Kisa cha mpiganaji risasi "Muhammed Mahran" mkombozi mwana wa port Said

Mkombozi MwanaPort Said , Shujaa Mohamed Mahran, alizaliwa mnamo Septemba 6,1938 katika eneo la Waarabu cha mji wa Port Said.
Wakati wa ukoloni wa kiingereza kwa Misri, walinzi wa Kitaifa wameshaundwa huko Port Said ili kukabiliana na ukoloni huo wa kuchukiza na kuutetea mji wa Port Said dhidi ya Waingereza na Shujaa huyo Muhammad Mahran alikuwa miongoni mwa vijana waliojiunga katika kambi ya mafunzo na kuchukua nafasi ya uongozi wa kundi la pili ya kikosi cha kwanza, na alikuwa na umri wa miaka 18 wakati huo.
Mahran na wenzake walipewa jukumu la kutetea Uwanja wa Ndege wa Port Said na eneo la Gemayel magharibi mwa mkoa huo mnamo Novemba 1956, ambapo eneo hilo lilikuwa likilengwa na askari wa Uchokozi wa Tatu ambao walishuka kwa purutangi ili kuingia Port Said. vilevile , adui alikuwa akishmbulia kwa mabomu na nabelm " Poda ya moto " na kushambulia kupitia ndege madaraja na barabara zinazoelekea Port Said na nyinginezo .
Adui aliongeza mashambulizi yake, yaliyo na kifuniko cha anga na mabomu, kisha helikopta ilitua, askari (5) wa Waingereza wenye silaha vyombo visivyo na waya , na hapo juu walilindwa kwa ndege 3 . Kisha helikopta iliruka na aliwaacha askari ardhini mwa Port Said na Wakati huo shujaa Muhammad Mahran na wenzake walikuwa wamo ndani ya shimo ili kufuatilia hali ilivyokuwa na Baada ya muda mfupi helikopta ilirudi tena kuwachukua askari, na wakati huo mmoja wa wenza wa Mahran alitoka shimoni akapigana vikali hadi aliuawa shahidi kwa risasi za adui. Adui aligundua eneo la shimo la mashujaa, kwa hivyo shujaa Muhammad Mahran aliharakisha kurusha mabomu anayo kwa adui pamoja na kupiga risasi zinazofuatana katika pande zote na aliweza kuua askari wa maadui kadhaa na shujaa akaanza kuelekea kutoka shimo moja hadi lingine. ghafla shujaa Muhammed Mahran alipigwa risasi kichwani na akaanguka ardhini akizimia kisha alitekwa nyara .
wakati ilipotangazwa saa sita mchana Novemba 5, 1956, Shujaa Muhammad Mahran alikuwa katika eneo la Al-Gamil, Magharibi kwa Uwanja wa Ndege wa Port Said, akaona kundi la askari wa Uingereza wakikunywa vinywaji na kucheka kwa kejeli, kisha mmoja wao akamsogea shujaa akasema: Nataka kunywa maji
askari akamwambia shujaa Muhammad Mahran: Abd El Nasser hakukuletea maji hapa ili unywe? .
Shujaa Muhammad Mahran alisema: Maji uliyo nayo ni maji ya Misri yaani ni maji ya Wamisri wote.
Askari huyo alimpiga teke shujaa Muhammad Mahran kwa mguu wake, na hapa shujaa alijaribu kumpokonya bunduki kutoka askari, na kweli aliweza kufanya hivyo, isipokuwa askari mwingereza mwengine nyuma ya shujaa huyo alirusha bomu juu ya mguu wa shujaa akakimbia kutokana na hiyo shujaa alijeruhiwa katika miguu yake.
Kesi bandia ilimeshafanywa kwa shujaa, wakamwambia: Chagua kinachokufaa,au ujibu maswali utakayoulizwa, au kuadhibu adhabu ambayo hutadhanishwa? .
Shujaa akawauliza: maswali gani?
Wakasema: Tunataka kujua maelezo juu ya Port Said na Misri yanayohusiana na wapiganaji wa Port Said na wapi maeneo yao , idadi ya vikosi na makundi , na aina gani za silaha mlizo nazo?
Shujaa akajibu, "Sijui chochote."
wakati huo kiongozi wao alisema: Usipojibu na ukaendelea kupinga malipo utakayolipa ni macho yako .
Shujaa Muhammad Mahran alisema: Sijui chochote.
Kabla hawajamng'oa macho yake , Waingereza walimhamisha hadi kwenye mojawapo ya ndege zilizokuwa juu ya jukwaa , kisha ndege ikaruka hadi Uwanja wa Larnaca huko Cyprus. Na Waingereza walimwita (mpiganaji risasi), kwa sababu aliwapiga kwa bunduki yake makumi ya askari waingereza wa anga kwenye pwani mwa Port Said, na alikuwa akiwalenga kichwani na machoni haswa, kwa hivyo walipanga kumng'oa macho yake . halafu Waingereza walisherehekea baada ya kumkamata kwani wakimzingatia, kama viongozi wao walivyosema, " pato lenye thamani."
Muhammad Mahran anasema: Tulipofika Cyprus, walinipelekea gari na kutoka hapo wakanipelekea Hospitali ya Jeshi la Uingereza huko Cyprus, na kule nilidhani kwamba nitapata matibabu yangu kama mfungwa ila nilipofika walinitupia kwenye chumba na watu waingereza wanne walikuwa wamenisubiri na walikuwa kama washenzi Hawana huruma hadi daktari mwingereza alipokuja kuwaamuru wasitishe adhabu na kuniambia: Tutakung'oa macho ikiwa hutajibu maswali, na baadhi ya maswali kuhusu eneo na shughuli ya upinzani katika Port Said, na kwa sababu ya kukataa kwake kwa kujibu, macho yake yameshang'olewa .
Na shujaa Muhammad Mahran anaelezea kuwa Rais Gamal Abd El Nasser alimletea zaidi ya timu moja ya madaktari wahusika kutoka nchi mbalimbali za ulimwenguni (Umoja wa Kisovyeti, Ujerumani Mashariki, Uhispania na Austria) kwa siku na miezi kadhaa kwa ajili ya kunisaidia kupata uwezo wa kuona tena, lakini madaktari wote waliripoti kwamba Waingereza walikuwa wamemng'oa mshipa wa macho mpaka majaribio yoyote ya kuyatibu yalishindwa .. na sababu ya kumkamata bingwa huyo ni kupambana kwa ushujaa na kuwaua kikosi na askari waingereza kadhaa karibuni kwa uwanja wa ndege wa Al-gamel na Baada ya kujeruhiwa, alikamatwa na inatakiwa kutendwa kama mfungwa wa vita , ila mtindo huo wa ukoloni mpya na ya zamani ambao niliuzoea kutoka kwao Wanajifanya wana ustaarabu na ubinadamu, na ndio wako mbali na hilo.
Rais wa Misri Abd El Fatah El-Sisi alimzawadia kwa kumrejesha katika kazi yake katika mambo ya maadili kwenye Makumbusho ya Kijeshi kama tathmini yake baada ya kutengwa, pamoja na kumpa Viza ya kuhiji kwa gharama ya jeshi, kuweka mlinzi anayeandamana naye milele . kwa maisha yote, kumkabidhi zawadi na kuutaja mradi mojawapo ya miradi ya makazi ya hivi karibuni kwa jina lake, kwa Shukrani na uthamani kwa jukumu lake la Kishujaa na la kiukomboaji .
Shujaa mpinzani wa Ukoloni kwa ajili ya Port Saidaliaga Dunia baada ya kuandika jina lake katika historia ya kishujaa kwa "Mji Shujaa" kwa kujitolea, mnamo Mei 10, 2021.