Mapinduzi ya Julai 23 Yaliyobadilisha Matukio ya Historia
Imeandikwa na: Esraa Abdelazeem Ahmed
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili/ Mervat Sakr
Mapinduzi ya Julai 23, 1952 yanazingatiwa kama tukio ambalo limebadilisha historia ya Misri, na pia yalikuwa mwanzo wa mapinduzi yote na harakati za ukombozi wa kikanda na kimataifa. Yalifanya mafanikio makubwa, na leo ni kumbukumbu sabini na mbili ya mapinduzi ya Julai 23 yaliyoanzishwa na baadhi ya maafisa wa kijeshi waliotajwa "maafisa huru" chini ya uongozi wa Gamal Abdel Nasser.
Baada ya hali ya mapinduzi kutulia, kamati kuu ya maafisa huru iliundwa upya na kujulikana kama "Baraza la Uongozi wa Mapinduzi." Baraza hili lilikuwa na wanachama kumi na tatu wakiongozwa na Mohamed Nagib. Wanachama wa baraza hili walikuwa:
• Gamal Abdel Nasser
• Anwar El Sadat
• Abdel Hakim Amer
• Youssef Seddik
• Hussein El Shafei
• Salah Salem
• Gamal Salem
• Khaled Mohieddin
• Zakaria Mohieddin
• Kamal Eldin Hassan
• Abdellatif El Baghdadi
• Abdel Menem Amin
• Hassan Ibrahim
Mohamed Nagib:
Alichaguliwa kuwa rais wa kundi la maafisa huru mnamo Julai 1952. Maafisa huru walimchagua Jenerali Mohamed Nagib kuwa kiongozi wa mapinduzi kwa sababu alikuwa na ujuzi wa hali ya juu katika kushughulikia masuala ya kijeshi na umeme, na alikuwa mvumilivu katika kushughulikia masuala ya kiraia. Alikuwa rais wa kwanza wa Jamhuri baada ya mapinduzi ya Julai 23.
Gamal Abdel Nasser:
Alikuwa kiongozi wa kweli wa Mapinduzi ya Julai 23, 1952, na kiongozi wa harakati za ukombozi katika Mashariki ya Kati na Afrika. Alikuwa rais wa pili wa Jamhuri baada ya kuondolewa kwa utawala wa Mfalme Farouk. Alikuwa na jukumu muhimu katika kuunda na kuongoza kundi la siri la kijeshi linaloitwa "Kundi la Maafisa Huru".
Mohamed Anwar El-Sadat:
Aliweza kutangaza taarifa ya kwanza ya mapinduzi na alifaulu kumshawishi "Ali Maher Basha" kuunda wizara baada ya mapinduzi, na pia kumshawishi Mfalme Farouk kukubali mahitaji ya jeshi.
Salah Salem:
Alijiunga na kundi la maafisa huru na alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya kundi hilo.
Gamal Salem:
Alijiunga na kundi la maafisa huru na alishiriki katika vita vya Gaza. Baada ya mafanikio ya mapinduzi, Gamal Salem alikuwa rais wa kamati kuu ya mageuzi ya kilimo.
Abdellatif El-Baghdadi:
Alikuwa afisa wa kwanza aliyeweza kurusha mabomu huko Tel Aviv. Alijiunga na kundi la maafisa huru na alisisitiza kwa maoni yake kuanzisha mapinduzi ya Januari 25, 1952 kufuatia moto wa Kairo.
Sababu za kuanzisha mapinduzi:
• Mfalme Farouk aliendelea kupuuza wengi na kutegemea vyama vya wachache.
• Kulikuwa na mgogoro wa ndani na mapigano makali kati ya serikali za Nakrashi na Abdel Hady.
• Vita vya Gaza vilianzishwa na mfalme, alilazimisha nchi kuingia vita hivyo bila kujiandaa kikamilifu na hatimaye kushindwa.
• Makubaliano ya uondoaji wa vikosi vya Uingereza yalionyeshwa kwa Umoja wa Mataifa, lakini Baraza la Usalama halikutoa azimio lolote kwa maslahi ya Misri.
• Upungufu wa ukubwa wa vikosi vya kijeshi baada ya Uingereza kuweka ulinzi wake juu ya Misri na kupeleka vikosi hadi Sudan ili kusaidia kuzima uasi wa Mahdi.
• Hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana katika Misri.
• Ukandamizaji na ukosefu wa haki ya kijamii kati ya madaraja ya raia na usambazaji mbaya wa mali na utajiri wa taifa.
• Utawala wa Mfalme Farouk ulikuwa wa kifahari katika ikulu, huku watu wakiteseka.
Mafanikio ya Mapinduzi ya Julai 23:
1. Yalikuwa mapinduzi ya amani, yaani hakukuwa na umwagaji wa damu.
2. Mapinduzi yalianzishwa na baadhi ya maafisa vijana chini ya uongozi wa Gamal Abdel Nasser, na jambo hilo lilikuwa jipya katika mapinduzi mengi ya kijeshi ambayo mara nyingi yanaanzishwa na maafisa wa cheo cha juu.
3. Kundi la Maafisa Huru lilikuwa na wanachama kutoka vyama na itikadi mbalimbali za kisiasa.
4. Mapinduzi yalipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wakulima na wafanyakazi waliokuwa wanateseka kutokana na hali mbaya nchini Misri.
5. Kutekeleza mpango wa kutenga vyama, kusimamisha katiba ya 1923, na kuweka kipindi cha miaka mitatu kuelekea utawala mpya wa umma.
6. Mapinduzi yalikuwa na sera ya ndani ya kubadilika kulingana na maslahi ya nchi, ambapo hayakusimamisha sera ya nje. Katika kukabiliana na ukoloni baada ya Marekani kukataa kutoa misaada ya kijeshi na kutekeleza miradi, Misri ilielekea kwa nchi nyingine ili kutekeleza miradi yake ya kitaifa.
7. Mapinduzi yaliunga mkono umoja wa nchi za Kiarabu na kusaidia nchi hizo kupigana na ukoloni. Pia, Misri iliungana na Syria na Yemen na kupigana na ukoloni barani Afrika na Asia. Aidha, Misri ilikuwa na jukumu kubwa katika kuanzisha Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote.