Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ni miongoni mwa wahitimu wa mpango wa Urais katika shughuli za sherehe ya Hitimisho ya Jukwaa la Vijana Duniani

Ahmed Mukhtar, Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa alishiriki katika shughuli za Jukwaa la Vijana Duniani, miongoni mwa wahitimu wa kundi la pili la mpango wa Urais katika urekebishaji wa watendaji kuongoza kundi la "Jenerali Assar" , ambapo sherehe ya kuhitimu kwa programu za Chuo cha Taifa cha mafunzo ilifanyikwa wakati wa shughuli za Jukwaa , kwa mahudhurio ya Mheshimiwa Rais Abd El Fatah al-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Kwa upande wake، Mukhtar anasifu ushiriki wake katika mpango wa Urais wa urekebishaji wa viongozi watendaji kama uzoefu wa kujifunza na kujihusisha kamili kwa uzoefu na ujuzi mzito pia kuandaa mtu tayari kuongoza nchi.
Anaeleza uzoefu wake wa kazi ya umma na kisiasa na ushiriki wake katika mpango wa Urais, akisema: "Sasa tunaishi katika enzi ya dhahabu, ambapo sisi kama vijana tunapata kuunga mkono sana na uongozi wa kisiasa, ambayo ni kufanya kazi kikamilifu na kwa uthabiti ili kuwawezesha wataalamu kutoka kwetu na kuunga juhudi za vijana katika pande zote, na nyanja zote. "
Anaendelea kauli yake akielezea Shukrani yake ya kushiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na kusifu msaada wa Serikali ya Misri kwa programu na miradi ya kimataifa kama hiyo, yanayochangia upanuzi wa matarajio ya vijana , kuzidisha matarajio yao , na kuboresha ustadi yao kwa mafunzo ya ujuzi na kubadilishana uzoefu nchi na hata mabara mengine.
Ahmed Mukhtar aliongeza akiashiria maneno ya Rais El Sisi "Ndoto haziishi" kama dalili na ushahidi,pia alieleza hotuba yake kwa vijana, akisema: "Shirikini, Badilisheni, fanyeni bidii, Subirini, na endeleeni vizuri, muwe na Ushirikiano zaidi na muwe na ndoto,msikate tamaa, muwe na imani kuwa Ndoto haziishi kulingana na wakati mrefu kama yaliyosemwa na Mheshimiwa Rais katika Jukwaa la Vijana Duniani".
Ikumbukwe kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Toleo lake la pili, ulizinduliwa mnamo Juni 2021, ukiwa na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, pamoja na ushiriki wa vijana viongozi 150 kutoka nchi 53 kutoka mabara matatu, Afrika, Asia, na Amerika ya Kusini, ili kuhamisha uzoefu wa ujenzi wa Misri na maendeleo na uimarishaji wa taasisi za kitaifa, pamoja na kujumuisha viongozi vijana kwenye Jukwaa moja la mazungumzo, kubadilishana muhtasari wa uzoefu wa kitaifa na mawazo, na kujadili masuala muhimu katika nyanja za kimataifa, pamoja na kukuza na kutangaza makada wao safu za mbele, na kuwawezesha katika vituo vya kukata maamuzi,pia unalenga kuunganisha vijana viongozi hao; kujitahidi kufikia Ukamilifu na Maendeleo kati ya nchi za Kusini- Kusini, na kisha kuandaa Raia wa Ulimwengu mzima.