Baraza la Wawakilishi la Misri

Baraza la Wawakilishi la Misri

Baraza la Wawakilishi ni mamlaka ya kutunga sheria katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na linatekeleza utaalamu mbalimbali ulioainishwa katika katiba ya 2014, ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 101 cha sura ya kwanza kutoka Jalada ya Tano, Baraza la Wawakilishi lina mamlaka ya kutunga sheria, na kuidhinisha sera kuu ya nchi, na mpango wa jumla wa maendeleo.

Sheria za zamani zaidi katika historia ya wanadamu

Misri ilitoa mifumo ya zamani zaidi ya kisheria na kiutawala kwa ubinadamu. Ambapo katika ukingo wa Mto wake wa Nile, serikali kongwe zaidi ilianzishwa, iliyojenga ustaarabu mkuu wa binadamu, na kwa enzi zote, ustaarabu wa hali ya juu wa Misri ulifululiza na ulistawi kwa kuzingatia misingi nguvu na iliyoimarishwa vyema katika mifumo na sanaa za utawala na usimamizi.

Ambapo takriban miaka 5,200 iliyopita, Mfalme Mena, mwanzilishi wa familia ya kwanza ya Mafarao, aliweza kuunganisha pande mbili za kikabila na bahari (kusini na kaskazini) huko Misri ili kuwa nchi yenye umoja, na aliweka mifumo ya zamani zaidi ya kutunga sheria katika historia ya mwanadamu, alipofanya sheria ya Thot, Mungu wa hekima, sheria iliyounganishwa iliyotawala katika Misri yote, na alichukua mji wa Memphis, kama mji mkuu na kituo cha utawala cha serikali kuu ya kwanza iliyounganishwa katika historia, inamiliki chombo kilichopangwa katika utawala, usimamizi, mahakama, elimu, polisi, jeshi na mengineyo.

Athari za ustaarabu wa Mafarao zinaonesha kiwango ambacho Wamisri walifikia maendeleo katika mifumo ya utawala na usimamizi. Ambapo mfalme (Farao) alikuwa mkuu wa nchi, na aliweka mtunza mkuu wa hazina au mtoza wa ushuru. Na kulikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi walioteuliwa kwa amri ya kifalme na kuhitimu katika kazi zao. Pia, tangu enzi ya Ufalme wa Kale, Misri imetumia mfumo mzuri wa serikali za mitaa.

Tangu enzi ya familia ya tatu na nne ya nchi la kale la Misri, amri na sheria mbalimbali zilionekana, kama vile sheria iliyoamua saa za kazi za mkulima, na sheria ya Mfalme Menkaure, iliyolenga kupambana na wachawi.

Tunaweza kutambua kiwango cha maendeleo na utofauti wa kazi zinazofanywa na serikali kutokana na kusoma maandishi ya kaburi la Rakhmi Ra, waziri mkuu na hakimu mkuu wa Mfalme Thutmose wa Tatu, kwenye kuta za kaburi lake huko Teba, ambapo yalijumuisha rekodi kamili ya sheria inayoelezea kazi na wadhifa za Waziri.

Katika enzi ya serikali ya kisasa ya Mafarao, jukumu la Mfalme Horemoheb, anayechukuliwa kama mmoja wa wabunge muhimu zaidi katika historia ya ubinadamu, liliibuka. Ambapo sheria yake ilikuwa na sifa ya asili ya kiraia mbali na masuala ya kidini, pia aliangalia kutoa sheria nyingi zinazodhibiti uhusiano kati ya mtu binafsi na mamlaka inayotawala. Vilevile, sheria yake ilikuwa na nafasi ya kwanza katika kuweka wazo la uhuru na haki za umma kama vile utakatifu wa nyumba na utakatifu wa barabara. Na pia alithibitisha wazo la ofisi ya umma ni huduma kwa watu na sio njia ya kuwatawala..na kuwa mfanyakazi wa umma ni mtumishi wa watu na si bwana juu yao.

Ustaarabu wa Mafarao uliacha athari nyingi na shahidi za maendeleo hayo ya utawala na kisheria, ikiwa ni pamoja na maandishi yanayopatikana kwenye kaburi la binti mfalme Idot huko Sakara, ambayo ni sheria ya kale zaidi ya kodi katika historia.

Na mara nyingi, Wamisri wa kale walisajili kwenye mahekalu na makaburi yao picha za mfalme akiwasilisha Maat, ishara ya haki na sheria kwa Miungu, kama ishara wazi ya utakaso wa dhana na maadili ya haki na utawala wa sheria.

Baada ya Alexander Mkuu alipoingia Misri mwaka wa 330 BC, utawala wa Wagiriki wa Misri ulianza, na baada ya kifo chake kikaja kipindi cha Ptolemaiki na kisha utawala wa Warumi, na licha ya ukali wa utawala wa Warumi, Wamisri waliweza kuhifadhi mila zao nyingi, mifumo, na desturi mpaka Ukristo ulipoingia Misri katika nusu ya kwanza ya karne ya kwanza, ambapo Kanisa la Misri lilichangia katika uimarishaji wa mifumo na mila kemkem.

Katika zama za Kiislamu, mifumo ya serikali na sheria ilitokana na Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtukufu Mtume (S.A.W) kwa kuzingatia kanuni ya Shura, ambayo ni moja ya kanuni za msingi katika mifumo ya utawala katika Uislamu.

Wakati Misri ilipokuwa mji mkuu wa Ukhalifa wa Fatimi (969-1171), mifumo ya utawala na sheria iliboreshwa, na mji wa Kairo ulipangwa kuwa mji mkuu wa Misri na Ukhalifa wa Kiislamu.

Na mnamo enzi ya nchi ya Ayyubid (1171-1250), ngome hiyo ikawa makao ya utawala na kitovu cha mamlaka, na mabaraza ya sheria na mahakama yalitofautiana. Ambapo baraza la haki na baraza la kuchunguza kero na mengineyo lilianzishwa. Na kazi za mabaraza hayo zilijumuisha kutoa sheria na kanuni na kufanya mikataba na nchi za nje.

Mnamo zama za Mamluk (1250-1517), Sultani Al-Zahir Baybars alijenga Nyumba ya Haki katika Ngome ya Salah al-Din al-Ayyubi ili kuwa makao ya serikali. Na utaalamu wa Baraza la Utawala katika enzi hiyo ulijumuisha utoaji na utekelezaji wa sheria na utatuzi wa migogoro, pamoja na kufanya mazungumzo na nchi jirani.

Katika enzi ya Uthmaniyya (1517-1805), mahakama za Sharia zilikuwa mfumo uliotumika nchini Misri, na majaji walitumia hukumu kutoka kwa Sharia moja kwa moja kwa migogoro yote ya kiraia, ya jinai na kesi za Sharia, na suala hili lilibakia hadi mwisho wa karne ya 18.

Mnamo miaka ya mwisho ya karne ya 18, Misri ilishuhudia maendeleo muhimu ya kisiasa na ya kijamii katika kiwango cha mawazo na mazoezi. Ambapo mnamo mwaka wa 1795, baada ya miaka sita baada ya Mapinduzi ya Ufaransa, Kairo ilishuhudia maasi makubwa ya kijamii na kisiasa kwa ajili ya haki, uhuru, na utawala wa sheria. Ndani yake, misimamo ya vikosi vya kitaifa na viongozi maarufu juu ya maswala ya watu ilijitokeza kimsingi, na safu ya mbele ya vikosi hivi ikapitisha matakwa ya kitaifa ya haki, usawa na uhuru. 

Katika mfumo wa kuongezeka kwa upinzani maarufu dhidi ya Mtawala wa Uthmaniyya na Mamluk. Misri ilikuwa karibu sana na mapinduzi makubwa ya watu yaliyopelekea wasomi na viongozi maarufu kutoa hoja iliyoandikwa kutoka kwa Mtawala wa Uthmaniyya na Mamluk. Hoja hii ilikuwa kama MagnaKarta (mkataba mkuu zaidi) ya kwanza ya Misri, ambapo ilitamani kuweka udhibiti wazi wa uhusiano kati ya mtu binafsi na mamlaka kuhusu kutotozwa faini au kodi bila ya idhini ya wanazuoni wa Al-Azhar kama wawakilishi wa watu.

Baraza Kuu

Mnamo Mei, mwaka wa 1805, Misri ilishuhudia mapinduzi ya kwanza ya kidemokrasia yaliyokomaa katika zama za kisasa. Ni mapinduzi yaliyoongozwa na wanazuoni wa Al-Azhar na makundi yote ya watu walishiriki katika mapinduzi hayo. Na viongozi wa mapinduzi hayo, yalimweka Muhammad Ali Pasha kama Mtawala wa Misri kwa jina la watu bila kungoja Sultani wa Uthmaniyya atume Mtawala kupitia yeye.

Muhammad Ali alipewa dhamana ya utii kama mtawala kwa masharti ya watu, yaliyojumuisha wazo la taifa ndio chimbuko la mamlaka. Ambapo masharti haya yalibainisha kuwa jambo hilo limekamilika baada ya mkataba wa aendelee na uadilifu, aweke hukumu na sheria, aache malalamiko, na asifanye amri isipokuwa kwa ushauri wa wanachuoni. Na alipokiuka masharti, wakamfukuza. Na baada ya ukombozi wake kwa kutawala Misri, Muhammad Ali alianza mapinduzi ya kiutawala ya kina ili kuanzisha taasisi za kisasa za utawala, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa bunge la kisasa la uwakilishi.

Na mnamo mwaka wa 1824, Baraza Kuu liliundwa, ambalo ni mwanzo halisi wa bunge la kwanza, ambalo baadhi ya wajumbe wake wanachaguliwa kwa njia ya uchaguzi, na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya watu unazingatiwa, kama ulijumuisha wanachama 24 hapo mwanzo, kisha idadi yake ikawa wanachama 48 baada ya kuongeza masheikh 24 na wanachuoni kwake. Kwa hivyo, iliundwa na wasimamizi wa ofisi, wakuu wa idara, wanazuoni wawili waliochaguliwa na Sheikh wa Al-Azhar, wafanyabiashara wawili waliochaguliwa na mfanyabiashara mkuu wa mji mkuu, watu wawili wenye ujuzi wa hesabu, na watu wawili mashuhuri kwa kila moja ya kurugenzi za nchi ya Misri zilizochaguliwa na wananchi.

Mnamo Januari ya mwaka wa 1825, Orodha ya kimsingi ya Baraza Kuu ilitolewa, ikifafanua utaalamu wake kama kujadili kile ambacho Muhammad Ali aliona au alichopendekeza kuhusu sera yake ya ndani. Na pia orodha hiyo ya msingi ilijumuisha nyakati za mikutano na njia ya kazi ya baraza. 

Baraza la Ushauri

Mafanikio ya Baraza Kuu yalisababisha kuanzishwa kwa baraza jingine mwaka wa 1829, nalo ni Baraza la Ushauri, ambalo ni kiini muhimu cha mfumo wa Ushauri, ambapo baraza hili lilikuwa na viongozi wakuu wa serikali, wasomi na watu mashuhuri wakiongozwa na Ibrahim Pasha. Baraza hilo lilikuja kwa idadi ya wajumbe wake na uwakilishi wao wa makundi mbalimbali ya wananchi kama mkutano mkuu unaojumuisha wajumbe 156:- 33 kati yao ni maafisa wakuu na wanazuoni, 24 ni makamishna wa mikoa, na 99 ni wajumbe waandamizi wa nchi ya Misri wanaochaguliwa kwa uchaguzi. Na Baraza la Ushauri liliitishwa ili kushauriana naye kuhusu masuala ya elimu, utawala na kazi za umma. Na mnamo mwaka wa 1830, seti ya maagizo ilitolewa kwa baraza hili iliyojumuisha kanuni na mbinu za kazi yake. Na mnamo mwaka wa 1833, Baraza la Ushauri lilitunga sheria yake yenyewe  iliyokuwa nyongeza ya maagizo yaliyotangulia, na ilishughulikia mpangilio wa vipindi vyake vya kuitisha, taratibu za mashauri yake, na maamuzi yaliyotolewa nayo.

Mnamo mwaka wa 1837, Muhammad Ali alitoa Sheria ya Msingi ya Dola, "Al-Seyasatnamah", iliyofuta Baraza la Ushauri na badala yake kuweka mabaraza mawili: "Baraza Maalum" la kutunga sheria, na "Baraza Kuu" ili kujadili mambo yanayoelekezwa kwake na serikali. Na serikali imepangwa katika ofisi saba za msingi.

Baraza la ushauri la Wawakilishi

Mwaka wa 1866 ulishuhudia hatua muhimu zaidi katika maendeleo ya maisha ya ubunge nchini Misri, kwa kuanzishwa kwa "Baraza la Wawakilishi la Ushauri" wakati wa enzi ya Khedive Ismail. Baraza hilo linachukuliwa kama bunge la kwanza kuwa na utaalamu wa kibunge, na sio tu baraza la ushauri ambalo kwa sehemu kubwa lina sifa ya utawala. Na amri ya Khedive ya kuanzisha Baraza ilitolewa mnamo Novemba, mwaka wa 1866, ikijumuisha orodha ya kimsingi na orodha ya kawaida za Baraza.

Na orodha ya kimsingi ilijumuisha vifungu 18: vilijumuisha mfumo wa uchaguzi, mahitaji ya kisheria ya kufaa kwa mshiriki mgombea, na vipindi vya mikutano ya baraza.

Mamlaka ya Baraza hilo yalijumuisha "kujadili mambo ya ndani, na kutoa ushauri kwa Khedive". Na kanuni za Baraza hilo ziliathiriwa sana na mifumo ya bunge iliyokuwa ikitumika Ulaya wakati huo, haswa Bunge la Ufaransa.

Baraza la Wawakilishi la Ushauri lilikuwa na wajumbe 75 waliochaguliwa na watu mashuhuri: huko Kairo, Alexandria, na Damietta, na mameya na masheikh wa miji katika wilaya zingine, waliochaguliwa kwa mara ya kwanza wakati wa enzi ya Khedive Ismail.

Pamoja na mwenyekiti wa Baraza, aliyeteuliwa kwa amri ya Khedive. Na muda wa Baraza ulikuwa wa miaka mitatu, huko kila mwaka huwekwa kwa muda wa miezi miwili. Baraza la Wawakilishi la Ushauri lilifanya vikao tisa juu ya vyombo vitatu vya uwakilishi, kuanzia tarehe 25 Novemba, mwaka wa 1866 hadi Julai 6, mwaka wa 1879.

Baada ya muda, mamlaka ya Baraza yaliongezeka polepole, na kiini cha mwelekeo wa upinzani ulianza kuonekana. Na maendeleo haya yalisaidiwa na kuenea kwa mawazo ya mwangaza mikononi mwa kundi la wanafikra na waandishi wakubwa.

Pamoja na kupatikana kwa magazeti wakati huo, jambo lililoimarisha hitaji la watu wengi la kuanzishwa kwa baraza la uwakilishi lenye mamlaka mapana ya kutunga sheria na usimamizi. Madai haya yalijitokeza mnamo mwaka wa 1878, wakati Baraza la Mawaziri la kwanza lilipoanzishwa nchini Misri (Baraza la Wasimamizi).

Bunge liliundwa upya, na mamlaka zaidi yakalitolewa, ingawa baadhi ya mambo yalisalia nje ya mamlaka ya bunge, kama vile baadhi ya masuala ya fedha. Mnamo Juni mwaka wa 1879, orodha mpya ya msingi ya Baraza la Wawakilishi la Ushauri ilitayarishwa kwa maandalizi ya kuiwasilisha kwa Khedive kwa ajili ya kutolewa, iliyofanya idadi ya manaibu kuwa manaibu 120 wanaowakilisha Misri na Sudan.

Jambo muhimu zaidi lililojumuishwa katika orodha lilikuwa: ripoti ya "wajibu wa Wizara", na kutoa mamlaka makubwa kwa Baraza katika masuala ya kifedha.

Hata hivyo, Khedive Tawfik, aliyeteuliwa mnamo Juni 26, mwaka wa 1879, aliikataa orodha hiyo na alitoa amri ya kuvunja baraza.. lakini licha ya hilo, baraza liliendelea kufanya vikao vyake hadi mwezi wa Julai, mwaka wa 1879.

Baraza la Wawakilishi la Misri

Mnamo  Septemba 9, 1881, Mapinduzi ya Urabi yalizuka, na miongoni mwa matakwa yake yalikuwa kuundwa kwa Bunge. Hakika, uchaguzi ulifanyika kwa Baraza la Wawakilishi la Shura kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya Baraza iliyotolewa mwaka 1886, ikisubiri maandalizi ya serikali ya rasimu mpya ya sheria ya msingi itakayowasilishwa kwenye Baraza kwa ajili ya kuidhinishwa, na Baraza jipya, ambalo liliitwa “Baraza la Wawakilishi la Misri” lilifunguliwa mnamo Desemba 26, 1881, na serikali iliwasilisha rasimu ya Sheria ya Msingi, na amri kuu ilitolewa mnamo Februari 7, 1882, na sheria hii ilifanya Wizara kuwajibika kwa Bunge lililochaguliwa na wananchi, pia lililokuwa na uwezo wa kutunga sheria na haki ya kuwahoji na kujadili na mawaziri.

Muda wa Bunge la Misri ukawa miaka mitano, na kikao hicho ni miezi mitatu.

Hivyo, kanuni za utendaji wa kidemokrasia wa Bunge nchini Misri zilianzishwa hatua kwa hatua, lakini hii haikudumu kwa muda mrefu, kwani Baraza la Wawakilishi la Misri liliitisha kikao kimoja cha kawaida kuanzia Desemba 26, 1881 hadi Machi 26, 1882, kisha Uingereza ikaikalia Misri mwaka 1882, na kufuta Sheria ya Msingi, na kutolewa mwaka 1883 kile kilichoitwa sheria ya kawaida, iliyokuwa kikwazo kwa maisha ya Bunge nchini Misri.

Baraza la Kutunga Sheria

Mnamo Julai 1913, Baraza la Ushauri la Sheria  na Mkutano Mkuu zilifutwa. Bunge lilianzishwa, lililokuwa na wajumbe 83: miongoni mwao 66 waliochaguliwa na 17 waliteuliwa. Sheria ya kisheria iliyotolewa mwanzoni mwa Julai mwaka huo huo ilieleza kuwa muda wa Bunge utakuwa miaka sita. Chama hicho kilidumu kuanzia Januari 22, 1914 hadi Juni 17, 1914, wakati Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilipozuka na sheria ya kijeshi ilipotangazwa nchini Misri. Kisha, mnamo Desemba 1914, Uingereza ilitangaza ulinzi juu ya Misri, na mkutano ukaahirishwa kwa muda usiojulikana.

Mwaka 1915, vifungu vya sheria ya kisheria vilisitishwa hadi Bunge lilipofutwa Aprili 1923.

Baraza la Ushauri la Sheria

Sheria ya Kisheria iliyotolewa mwaka 1883 ilijumuisha kuundwa kwa Bunge la Misri kutoka vyumba viwili: “Baraza la Ushauri la Sheria” na “Mkutano Mkuu”. Sheria hiyo pia ilianzisha halmashauri za wilaya, kazi yake ilizokuwa ya kiutawala badala ya kutunga sheria, lakini zilizokuwa na uwezo wa kuchagua wajumbe wa Baraza la Shura la Sheria.

Baraza la Ushauri la Sheria linaweza kuwa na wajumbe 30: wajumbe 14 walioteuliwa, akiwemo Spika na mmoja wa manaibu wawili, na wajumbe 16 waliochaguliwa, akiwemo naibu wa pili wa Baraza. Muda wake ulikuwa miaka 6. Kwa upande wa Baraza Kuu, lilikuwa na wajumbe 83: wajumbe 46 waliochaguliwa, wajumbe wengine wa zamani, wajumbe wa Baraza la Sheria la Shura, na mawaziri saba. Mkutano Mkuu unaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Sheria Shura. Kuanzia 1883 hadi 1913, Baraza la Sheria Shura na Mkutano Mkuu walikutana katika vikao 31 katika vyombo vitano vya Bunge.

Katiba ya 1923

Baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, mapinduzi ya Misri yalizuka mwaka 1919, yakidai uhuru wa Misri, na kuanzishwa kwa maisha ya uwakilishi na demokrasia kamili.

Mapinduzi hayo yalisababisha kutangazwa kwa azimio la Februari 28, 1922, lililotambua Misri kama nchi huru (na Masharti manne) na kuhakikisha kusitishwa kwa udhibiti wa Uingereza juu ya Misri.

Kulingana na ukweli huu mpya. Katiba mpya iliandaliwa Aprili 1923 na kuandaliwa na kamati ya wajumbe thelathini iliyojumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi maarufu, na viongozi wa Harakati ya kitaifa.

Katiba ya 1923 ilianzisha mfumo wa uwakilishi wa buynge kwa kuzingatia utengano na ushirikiano kati ya madaraka. Uhusiano kati ya matawi ya kutunga sheria na utendaji uliandaliwa kwa misingi ya kanuni ya udhibiti na usawa. Iliifanya Wizara hiyo kuwajibika kwa Bunge, ambalo lina haki ya kupiga kura ya imani nalo. Wakati akitoa haki ya mfalme kulivunja bunge na kuliita kuitisha, lakini akalipa bunge haki ya kukutana kwa mujibu wa katiba kama halikuitwa kwa wakati.

Katiba ya 1923 ilipitisha mfumo wa mabaraza hayo mawili: Seneti na Baraza la Wawakilishi. Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, Katiba inaeleza kuwa wajumbe wake wote wanachaguliwa, na muda wa kukaa madarakani ni miaka mitano.

Bunge la Seneti, 3/5 ya wajumbe wake walichaguliwa na 2/5  waliteuliwa. Katiba ilipitisha kanuni ya mamlaka sawa kati ya vyumba hivyo viwili kama kanuni ya jumla, isipokuwa baadhi.

Idadi ya wajumbe wa vyumba vyote viwili iliongezeka mara kwa mara, kwani Katiba ilipitisha kanuni ya kupunguza idadi ya wajumbe wa mabunge yote mawili kwa asilimia fulani ya wananchi. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa Katiba ya 1923 walikuwa wajumbe 214 na waliendelea pia kutoka mwaka 1924 hadi 1930, kisha wakaongezeka hadi wajumbe 235, kisha idadi ikapungua chini ya Katiba ya 1930, iliyoendelea kutumika kutoka 1931 hadi 1934 hadi wajumbe 150, kisha idadi ikaongezeka tena chini ya marejesho ya Katiba ya 1923, ambayo iliendelea kutumika kutoka 1936 hadi 1952 hadi wajumbe 232 kutoka 1936 hadi 1938, baadaye idadi ikawa wanachama 264 kutoka 1938 hadi 1949, na kisha ikaongezeka mwaka 1950 hadi wanachama 319 na kubaki hivyo hadi Mapinduzi ya Julai mwaka 1952.

Bunge hilo lililoainishwa katika Katiba ya Misri iliyotolewa mwaka 1923, lilikuwa ni hatua ya hali ya juu katika mfumo wa maisha ya bunge na mabaraza nchini Misri, lakini utaratibu huo uligubikwa na mabaya mengi, hivyo maisha ya kisiasa katika kipindi cha kuanzia mwaka 1923 hadi 1952 yalikuwa kati ya vipindi vya wimbi dogo la kidemokrasia na maarufu, na vipindi vya kupungua vilivyotokana na kuingilia kati kwa mamlaka za uvamizi na ikulu ilichukua sehemu kubwa ya kipindi hiki, jambo lililosababisha kuvunjwa kwa bunge takriban mara kumi. Aidha, mwaka 1930 ulishuhudia utoaji wa katiba mpya ya nchi, ambayo ilidumu kwa miaka mitano ambayo ilikuwa kikwazo kwa maisha ya kidemokrasia, hadi nchi iliporejea tena kwenye katiba ya 1923 mwaka 1935.

Hivyo, hali ya kikatiba ilizorota kwa sababu za ndani na nje kufikia dola ambayo nchi ilikuwa kabla ya mapinduzi ya 1952, ambayo ilikuwa na sifa ya kukosekana kwa utulivu mkubwa wa kisiasa na kiserikali, kiasi kwamba Misri iliadhibiwa na wizara 40, na mabadiliko ya mawaziri, katika kipindi cha kuanzia 1923 hadi 1952.

Maisha ya bunge nchini Misri baada ya mapinduzi ya 1952

Moja ya misingi ya mapinduzi ya Julai 23, 1952 nchini Misri ilikuwa kanuni ya “kuanzisha Maisha sawa ya kidemokrasia ”, baada ya mapinduzi kufuta katiba iliyopita, kutangaza jamhuri na kuvunja vyama.

Mwaka 1956, katiba mpya ilitangazwa, kwa mujibu wa Bunge liliundwa Julai 22, 1957 kutoka kwa wajumbe 350 waliochaguliwa, na bunge hili liliahirisha kikao chake cha kwanza cha kawaida Februari 10, 1958.

Mnamo Februari 1958, kutokana na kuanzishwa kwa umoja kati ya Misri na Syria, katiba ya 1956 ilifutwa, na katiba ya mpito ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu ilitolewa Machi 1958, kwa msingi ambapo bunge la pamoja la wateule liliundwa (wajumbe 400 kutoka Misri na wajumbe 200 kutoka Syria) na mkutano wa kwanza ulifanyika Julai 21, 1960 na kuendelea hadi Juni 22, 1961, kisha utengano kati ya Misri na Syria ulitokea Septemba 28, 1961.

Mnamo Machi 1964, katiba nyingine ya mpito ilitolewa nchini Misri, kwa msingi ambao Bunge lilianzishwa likiwa na wajumbe 350 waliochaguliwa, angalau nusu yao walikuwa wafanyakazi na wakulima, ikionesha utoaji wa sheria za ujamaa za Julai 1961, pamoja na manaibu kumi walioteuliwa na Rais wa Jamhuri.

Baraza hilo lilidumu kuanzia Machi 26, 1964 hadi Novemba 12, 1968 na uchaguzi wa Baraza jipya ulifanyika Januari 20, 1966, ambao nao uliendelea kuwepo hadi Agosti 30, 1971, Bunge lilipotekeleza vikao vyote hivi mamlaka yake ya kikatiba.

Kisha katiba mpya ikatolewa kwa ajili ya nchi mnamo Septemba 11, 1971, iliyoendelea kutumika hadi tamko la katiba lilipotolewa mnamo  Februari 13, 2011 baada ya mapinduzi ya Januari 25, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kusitisha kazi ya vifungu vyake.

Mnamo 1976, uchaguzi wa wabunge ulifanyika kwa misingi ya majukwaa mengi ndani ya Umoja wa Kisoshalisti wa Kiarabu, shirika pekee la kisiasa lililokuwepo wakati huo.

Mwaka 1979, uchaguzi wa kwanza wa wabunge nchini Misri ulifanyika kwa misingi ya vyama, kwa mara ya kwanza tangu kufutwa kwa vyama vya siasa nchini Misri baada ya mapinduzi ya Julai 1952, ambapo vyama kadhaa vya siasa viliundwa baada ya kutolewa kwa Sheria ya Vyama vya Siasa mwaka 1977 vilishiriki.

Mwaka 1980, Baraza la Ushauri lilianzishwa, kwa lengo la kupanua mzunguko wa ushiriki wa kisiasa na kidemokrasia. Hata hivyo, mfumo wa upigaji kura wa mtu binafsi umerejeshwa. Mwaka 1990, amri kwa mujibu wa sheria ilitolewa ya kurejea katika mfumo huo, na jamhuri iligawanywa katika majimbo 222 ya uchaguzi, kila moja iliyochagua wajumbe wawili, angalau mmoja wao angekuwa wafanyakazi na wakulima. 

Idadi ya wajumbe wa Bunge la Wananchi ikawa wajumbe 454, wakiwemo wajumbe kumi walioteuliwa na Rais wa Jamhuri, na baada ya mapinduzi ya Januari 25, Sheria ya Uchaguzi ya Bunge la Wananchi na Baraza la Shura Na. 38 ya mwaka 1972 ilifanyiwa marekebisho na kuwa uchaguzi wa theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge la Wananchi kwa mfumo wa orodha ya vyama vilivyofungwa na theluthi nyingine kwa mfumo wa mtu binafsi, na idadi ya wajumbe wa Baraza kulingana na marekebisho hayo ikawa wajumbe 498 waliochaguliwa kwa uchaguzi wa siri wa moja kwa moja wa umma, ili mradi angalau nusu yao ni wafanyakazi na wakulima, pamoja na manaibu 10 kwa ujumla. Wanaweza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri.

Maisha ya kisiasa ya Misri yalishuhudia kushamiri kwa vuguvugu la wananchi kutokana na kuzuka kwa mapinduzi ya Januari 25 na Juni 30, ikifuatiwa na chaguzi kadhaa za wabunge zilizosababisha kuibuka kwa bunge la sasa chini ya katiba ya 2014, iliyopigiwa kura na wananchi Januari 18, 2014, ambayo ilirejesha mfumo usio wa kawaida kuwa bunge la Misri pamoja na jina la Baraza la Wawakilishi mnamo 2016, na baraza la sasa ni mafanikio yasiyo ya kawaida katika historia ya maisha ya Bunge nchini Misri, iwe kwa mujibu wa uwezo uliokabidhiwa chini ya katiba ya 2014 au kwa upande wa safu ya kipekee, inayojumuisha kwa mara ya kwanza wanawake 90 kwa (15%) ya wanachama wake wote, pamoja na uwakilishi wa walemavu na (9) wanachama, na Wamisri nje ya nchi na wajumbe 9, pamoja na asilimia ya vijana chini ya miaka 35, inayofikia zaidi ya robo ya wabunge, ili bunge la 2016 liwe hatua muhimu katika historia ya maisha ya bunge nchini Misri, ikiandika kwa barua za mwanga sura mpya katika kumbukumbu ya historia yake ya bunge la kale, ambayo ni epic ya kipekee ya kitaifa  inayoshuhudiwa Historia juu ya kina na utukufu wa uzoefu wa bunge la Misri kati ya mabunge ya ulimwengu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 102, Baraza la Wawakilishi litakuwa na wajumbe wasiopungua mia nne na hamsini, watakaochaguliwa kwa kura ya siri ya moja kwa moja, mradi masharti ya kugombea, mfumo wa uchaguzi, na mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi yazingatie uwakilishi wa haki wa wananchi, majimbo, na uwakilishi sawa wa wapiga kura. Kifungu hicho pia kinamruhusu Rais wa Jamhuri kuteua wajumbe kadhaa wasiozidi asilimia 5, mradi sheria iamue namna ya kuwateua, na kwa mujibu wa Ibara ya 106 ya Katiba, muda wa uanachama wa Baraza la Wawakilishi ni miaka mitano ya Gregori, kuanzia tarehe ya mkutano wake wa kwanza.

Kwa mujibu wa kifungu cha 107, mamlaka ya kuamua juu ya uhalali wa uanachama wa wajumbe wa Baraza hilo yalifanyika na Mahakama ya Kadhi, na rufaa zitawasilishwa kwake ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini kuanzia tarehe ya kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi, na rufaa hiyo itaamuliwa ndani ya siku sitini kuanzia tarehe ya kupokelewa kwake, na uanachama utachukuliwa kuwa batili – wakati mahakama itakapoamua – kuanzia tarehe ya kuliarifu Baraza la uamuzi.

Uanachama wa mwanachama hauwezi kufutwa isipokuwa atapoteza imani na umakini, kupoteza moja ya masharti ya uanachama kwa misingi aliyochaguliwa, au kukiuka majukumu yake, na uamuzi wa kuacha uanachama utakuwa kwa theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (Ibara ya 110) na hairuhusiwi, isipokuwa kwa upande wa flagrante delicto, kuchukua hatua yoyote ya jinai dhidi ya mjumbe katika ibara za makosa na makosa isipokuwa kwa ruhusa ya awali kutoka Baraza.

 Jengo la Bunge

Jengo la Bunge la Misri katikati ya mji wa Kairo lina thamani kubwa ya kihistoria na usanifu. Ni ishara ya maadili na kanuni ambazo watu wa Misri wamezipigania kwa miaka mingi. 

Jengo hilo, ambalo kwa sasa lina baraza la wawakilishi na Baraza la Shura, limeshuhudia matukio muhimu katika historia ya kisasa ya Misri na maandamano ya kazi ya kitaifa ndani yake, tangu kufunguliwa kwake mnamo 1924 kupokea bunge la kwanza la kisasa la Misri baada ya kutolewa kwa katiba ya 1923. 

Ndani ya jengo hilo, kikao cha kwanza cha Seneti na Baraza la Wawakilishi kilifanyika Jumamosi ya Machi 15, 1924. 

Jengo hili ni shahidi hai wa ukweli wa zaidi ya miaka sabini ya maisha ya kisiasa na kibunge nchini Misri.
 
Jengo hilo lina thamani ya jumla ya kisanii na usanifu, kwani lilijengwa kwa mtindo uliounganisha mitindo ya usanifu wa Ulaya mwishoni mwa karne ya kumi na tisa na mapema karne ya ishirini na ushawishi wa Kiislamu katika usanifu na sanaa.

Ubunifu wa usanifu wa jengo hilo una ukumbi mkuu wa mviringo wenye kipenyo cha mita 22 na urefu wa mita 30 uliopigwa na kuba yenye sehemu ya mviringo iliyofunikwa na kioo katikati… Sehemu hii inapigwa na panya mwenye kuba ndogo ya chini… Rattle ina madirisha manne na nje ya kuba kuna bendi maarufu zinazowakilisha vitengo maarufu vya mapambo vya mara kwa mara… Kitovu cha duara kutoka ndani kimezungukwa na motifu za maua zinazowakilisha mtindo uliotawala katika miaka ya ishirini wakati wa ujenzi… Ukumbi huo una ghorofa mbili, kila moja ikiwa na balcony… Kuhusu mbele ya ukumbi, tunapata katikati nembo ya Jamhuri na kisha jukwaa la rais… Mabawa kadhaa yameunganishwa ukumbini, ikiwa ni pamoja na ushawishi wa Farao na nyumba nyingine ya Rais wa Jamhuri na Waziri Mkuu. 

Mnamo miaka ya hivi karibuni, jengo jingine la kihistoria lililokaliwa na Wizara ya Umwagiliaji na Kazi za Umma limejumuishwa katika jengo la Bunge, ambalo lina mtindo wa usanifu sawa na jengo la Bunge. 

Kazi ya matengenezo na marejesho hufanywa kwa kudumu ili kuhifadhi thamani hii muhimu ya usanifu na kihistoria. 

Vyanzo 

Tovuti ya Baraza la Wawakilishi la Misri.