Abdul Rahman Azzam Pasha.. Katibu wa kwanza kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

"Lengo kuu la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ni kuondoa majeshi ya kigeni kutoka nchi za Kiarabu na kukataza kuendelea ukoloni "
Abdul Rahman Azzam Pasha alizaliwa mnamo Machi 8,1893 , katika kijiji cha Shoubak cha magharibi, kilichounganishwa na Kituo cha Al-Ayyat cha Mkoa wa Giza, kutoka kwa familia ya Kiarabu ambayo asili yake ni ya kisiwa cha Arabia, babake Sheikh Hassan Beck Azzam ni mmoja wa wakuu wa Giza na mwenyekiti wa kamati ya sheria ( Baraza la kwanza la kutunga sheria ya kimisri ) na hivyo ni kabla ya kuanzisha maisha ya kisheria nchini Misri. Babu yake, Sheikh Salem Beck Azzam, alikuwa Gavana wa Giza, na alihamishwa wakati wa uvamizi wa Waingereza kwa Sudan, na aliaga Dunia na kuzikwa mjini Khartoum.
Abdul Rahman alipata elimu yake ya kimsingi, akaendelea na masomo yake hadi alipopata stashahada ya sekondari mnamo mwaka 1912, baada ya hapo aliomba kusafiri hadi Uingereza ili kumalizia elimu yake, na akawaomba wazazi aende kusoma huko Chuo cha San Thomas cha Kiingereza na Abdul Rahman hajakuwa na mwelekeo wa matibabu, na umri wake haukuruhusu kwa hilo lakini tayari alisisitiza kusafiri na huko alianza shughuli yake ya kisiasa na kusimamia kamati ya Abu AlHall ya kimisri ( ambayo ilianzishwa na Wanafunzi wamisri). Azzam alisafiri hadi Geneva, huko Uswisi na alikutana na kiongozi wa Chama cha Taifa, Mohamed Farid.
Na huko Geneva wanafunzi wamisri walikutana katika mkutano ulioongozwa na Mohamed Farid, na Azzam alizungumza katika mkutano huo, uliofanyika ili kushughulikia suala la kimisri na uhuru wa Misri, ambapo Azzam alizungumzia maombi ya kuanzisha maisha ya kikatiba nchini Misri.
wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia vilipoanza, alisafiri bila ya utambulisho, na alikuwa na utambulisho mdogo wa uandishi wa habari kutoka gazeti la kawaida la Kiingereza, gazeti la "Daily Citizen." Gazeti hilo halikujulikana nchini Uingereza, jambo litakuwaje akionesha utambulisho huo katika nchi nyingine, na jambo hili lilikuwa limemaanisha kitu fulani, kwani ilikuwa ni dalili ya roho ya Azzam ya ujasiri wa kiasi cha juu , na wakati alipofika katika mji uitwao "Shkodra", alitanabahi mandhari ya uharibifu yaliyotokea mjini wakati wa vita, na mwili wake ulikonda , basi alikuwa na muonekano wa kutia wasiwasi, na huko alipelekwa kwa Mtawala wa Kiingereza, na Mtawala huyo alikuwa mkali, na alipomuuliza kwanini ulikuja hapa ? , Azzam akajibu: kwamba alikuja kwa ajili ya kutekeleza kazi za uandishi wa habari, na bila shaka mtawala hakuamini gazeti ambalo Azzam alilitaja, na mazungumzo yalifanyika baina ya mtawala na Azzam kuhusu lengo la kazi aliyokuja kwa ajili yake , na jinsi gazeti maskini kama hili limekupeleka ili kuripoti matukio makubwa ya aina hii, na baada ya mazungumzo marefu, Mtawala wa Kiingereza alikubali kumsaidia Azzam katika misheni yake inayoazimiwa , lakini kwa sharti kwamba aandike ukurasa wa kukiri inayoandikwa kwa hati yake ya mkononi , akionesha kwamba yeye - yaani mtawala. - alimshauri kuachana na misheni hiyo , lakini hakubali nasaha yake - pia Azzam aliandika kwenye kumbukumbu zake, na baada ya matukio kadha yenye changamoto Azzam alirudi Uingereza mwanzoni mwa 1913 , na akachukua uamuzi madhubuti nao ni kujifunza wakati wa mchana,na kushughulikia katika mambo ya siasa usiku, na alikuwa amerudi mwenye chuki kwa ukoloni na uvamizi wowote wa nchi nyingine yoyote, na mawazo yake yalikuwa yamelenga kufikia malengo mawili ya kwanza ilikuwa imezingatia kuchapisha maelezo ya ukatili uliofanywa na Wabulgaria dhidi ya Waalbania Waislamu, na ya pili ilikuwa ni kutimiza ombi la wazalendo Waalbania ya wawe na nchi huru inayotawaliwa na Amiri Mwislamu.
Mnamo 1915 Abdul Rahman alirudi Misri, kisha akasafiri Libya, na kushiriki katika harakati za kitaifa za Libya dhidi ya uvamizi wa Italia. pia alikuwa mshauri wa kwanza wa Jamhuri ya kwanza ya Libya, na aliendelea kupambana katika safu ya majeshi ya Libya, kupatanisha kati ya viongozi wa Libya, na mpiganaji dhidi ya uvamizi wa Italia.
Azzam alirudi Misri mnamo 1922, na alichaguliwa katika Baraza la kwanza la Wawakilishi la Misri mwaka 1924 baada ya kutangazwa kwa katiba na alikuwa mwanachama mdogo zaidi ya baraza hilo na alichaguliwa kama msaidizi kwa baraza la wawakilishi akarudi kuchaguliwa tena mpaka mwaka 1936.
Na uhusiano wake na kiongozi wa wapingazi wa Libya, Omar Al-Mukhtar, uliendelea, kama anavyothibitisha katika mojawapo ya mahojiano yake na waandishi wa habari.“Azzam” alisema kwamba mkutano wa mwisho kati yake na “Si Omar Al-Mukhtar” “hivyo ndivyo anavyoitamka kwa lahaja ya Libya” ilikuwa mwaka 1923 .. Anasema: “Tulikuwa tumerudi sote, ambao walikaa miongoni mwa wapiganaji katika vita vya upinzani vya Libya dhidi ya jeshi la uvamizi la Italia mnamo mwaka 1922.. Tulirudi Misri baada ya kukubaliana kwamba kuendelea kwa mapigano dhidi ya wavamizi wa Italia ni kujiua, na hayo baada ya uvamizi huo kuenea, na maangamizi yake kwa wapiganaji yaliongezwa , na baada ya vikosi vya jeshi la Italia kuangamiza Libya kwa uwezo wao wote wa Vita dhidi , na ingawa tulitia utaishi na hofu kwa vikosi vya majeshi haya makubwa, ila tuliamua sote kusitisha mapigano, baada ya kupoteza uwezo wa mapambano, na wengi kutoka sisi tukahukumiwa kuuwawa , na mimi nikahukumiwa kwa kifo, kisha hukumu nyingine kwa kifo kutoka kwa Mussolini mwenyewe, na tukarudi Misri kupitia jangwani, na tulikuwa na Walibya karibu na laki moja, na mpango wetu ulikuwa kuanzisha vita vya kisiasa dhidi ya Italia, mpaka hali itakapokuwa sawa ili tuendelee na mapambano, na ndugu zetu wakaenea katika mikoa mingi "Omar Al-Mukhtar" alikuwa miongoni mwao .
Bw.Omar Al-Mukhtar alikuwa akinisubiri pamoja na baadhi ya wanaume, lakini hakusubiri muda mrefu, kwa sababu nilirudi mapema baada ya mjadala mkali katika Baraza la Wawakilishi uliosababisha mgogoro kati yangu na marehemu kiongozi Saad Zaghloul ambaye nilikuwa naheshimu na kumthamini ... Bw. Omar alianza kusema: Bw. Abdul Rahman, niliamua kurudi katika mapambano huko Libya, kwa sababu sikuweza kuishi bila kupigana na Waitaliano ... umri wake ulikuwa unakaribia kufika miaka sabini na ninamhofia hatima ya kweli, na nikajaribu kubadilisha nia yake, lakini alisisitiza,kusema: Niliamua kuuawa kishahidi.Abdul Rahman, niliamua hili, na sitabadilisha maoni yangu , na sitaki zaidi ya kuniunga mkono mpaka nifike ndani ya Libya.
Azzam anakumbuka: “Gharama za maandalizi zilikuwa ndogo, hazizidi paundi 13. Tulikopa na tukanunua ngamia wawili na baadhi ya blanketi na chakula.Silaha hazikuwa tatizo, ambapo wanazipata kutoka kwa adui yao kwa nguvu tena bure.” Azzam anaongeza kusema : “ bwana Omar” alikwenda pamoja na watu watatu kwa ngamia wawili. kabla hajafika , alianza tena kupigana na Waitalia, na kwa kweli sikudhani atabaki hai hata kwa siku chache, kwa sababu ukoloni wa Waitalia ulikuwa maadui wabaya zaidi tuliowajua , lakini bwana Omar aliendelea kupigana kwa muda wa miaka mitano, na alikaa kwa sababu nakuogopa kifo, na kwa hiyo maisha yake iliendelea , na Hili ni somo hai kwa wapiganaji wote waheshimika, licha ya bwana Omar, wakati aliona hatari ya majeshi ya ukoloni inawazingira kila mahali, akanituma kusema: “Atawakusanya wanawake na watoto na wanaume ambao hawawezi kupigana na atawapeleka Misri.
“Azzam” anaongeza kusema “Barua zake alizoniandikia zilikuwa kupitia baadhi ya Waalgeria, hivyo nikatuma onyo la kutozituma kwa njia ya Salloum, kwa sababu mamlaka za Misri zinazuia hilo, na niliogopa kwamba wangezikabidhi kwa mamlaka ya Italia, na Nilimomba kwamba kuingia kwao kupitia kusini mwa Siwa Oasis huko kusini mwa Misri na huko Omar aliteulia vijana na wale wanaoweza kutumia silaha , akawaaga wengine , kisha akarudi kwenye mapambano, lakini baada ya hapo kwa bahati mbaya akaanguka mikononi mwa vikosi vya ukoloni akiwa amejeruhiwa na hajainama kichwa wala hajaomba msamaha na alikumba kifo kwa ujasiri usio wa kifani . "
Azzam aliandika makala kadha ambazo zilielekea upande wa kiarabu na Umoja wa kiarabu, na miongoni mwa aliyoyaandika, utafiti wake wa awali kabisa, aliouandika katika jarida la “Al-Hilal” mnamo Februari 1934, na kichwa chake kilikuwa cha kuvutia “ Dola ya kiarabu , na je, wakati wa kuanzishwa kwake umefika?”, na Azzam alianza utafiti wake kwa kusema: “Wito wa kuanzishwa dola ya Kiarabu labda ni moja ya ndoto , lakini ni miradi mingapi mikubwa na uhalisia mkubwa kabla ya kuwepo kwake ilikuwa ndoto vichwani mwa wanafikra, na fantasia akilini mwao, hadi ndoto na mawazo yalitimia, na kila kitu kimekuwa ukweli katika hali halisi , na dola ilikuwepo zaidi ya mara moja katika zama zilizopita mnamo zama za Bani Umayya, Bani Abbasiyya na wengineo, kwa hivyo si mbali kwamba dola hii itarudi kwa jinsi ilivyokuwa au kwa bora kuliko ilivyokuwa, na si mbali kwamba leo ni ndoto, kisha kesho itakuwa ukweli.
Mnamo 1936 Azzam aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Mwakilishi Mkuu wa Ufalme wa Misri, na Kamisheni hii ilijumuisha nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu, ambazo ni Iraq, Iran, Afghanistan na Saudi Arabia, kisha akahamishwa kwenda kufanya kazi Uturuki na Bulgaria mnamo 1939.
Alichaguliwa kuwa Waziri wa Awqaf mwaka 1939 kisha Waziri wa Masuala ya Kijamii, na wakati wa wizara yake, alichukua jukumu la kuanzisha vikosi vilivyowekwa na kuteuliwa kuwa kiongozi wao, pamoja na kazi yake ya uwaziri na kisha kuwa Waziri wa Mambo ya Nje baada ya hapo.
Na alikuwa na jukumu kubwa katika kuunda jeshi hili lililowekwa, kulingana na masharti ya mkataba wa 1936 Misri iliwekewa vikwazo, haswa katika suala la jeshi, na kutoka hapa Azzam akawa na mawazo ya kijeshi ambayo Uingereza haufahamu kabisa, ambayo ni uanzishaji wa mashirika ya silaha ya asili maarufu ambayo inaweza kuendeleza uwezo wa kijeshi wa Misri, hivyo wazo la jeshi lililowekwa lilikuwa jibu kwa Uingereza kuinyima Misri katika kuanzisha jeshi lenye nguvu. Na alieleza kuwa lengo la kuanzishwa kwa jeshi hilo ni kuandaa idadi kubwa ya watu watakaobeba silaha katika nyakati ngumu.
Balozi Azzam alishiriki katika ujumbe wa Misri kwenye Kongamano la Palestina lililofanyika huko London mwaka 1939, ambapo hadhi yake, historia ,utamaduni na Uarabu vilikuwa vipengele muhimu katika kumwezesha kumfikisha hatua ya mwanzilishi.Inafaa kufahamu kwamba Abdul Rahman Azzam alipigana vita vya kiakili ili kuanzisha nadharia huru ya Kiarabu, ambayo ilifanywa na jarida la Al-Hilal mnamo 1931, ambayo ni kama kura ya maoni juu ya mabadiliko ya wasomi wa Kiarabu wenye mwelekeo wa utaifa na kuzingatia mshikamano wa jumla kati ya Nchi za Kiarabu, na katika kura hii ya maoni, madai mengi yenye nguvu yaliibuka kwa ajili ya kanuni ya mshikamano baina ya nchi za Kiarabu, na huu ulikuwa ni wito wa mapema sana, na ulikuwa ni Muungano wa Pan-Arabism nchini Misri, ambao ulikuwa unaongozwa na Ahmed Zaki Pasha ambaye anaitwa Sheikh wa Uarabuni anayeiongoza na maandishi ya Abdul Rahman Azzam yalikuwa marejeo bora zaidi na uungaji mkono wa uhusiano huo, na Muhammad Ali Alouba Saleh Harb na wengineo walikuwa pamoja naye.
Wazo la Abdul Rahman Azzam lilikuwa kuanzisha Umoja wa Waarabu ambao utajumuisha watu wote wa Kiarabu, pamoja na watu wa Palestina na nchi ya Palestina, na alitoa barua kwa viongozi kadhaa wa nchi za kiarabu haswa wamisri, tena alikuwa wazi kutokana na hotuba yake kwamba kama Misri ingekubali mradi huo, ingefaulu, na Hakika serikali ya wajumbe wa Misri, iliyoongozwa na kiongozi Mustafa al-Nahhas Pasha ilikuwa na shauku, wakati huo alikuwa na wazo la muungano kwa jina la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Azzam alichaguliwa kama mjumbe wa Al Wafd Al Masri na wakati hati ya Umoja wa Mataifa ya Kiarabu ilipoundwa mwaka 1945. na wakati mkataba wa Umoja huo ulipotiwa saini na nchi saba za Kiarabu mnamo Machi 22 ya mwaka huo huo, alichaguliwa kwa kauli moja kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Ligi na akabaki humo hadi 1952.
Katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Azzam hakuwa tu mrasimu, kisiasa au mwanadiplomasia, kama baadhi ya watawala wa Kiarabu walivyotaka kwa sababu aliendelea kuwa mwaminifu kwa kanuni zilizomsukuma kujitolea katika nyanja za jihadi katika Balkans na katika Cyrenaica na Tripoli, ambapo muhimu zaidi ni kanuni mbili: ya kwanza ni kwamba hakutofautisha kati ya kufanya kazi kwa Uarabu na kufanya kazi kwa Uislamu.
Ya pili: Hakutofautisha kazi ya kisiasa na jihadi kwenye nyanja za vita.
Wakati wa kazi yake katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, aliendelea kujiona kuwa ni mujahid, kama alivyokuwa kabla yake, na katika jihadi yake hakutofautisha baina ya Uarabu na Uislamu, wala baina ya medani za vita na uwanja wa siasa.
Watafiti walimwita Arab Guevara haswa baada ya maisha yake kuhusishwa na mapambano ya ulimwengu na akakubali sababu ya uhuru wa Indonesia na wito wake wa uhuru wake na kuliweka suala hilo mbele ya Baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, nayo ilikuwa shirika la kwanza la kimataifa kutambua uhuru wake.
Tena tangu mwanzo wa maisha yake ya kisiasa, alipendezwa na Palestina na sababu yake na akaelezea ukweli wa kadhia ya Palestina kwa walimwengu na matarajio mashuhuri ya Uyahudi.Pia alishiriki katika Mkutano wa Kiislamu huko Jerusalem ambao ni wa kwanza kwake. Ushiriki rasmi wa kujadili masuala ya Palestina na matarajio ya Wayahudi kisha alishiriki katika Mkutano wa Duru ya Mzunguko huko London.
Baada ya kumalizika kwa mamlaka yake kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Azzam aliwahi kuwa mshauri wa Ufalme wa Saudi Arabia na akauwakilisha katika mzozo unaohusiana na nyasi za Burma.
Licha ya udhalimu wa mambo ya siasa na matukio ya vita katika maisha yake alikuwa mwandishi wa vitabu vingi, ana mtindo wa masimulizi unaochukua akili anapoongelea matukio yake katika nchi za Balkan na Libya.
Aliandika kwa Kiingereza kuhusu taswira mpya miongoni mwa picha kadhaa za kihistoria na za hadithi za Sultan Salah Aldin Yusuf ibn Ayyub katika kitabu chake Salah Aldin Alayyubi na Ufufuo wa Mafundisho ya Kisunni.
Na tunaonesha kutoka katika wasifu wa shujaa Salah Aldine Alayyubi hadi Shujaa wa Mashujaa ambacho ni kitabu alichoandika kwa mamlaka ya Mtume Muhammad (S. A. W). Watu wengi ijapokuwa mwandishi wake ni mwanasiasa wa daraja la kwanza, Azzam alishughulika na wasifu wa Muhuri wa Mitume Muhammad (S. A. W) kwa mtazamo wa kimaadili na hekima yake katika kusimamia mambo. Na athari ya wito wa Muhammad kwa mtu binafsi na kundi hivyo akawaeleza watu jambo la ajabu sana linalojulikana kwa wanadamu la wasifu lililo zuri zaidi na la thamani zaidi ambalo historia na siku wanalifahamu katika suala la uumbaji na ukuu.
Utoaji wa kiakili wa AbdulRahman Azzam unaendelea kupitia kitabu cha (Ujumbe wa Milele) ambacho kinachukuliwa kuwa moja ya kazi muhimu zaidi za Abd al-Rahman Azzam. Kilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1365 / 1946, Inachanganya kanuni za kimafundisho ambazo haziwezi kupuuzwa au kubadilishwa katika jamii za Kiislamu na vigezo vya ustaarabu ambavyo lazima vichukuliwe ili kuufanya upya na kuufanya mradi wa Kiislamu kuwa wa kisasa kwa njia inayouwezesha kuongoza ulimwengu na kufikia haki usalama na amani ya kimataifa.
Pia inafichua uasilia wa mawazo ya Abdul Rahman Azzam jambo jipya la mbinu yake ya upatanisho kati ya zamani na mpya, unyoofu wa jihadi yake na mapambano katika kutetea harakati za ukombozi katika ulimwengu wa Kiarabu juhudi zake za kuanzisha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, na wito wake wa kuanzishwa kwa shirika au shirikisho la mataifa ya Kiislamu.
Kwa maoni yake ujumbe wa milele wa Waarabu ni ujumbe wa Kiislamu kwani yeye aliuamini na jinsi alivyopanga hatua zake na kuutetea katika kitabu hiki moja ya misingi ya ujumbe huu ni kwamba haukubali fahari katika mbio au jinsia na kwamba thamani ya mwanadamu katika kazi yake na katika medani ya kazi na jihadi ni kwamba kila mtu anafurahia udugu wa kujitolea muhanga umoja wa hatima na mbio za kufa kishahidi.
Maoni ya mwandishi yameathiri duru za utafiti zinazohusika na mawazo ya Kiislamu katika Mashariki na Magharibi.Ujumbe huu umetafsiriwa katika lugha nyingi na matoleo kadhaa yamechapishwa.
Pamoja na hayo ila Abdul Rahman Azzam alikuwa na mawazo yenye utata na haya yaliibuliwa na mwanafikra wa Kiarabu Sata Al-Husari, ambapo Gazeti la Al Musawer la Kihabari lililofunguliwa mwaka wa 1953, naye Abdul Rahman alizungumzia na akataja kubwa Misri inaweza iwe na ukaribu na watu tofauti na Mwenyezi Mungu aliiweka katikati ya dunia ili iweze kuunga mkono watu wote, na kwamba Misri ni kituo chenye kuendelea cha mionzi ya kimataifa.Tuko hapa Kairo, tukikasirika watu watatukera na tukiridhika watu wa rangi na mawazo yote wataridhika.
Azzam alipokea mapambo ya hali ya juu kutoka kwa serikali za nchi za Kiarabu, Iraq, Syria, Lebnan na Jordan, na pia kutoka kwa serikali za Afghanistan, Iran, Uturuki na Jimbo la Vatican, na kabla ya hapo serikali ya Dola ya Ottoman ilimtunuku Agizo la Majidi la Ottoman na Hilali Al Hadidi.
Abdul Rahman Azzam Pasha alifariki Dunia mnamo Juni 2, 1976 na akazikwa katika Msikiti wa Azzam huko Helwan.
Vyanzo:
Gazeti la Masuala ya Kiarabu.
Tovuti ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Makala ya uandishi wa habari yenye kichwa cha " Siku moja .. Januari 19,1973..Abdul Rahman Azzam no Katibu wa kwanza wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu anakumbuka mahojiano yake ya hivi karibuni pamoja na "Mujahid mkuu wa Libya" Omar Al mukhtar, kwa mwandishi Said Al-Shahat, Al Youm Al Sabe.
Makala ya uandishi wa habari yenye kichwa cha " Abdul Rahman Azzam... Katibu wa kwanza wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Mwanzilishi wa Jeshi la Kimisri"Linalofungamana", na Safi Al maairgi, Akhbar Al Youm.