ya Dakhla.

Kampuni ikiisha kufilisika na kuuza laini hii na treni kwa serikali ya Misri, ambayo iliiendesha kuwatoa huduma kwa watu wa oas. Njia yake ilikuwa kutoka kwenye jukwaa kwenye reli, barabara ya Cairo-Aswan, kwenye kituo kiitwacho (Mwasala Wahat  ), na inaishia kaskazini mwa mji wa Kharga, kilo moja na nusu kutoka mji wa zamani wa Kharga, na makao makuu ya kituo hicho yalikuwa (klabu ya mkoa wa kijamii sasa)

Majengo ya reli na gari la kubebea mizigo bado vipo ndani ya klabu hadi sasa, na muda wa kusafiri kutoka nje hadi kuendelea kwa mawasiliano ya alwahat ni takribani saa 10 hadi 12, iwe ni kwenda au kurudi, na treni hufanya safari moja kwa wiki. kila wiki na hakuna mawasiliano mengine zaidi ya hayo.

raia wa Dakhla, walikuwa walikwenda kwa Kharga kwa treni hii au kwa magari ya lori kutoka kwa mabaki ya jeshi la Kiingereza, ambayo yalinunuliwa na Mameya wa Dakhla kutoka warsha za Alsabtia huko Kairo na kuendeshwa ili kusafiri  wananchi kutoka Dakhla hadi Kharga safari hilo ilichukua zaidi ya saa 24 kwenye barabara iliyopangwa na lami , hukuwa mateso makali ya Magari yanakwama kwenye mchanga mara nyingi, abiria walitua na shuka linawekwa chini ya magurudumu, gari linasogezwa, basi kupanda gari  tena, na hii inarudiwa zaidi ya mara 10 wakati wa safari hii ni pamoja na kuwa abiria hao wawe wanaume, wanawake na watoto, kwenye boksi la lori pamoja na  pipa lililojaa maji na pipa jingine la petroli, ndama na ng'ombe kuwasafirisha hadi Kharga, na tegemeo lilikuwa juu ya shughuli za mifugo ili kutoa nyama kwa ajili ya Kharga kutoka Dakhla .

Na hali hii iliendelea hadi barabara ya Assiut Alwadi Algadeed iliyotengenezwa lami ambayo ilifunguliwa katikati ya Januari 1961 , na njia/ laini ya mabasi iliendeshwa kwenye barabara hii Januari 25, 1961 , na siku hiyo hiyo treni ya mwisho ya reli ilisafiri na kutangaza. kusitishwa kwa uendeshaji wake, na mabasi haya yalikuwa ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu. Hii ilifuatiwa na ufunguzi wa barabara ya Kharga/Dakhla baada ya kujengwa kwa lami mnamo Novemba 16, 1962,  na basi la kwanza kwenda Dakhla liliendeshwa, na mnamo Machi 25, 1963, barabara ya Kharga-Paris ilifunguliwa baada ya kuanzishwa lami.

Na kwa Mamlaka ya Mipaka kupokea shughuli za usimamizi wa mkoa huu, ilifanya kazi ya kutumia simu isiyo na waya iliyopanuliwa na mpango wa reli na imeunganishwa na  Kituo cha simu cha Nagaa Hammadi na njia nyingine ya reli kwa usalama wa uendeshaji wa treni.

 Ambapo kuna kamanda wa kijeshi (kutoka Kikosi cha Mpakani), basi mstari wa ndani unapanuliwa kuunganisha vijiji vyote vilivyounganishwa na kituo.Wakati wa kuzungumza, makao makuu yote ya mameya yanajibu, na msemaji/ Spika anauliza yeyote anayetaka, kila mtu anasikia mazungumzo yakifanyika kati ya mzungumzaji mkuu na yule anayetakiwa kuzungumza naye, kuwa mstari mwingine unapanuliwa kutoka viunga hadi Paris na unajumuisha Mameya wa wadi ya Bulaq, Paris, Al-Kharga, na makao makuu. ya laini (Kituo cha Al-Kharga), na kituo hicho kinawasiliana na laini iliyo na swichi ya mkoa ambamo makamo makuu ya  gavana yuko. Kuhusu kuwasiliana na Mamlaka ya Mipaka, ilifanywa kupitia vifaa ambavyo  visivyo na waya huko Kharga na Dakhla, kutoa kamili kila baada ya saa mbili, au kufungua na mamlaka wakati wa dharura, kulingana na maagizo ya Gavana.

Simu za kiraia kwa raia, ambao unafanywa kupitia kituo cha simu cha  Nagaa Hammadi sawa ya kutoka Dakhla au Kharga, kwa hivyo ilifanyika na hakuna kitu kibaya nayo, na walikuwa wakingojea kwa zaidi ya saa 3 au 4, na ndivyo ilivyokuwa hadi mkoa uliingia katika utawala wa eneo hilo na kufungua ubadilishanaji wa mwongozo nje ya Kharga iliyounganishwa na Assiut baada ya kuwekewa waya kupitia Ubadilishanaji huu unatoka Kharga, na saa maalum zimewekwa kufanya kazi kwenye mstari huu kutoka Dakhla, na hali iliendelea hadi ikabadilishwa kuwa moja kwa moja kiotomatiki kibao mnamo Mei 26, 1980, ubadilishanaji wa kiotomatiki uliendeshwa na uwezo wa 800 katika jiji la Kharga.

Wizara ya Utamaduni haikuingia katika Alwadi Algadeed hadi mwisho wa 1969, wakati wajumbe wawili kutoka kwa utamaduni wa watu wengi (Saad Kamel - Saeed Ezzat) Kusoma kushughulika  jumba la kiutamaduni linalohudumia mkoa wa New Valley, na kwa ushirikiano na mkoa, Jumba la Utamaduni la New Valley lililoanzishwa kwa sasa limeendeshwa. 
Ambayo palikuwa na ukumbi wa michezo (Hanger Sag), ambayo ndani yake kulikuwa na viti vilivyotengenezwa na karakana za Mamlaka ya Ujenzi wa Jangwani, na jukwaa lililojumuisha sakafu ya mbao za hema na (2) vibanda vya mbao katika vibanda vya kubomoa. 

na baada ya vita vya Oktoba 1973, utamaduni wa watu wengi ulianza kubomoa vibanda vya mbao na Hangar Sag na kujenga majengo ya jumba ambayo bado yamesimama juu yake.

Mkoa huu una sifa ya uchoraji mchanga, bidhaa za viwanda vya Mitende  sanaa ya plastiki, arabesque,wicker, keramik, ufinyanzi, bidhaa za kilim na mazulia .
.pia hufurahia hali ya hewa kavu wakati wa kiangazi na joto wakati wa baridi, na asilimia kubwa zaidi ya jua Duniani kote mwaka mzima. 

New Valley linagawanywa kiutawala katika: 

Kituo cha Al-Kharga

 kinajumuisha mabaraza 8 ya vijiji: Al-Munira, Nasir Al-Thawra, Bulaq, Paris, Bulaq Mashariki, Sana'a, Baghdad, na Al-Max. 

Kituo cha Dakhla
 kinajumuisha mabaraza 8 ya vijiji: Tanida Balat, Al Maasara, Al Rashida, Al Jadida, Al Qasr, Al Farafra, na Gharb Al Mahoub. Mkoa wa AlwadiAlgadeed linajumuisha kundi la alama muhimu.

ambazo ni muhimu zaidi ni: 
Hifadhi ya Jangwa Nyeupe 
Bustani ya kwanza ya kijiolojia ya Misri, moja ya hifadhi nzuri zaidi na muhimu ya asili katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kilomita 38 kutoka mji wa Farafra kuelekea Oasis Bahariya  na karibu na barabara ya lami kwa kina cha kilomita 25. 
Ni muundo wa sedimentary wa chokaa, sababu za mmomonyoko ziliunda sehemu nyingi katika  mabaki ya aina tofauti za wanyama au mimea, na zinaonyeshwa na uzuri wa asili ya kupendeza, mazingira safi na hewa safi na baadhi ya miti kama vile miti ya acacia na mitende. ambayo hukua kati ya miamba hii.

Aljolf Al-kabeer 

Hifadhi ya Al-Jolf Al-Kabeer iko kusini mwa mlima wa Al-Awainat, na inachukuliwa kuwa uwanja mkubwa zaidi wa meteorites kuanguka ulimwenguni.
Uwanda wa Al-Jilf Al-Kabir una mawe ya mchanga wa Nubiani, takriban 1,000. mita juu ya usawa wa bahari, na kuna maeneo ya milimani, mabonde nyembamba yenye kina kirefu, na minyororo ya Bahari ya Mchanga Kubwa Zaidi inayoenea kutoka kaskazini hadi kusini. 

Pia ina sifa ya kipekee ya glasi, ambayo inaweza kutumika kiuchumi. Kuna aina mbalimbali za wanyama ambao wako hatarini kutoweka, kama vile kondoo dume aina ya Arwa, kulungu wa Misri, na kulungu weupe.Kwa ujumla, ina aina mbalimbali za kibayolojia kwa kuwa na aina (11) za mamalia, (10) aina ya ndege, na aina (75) za mimea ya porini. 

Pango Gara

liko umbali wa kilomita 120 kutoka Alfrafra, na linarudi kwenye enzi ya kijiolojia kwa namna ya pengo kubwa chini ya uso wa dunia, na inaonyesha kwamba mtu wa kwanza aliishi katika eneo hili na mgeni anaweza. Kutembea kwa urahisi ndani ya pango anapoingia ndani ya pango, kwani kuna michoro ya asili ya wanyama ambayo iliundwa na wanadamu kabla ya historia na inachukuliwa kuwa moja ya mapango makuukuu zaidi ulimwenguni, ambayo imepangwa kuwa hifadhi ya asili ya kuilinda. kutoka kwa uharibifu.

Wadi Hans 
Maeneo haya ni kilomita 55 kutoka mji wa Farafra kuelekea kaskazini na hupokea idadi kubwa za watalii kutumia usiku mmoja au zaidi, haswa katika usiku wa mwezi, kufurahia uzuri wa asili ya kupendeza na safi. mazingira kavu ya uchafuzi wa mazingira. mitende na "mishita" , na kuna wanyama pori adimu na ndege katika maeneo haya, na maeneo haya yamekusudiwa kuwa hifadhi za asili.

Mlima wa Waingereza 
Ilipa jina hili kwa sababu vikosi vya Kiingereza viliwekwa huko wakati wa uvamizi wa Waingereza wa oasis, na inaweza kutambuliwa kupitia magofu yaliyo juu yake.Vikosi vya Senussii vilivyokuwa vinashambulia oasis wakati huo. Mlima wa Waingereza unatofautishwa na kilele chake cheusi kwa sababu una mawe ya dolite na basalt, ambayo ni miamba ya volkeno  ambayo inaonyesha kuwepo kwa shughuli za kale za volkano katika eneo hilo. umuhimu wa eneo la mlima wa Waingereza unatokana na eneo lake katikati ya eneo la mijini, pamoja na uwepo wa kisima cha maji cha Kirumi kwenye kilele cha mlima.

Hifadhi ya Jabal Kamel

Hiyo iko katika mkoa wa Toshka katika eneo kati ya Jabal Kamel na Jabal Al-Awainat karibu na Hifadhi ya Golf Al-Kabeer katika Jangwa la Magharibi, karibu kilomita 2 kutoka mpaka wa Sudan na karibu kilomita 150 kutoka mpaka wa Libya. hufikia takriban tani 10 na urefu wa mdomo wake hufikia takriban mita 45. Ina kina cha meta 16 hivi, na kreta inakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 4,000 na 5,000 meteorite ya mlima wa Kamel uligunduliwa mnamo Februari 2010 wakati wa msafara wa kijiofizikia uliojumuisha timu ya watafiti wa Misri na Italia Tukio hili kubwa la kisayansi la kimataifa lilichapishwa katika majarida mengi ya kisayansi ya kimataifa wakati wa mwezi wa 7 mwaka wa 2010.

Athari za Al Kharga:

Hekalu la Hibis 

Hekalu la Hibis liko karibu kilomita 1 kaskazini mwa mji wa Kharga. Hekalu hili lina umuhimu wa pekee, kwani linawakilisha enzi tofauti za kihistoria, Faraonic, Kiajemi,Ptolemaic, na Kirumi. 
Historia yake inaanzia enzi ya Mafarao - nasaba ya 26 - na ilijengwa kuabudu Utatu Mtakatifu (Amun-Mutt-Khonsu) ilianzishwa  kujenga na binti zake Iris na kisha kukamilishwa na mrithi wake Ahmose II, lakini sehemu kubwa ya majengo yalikamilishwa wakati wa enzi ya Uajemi wakati wa utawala wa Mfalme Dara 1 mnamo 522 , na maandishi. Sehemu ya mbele ya hekalu la Mfalme Nekhtanebo mnamo 350 .
Hekalu linaanzia mashariki na ziwa takatifu, kisha marina, kisha lango la Kirumi, ambalo lina maandishi ya Kigiriki kutoka enzi ya Mfalme (Galba) katika mwaka wa 69, Lango linafuatwa na njia ya kondoo waume inayoelekea kwenye lango kubwa, kisha lango kuu.Mwisho wa hekalu ni Patakatifu pa Patakatifu pamoja na maandishi yake ya kipekee.

Jabana Al-Bujat 
iko kilomita 3 kaskazini mwa mji wa nje nyuma ya Hekalu la Hibis na jina lake linatokana na mtindo wake wa usanifu katika mfumo wa domes, na historia yake inaanzia karne ya pili hadi karne ya saba na inajumuisha 263 ndogo. makaburi yenye umbo la kanisa yaliyojengwa kwa mtindo wa majumba na katikati yake ni magofu ya kanisa linalofikiriwa kuwa mojawapo ya makanisa ya zamani zaidi ya Coptic nchini Misri.
Muhimu zaidi kati ya makaburi hayo ni makaburi ya (Alkhrog), ambayo michoro yake inaeleza kisa cha kutoka kwa wana wa Israel kutoka Misri, ikifuatiwa na Firauni pamoja na askari wake, na kufuatiwa na makaburi ya (Amani), ambayo ndani yake kuna picha za Yakobo, Bikira Maria, na watakatifu Paula na Takla, na kwenye makaburi mengine kuna maandishi ya rangi na maandishi ya Coptic ambayo yanasimulia hadithi za Ukristo huko Misri.

Allabkha
Ni takriban kilomita 13 kaskazini mwa mji wa Kharga, na inajumuisha mabaki ya ngome, hekalu, na makaburi ya matofali ya udongo yaliyotawanyika katika vilima vya eneo hilo. Pia kuna miti ya mshita na mitende katika eneo hilo, na huko. ni mfumo wa njia za kale za kukusanya maji na kumwagilia eneo hilo katika enzi ya Warumi. 


Majumba ya Al-Nadura
 yapo kilomita 1 kutoka mji wa Kharga kutoka upande wa mashariki wa Hekalu la Hibis. Iliitwa Nadura kwa sababu ilitumika kama kituo cha udhibiti wakati wa Waturuki na Wamamluki kugundua - Mtawala Antonius Pius mwanzoni mwa karne ya pili .Ina mabaki ya maandishi ya hieroglyphic na maandishi ya mungu wa kike Aphrodite.

Jumba la Mustafa Al-Kashif 
 Liko chini ya kilomita moja nyuma ya makaburi ya Al-Bajawat, ambayo ni mabaki ya ngome ya Warumi ambayo ilikuwa kama ngome kubwa.
 sehemu ya jengo, ambayo ni makazi ya kujitegemea na paa katika mfumo wa kuba ambamo matambiko ya kidini yalifanyika.Pia ilitumika kama makazi ya wafanyabiashara wanaopita.

Hekalu la Ghuwaita
 liko kilomita 21 kusini mwa mji wa Kharga.Lilianza tangu Enzi ya 27 (522) na lilijengwa kwa ajili ya ibada ya Utatu Mtakatifu (Amun-Mut-Khonsu).
Kuna maandishi kwenye hekalu la Ptolemy akiwa amevaa taji ya Misri ya Juu kutoka upande wa kusini na taji ya Misri ya Chini kutoka upande.Ile ya kaskazini, na hekalu inaishia na Patakatifu, na kando yake kuna vyumba vya namna ya kuba. 

Hekalu la Dosh huko kijijini Paris 
lililoko kilomita 23 kutoka kijiji cha Paris katika jangwa.Ilijengwa kwa ajili ya ibada ya mungu Saber Apis, mungu wa Warumi na mungu Isis. Ilianza enzi za wafalme wa Kirumi ( Trajan na Hadrian) na kuna picha kwenye kuta zake za Mtawala Tarhan akimtolea mungu sadaka. 
Hekalu la Qasr al-Zayan 
liko kusini mwa Qasr Ghuwaita, kilomita 25 kusini mwa mji wa Kharga. Ujenzi wake ulianza enzi ya Ptolemaic na ulijengwa kwa ajili ya ibada ya (Amun Hept).Katika maandishi yake, mfalme anaonekana. kutoa sanamu (Maat) ya mungu Amun juu ya kichwa cha kondoo . 

Makumbusho ya Mambo ya Kale "Alana za kale"
huko Kharga Jumba hili la makumbusho linajumuisha mabaki mengi ya kale ambayo yalipatikana katika maeneo mbalimbali ya kiakiolojia, ikiwa ni pamoja na picha za kuchora za Mafarao zinazopatikana katika eneo la kasri la Dabba huko Balat, na hiyo ni sanamu ya mungu Horus, na sanamu ya simba anayechutama akiwa na uso wa binadamu ambao ulipatikana katika hekalu la Deir Al-Hajar, pamoja na mkusanyiko vyombo vya ufinyanzi kutoka enzi ya Coptic na vipande vingine vilipatikana katika eneo la Mut huko Dakhla. 

Baadhi ya magofu ya Dakhla: 

Darb al-Ghubari 
ni njia ya lami inayounganisha oasisi ya Kharga na Dakhla.Ni moja ya njia za zamani za jangwa zilizokuwa zikiunganisha oasi pamoja hapo zamani.Karibu na mwisho wa barabara na Kabla ya kijiji cha Tenida, kuna baadhi ya mawe ya mchanga ambayo yana sura nyingi katika umbo la ngamia, ambayo yanahusishwa na michoro fulani ya picha ya baadhi ya wanyama. 

Kijiji cha Al-Bashandi 

Kijiji kidogo ambacho makao yake yalijengwa kwa  mtindo wa Mafarao kwa matofali ya kijani kibichi, na kina hekalu la zamani lililozikwa kwenye mchanga. 
Inawezekana kwamba ilitokana na familia ya 19 ya Mafarao, kisha ilirejeshwa wakati wa utawala wa Ramesses IX. Pia kuna makaburi ya Kirumi ya watawala wa eneo hili tangu karne ya kwanza AD, na imeandikwa kwa njia ya zamani. ambayo inasimulia mchakato wa kuangamizwa na kesi ya wafu katika mahakama ya Osiris.Katika kijiji hicho, kuna makaburi ya Kiislamu ya Sheikh Bashandi, ambaye aliitwa kwa jina lake na kutumika Kama kitabu cha kufundisha Qur'ani Tukufu. watoto wa kijiji hicho, na iko kusini mwa kijiji hicho ni hekalu huko Rabia, ambalo lilianzia enzi ya Warumi na lilijengwa kwa jiwe la mchanga. 

Makaburi ya mahakama ya Mafarao yana matuta matano ambayo yanainuka juu ya kila mmoja, kama vile vipande vya makaburi ya Farao karibu nao, makaburi mengine ya Warumi, na pia kuna lango la kaburi la mtawala wa eneo hilo lililotawazwa na taji mbili ndogo. obelisks na mlango uliowekwa na hieroglyphs kwamba yeye ndiye watawala hodari wa jangwa, na matuta yote ni ya watawala wa oases na kurudi kwenye enzi ya Ufalme wa Kale, Nasaba ya Sita 2430  . 

Ikulu ya Kijiji cha Kiislamu 

Kiko kilomita 22 kaskazini mwa mji wa Mut, na ni sehemu ya kwanza ambayo yalipokea makabila ya Kiislamu baada ya kuwasili katika oasisi katika mwaka wa 50 Hijiria, na ina mabaki ya msikiti kutoka karne ya kwanza Hijiria. ilisitawi katika enzi ya Ayyubid Misikiti kadhaa kutoka enzi ya Waturuki na Mamluk, na kuna lango katika umbo la hekalu la mungu Thoth lililotumiwa kama lango la nyumba. 

Makaburi ya Al-Mazouqa
 Yapo umbali wa kilomita 5 kutoka kwenye jimbo, na kilomita 37 kutoka mji wa (Mutt) Dakhla, nayo ina barabara ya lami, na mitende, ndege, mummification, hesabu, na adhabu. na ziligunduliwa mwaka 1973 AD na Dkt. Ahmed Fakhry, na ina makaburi mawili ya watu wawili, mmoja wao ni Bady Osiris na mwingine ni Bady Bastet.


Hekalu la Deir al-Hajar 


 liko umbali wa kilomita 15 kutoka ikulu na kilomita 47 kutoka mji wa Mutt. Lilianza zama za wafalme wa Kirumi (Mfalme Nero), na limejengwa kwa mawe ya mchanga na kuchorwa kwenye kuta zake. picha na maandishi yanayowakilisha imani ya Farauni.Ilijengwa ili kuabudu miungu Amun, Mut na Khonsu, na ni moja ya mahekalu muhimu huko Dakhla.

Vyanzo :
Lango la kielektroniki la Mkoa wa New Valley.
Tovuti za Chuo Kikuu cha New Valley.
Tovuti ya Taasisi kuu ya Taarifa.
Makala ya Kichwa cha " Oktoba 3,1959 .... Historia ya kufikia kwa msafara wa kwanza wa maendeleo huko New Valley", Al Masry Al Yom.