Maonesho na Mkutano wa Matibabu wa Kiafrika na (ExCon)

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky
Mahusiano ya Misri- Afrika yanaunganishwa katika ngazi zote, na katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kiusalama, kiutamaduni, kisayansi na vilevile matibabu, inayoonesha ushirikiano wa unachama wa kimkakati kati ya Misri na nchi za bara, kwa namna inayochangia kuongeza mafanikio ya pamoja, na maslahi na kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Kufanyikwa kwa Mkutano na Maonesho ya Matibabu wa Afrika nchini Misri kunadhihirisha kipaumbele kikubwa ambacho Misri inayotoa kwa Bara la Afrika haswa katika nyanja za tibabu, afya na tiba ya magonjwa mbalimbali kwa kuongeza tafiti mbalimbali za kimatibabu ili kukabiliana na kila aina ya magonjwa na janga Barani Afrika na kuendeleza matibabu ya dawa kwa ajili yakr kwa namna ambayo inahifadhi afya ya mwafrika.
Kuanzisha teknolojia ya matibabu na kuweka viwanda vya dawa nchini Misri, pamoja na hatua madhubuti za kuzuia kuenea kwa magonjwa, ambayo ni kielelezo cha msukumo kwa nchi za Kiafrika, hakuna shaka kwamba kutoa maji safi, kutoa chakula bora, kueneza ufahamu juu ya lishe bora , kukuza utafiti wa kisayansi, kuunga mkono madaktari na kuendeleza hospitali inawakilisha ramani ya barabara ya Afrika muhimu kwa kuboresha sekta ya matibabu, kuondokana na magonjwa mbalimbali na kuunda vizazi vyenye afya vinavyoweza kutoa na kushiriki kikamilifu katika maendeleo na kufurahia maisha, ambayo inawakilisha lengo la kimkakati la Afrika.
Hakuna shaka kwamba Mkutano wa Kimatibabu wa Afrika linawakilisha hatua muhimu katika kusaidia kutafuta suluhisho la matatizo ya afya Barani, na kufikia ushirikiano wa kiafya kati ya nchi za Afrika.
Mkutano huo, katika toleo lake la kwanza, ulifanyika na kauli mbiu "Lango Lako la Ubunifu na Biashara", na ulizinduliwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi mwaka jana, ulioandaliwa na Mamlaka ya Ununuzi wa Pamoja, Ufadhili wa Matibabu na Ufadhili wa Misri na Idara ya Teknolojia ya Matibabu; Vikao zaidi ya 350 vya kisayansi na warsha 20 zilifanyika, kwa ushiriki wa wasemaji zaidi ya 800 na wataalam wa kimataifa katika uwanja wa matibabu, zaidi ya wanachama 400 wa Chumba cha Huduma ya Afya na idadi ya makampuni ya kimataifa na ya ndani yanayofanya kazi katika sekta mbalimbali za huduma za matibabu.
Shughuli za Maonesho na Mkutano huo, uliofanyika kwa muda wa siku tatu mnamo kipindi cha 5 hadi 7 Juni 2022 , katika Kituo cha Maonesho cha Kimataifa cha Misri (Kituo cha Al-Manara cha Mikutano ya Kimataifa) Fifth Settlement area huko Kairo mpya, ilijumuisha vikao mbalimbali vilivyokagua teknolojia za hivi karibuni zaidi za teknolojia katika nyanja mbalimbali za matibabu, pamoja na kuwasilisha na kujadili idadi ya mipango muhimu katika uwanja wa matibabu, ambayo huongeza jukumu la mkutano kama jukwaa endelevu linalounganisha washirika wote wa afya Duniani, chini ya paa moja.
Mipango itakayojadiliwa na kuwekwa , ukiwemo mpango wa Misri wa kutokomeza saratani ya kizazi, hivyo mbele ya wataalam kadhaa wa kimataifa na wawakilishi wa mashirika na taasisi za serikali nchini Misri kwa lengo la kuwakinga wanawake wa Misri na Afrika dhidi ya saratani ya kizazi. pamoja na mjadala muhimu kuhusu mpango wa Rais wa Jamhuri wa kuwatibu wagonjwa wa kuharibika kwa misuli.
Mkutano na Maonesho hayo pia yalitoa fursa ya kielimu kupitia vikao vya mihadhara ya kisayansi, vikao vya mafunzo na warsha, ambazo zilishughulikia mada zilizozoeneza zaidi katika sekta hii, ambayo Kamati ya ufundi ilijumuisha takriban wataalamu ishirini na tisa waliopopea katika sekta mbalimbali na taasisi za matibabu ilitayarisha na kusimamia vikao na warsha hiyo.
Maonesho na Mkutano wa kwanza wa matibabu wa Kiafrika ni jukwaa la mazungumzo kati ya nchi za Kiafrika kubadilishana uzoefu kati yao, na kuratibu na kampuni za kimataifa ili kusaidia kupata suluhisho la matatizo ya kiafya katika kiwango cha bara la Afrika kulingana na maono ya 2030 ya Misri, Ajenda ya Umoja wa Afrika na malengo ya Umoja wa Mataifa, ambayo yote yanalenga kusaidia kutatua matatizo ya afya katika bara la Afrika na kutoa maisha yenye afya na salama kwa raia.
Mkutano na Maonesho ya Kiafya ya Kiafrika huwaleta pamoja wawakilishi wote wa huduma za afya ili kuwapa fursa ya kipekee ya kuchunguza kile kinachotolewa katika sekta mbalimbali kama vile vifaa vya matibabu, vifaa vya matibabu, dawa, vifaa vya matumizi ya maabara na kemikali, vifaa vya meno na vifaa ngozi, lishe na vitamini, Watoa huduma za afya, maduka ya dawa, huduma za afya, viwanda vya chakula na ufungaji.
Vyanzo:
Tovuti la Maonesho na Mkutano wa kwanza wa Matibabu la Kiafrika.
Tovuti ya Urais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri .
Tovuti ya Mamlaka ya Madawa ya Misri.
Tovuti ya Taasisi Kuu ya Taarifa.
Gazeti la Al- Ahram la Misri.