Mansoura mpya...Miji ya kizazi cha Nne

Mansoura mpya...Miji ya kizazi cha Nne

Imeandikwa na / Dkt. Khairat Dergham

Imefasiriwa na / Mervat Sakr

Mji mpya wa Mansoura ni mojawapo ya miji ya kizazi cha nne iliyozinduliwa kwa agizo la urais mnamo 2018 ya kuchukua takriban watu elfu 680 wa idadi ya watu kwenye eneo la ekari 720, Kazi ilianza awamu ya kwanza mnamo Januari 2017 kama hatua ndani ya hatua nne mfululizo, kwani mji uko kwenye barabara ya kimataifa ya pwani, ambayo iko ndani ya miji ya Mkoa wa Dakahlia na inashirikiana kiutawala na Mamlaka ya Jamii za Mijini, na awamu ya kwanza ya mji mpya wa Mansoura inajumuisha kuwa kwenye barabara ya pwani karibu na mji wa Gamasa na iko mbali Mji wa Mansoura kwa mji mkongwe ni kilomita 45 na mradi wa treni ya umeme kuunganisha mji wa zamani na mji mpya kuchukua muda wa dakika 15 na una makazi ya kijamii, nyumba za kati, nyumba za watalii na majumba ya kiutalii, Awamu ya kwanza ina eneo la ekari 2036 na imekamilika kwa 100% Ndani ya awamu ya kwanza, kuna Chuo Kikuu cha New Mansoura na jengo la udhibiti wa kizazi cha nne,  linalofika chumba kikuu cha kudhibiti.

 Mji mpya wa Mansoura unajumuisha chuo kikuu cha mkoa, eneo la vifaa na huduma, chuo kikuu cha kibinafsi kinachohusishwa na Chuo Kikuu cha Mansoura, jiji la matibabu, na maeneo ya viwanda vya teknolojia, na ina mtambo mkubwa zaidi wa kuondoa maji katika Delta yenye uwezo wa mita za ujazo elfu 160 kwa siku, pamoja na corniche tisa za urefu wa mita 4.2, kundi la shule, vituo vya matibabu, masoko, na pia kundi la fukwe za umma, na awamu ya kwanza ya jiji inawakilisha 40% ya eneo lote, kwani inajumuisha nyumba 25,000.

 Pia kinajumuisha Chuo Kikuu kipya cha Mansoura  kipo katika eneo la ekari 127 na kinachojumuisha vyuo 14, na wanafunzi wanapokelewa katika mwaka mpya katika vyuo 8, ikiwa ni pamoja na programu 23 za kisayansi katika vitivo vya sayansi ya uhandisi, sayansi ya kompyuta, dawa, meno, maduka ya dawa, sayansi ya msingi, sayansi ya kimataifa na shughuli za kisheria, mradi utafiti huo uko kwenye mifumo ya kisasa ya masomo inayoendana na kasi ya vyuo vikuu vya kimataifa na Duniani.

Alfajiri ya siku mpya, ulimwengu ushuhudie ufunguzi wa mji mpya wa Al-Masoura, moja ya miji mipya, iliyoanzishwa ili kuendana na makundi yote ya jamii, riziki na maisha mazuri kwa raia wa Misri, ili mafanikio hayo yote yawe katika zama za kiongozi mkubwa wa Misri anayetaka kutoa njia zote za maisha kwa maisha mazuri yanayolingana na mwananchi wa Misri.

Wakati wa ufunguzi wa mji mpya wa Mansoura, Rais pia alishuhudia ziara ya Rais katika Shule ya Msingi katika Mkoa wa Dakahlia, moja ya vijiji vya Mpango wa Rais wa Maisha Bora, ambao uliwafurahisha wale wote waliokuwepo na maelezo jumuishi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Maisha Bora, Bi. Aya Omar Al-Qamari, mfano wa heshima kwa vijana wenye tamaa na bidii wa Misri wenye kiwango cha juu cha mawazo, sayansi na shughuli ambazo tunajivunia, na ambazo natumai kutoka kwa vijana wa Misri kwamba mifano hiyo ya heshima itakuwa mfano kwao.