Rawya Attia "Mama wa Mashahidi"

Rawya Attia "Mama wa Mashahidi"

Imetafsiriwa na/ Mariem El-Hosseny
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Rawya Shams Al-Din Attia alizaliwa tarehe Aprili 19 1926, kwenye Mkoa wa Giza, na akakulia katika familia ambayo ina shughuli za kisiasa, kama baba yake ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafd Mkoani mwa Gharbia. 

Rawya alijiunga na Shule ya Sekondari ya Princess Fawzia akiwa na Umri wa miaka kumi, baba yake alifungwa jela kwa sababu ya shughuli zake kali za kisiasa, akiwa na Umri wa miaka kumi na minne, lakini alimwacha msichana aliyeasi, akishiriki katika maandamano ya kupinga Uvamizi wa Uingereza na wakati mmoja alipigwa risasi na kubebwa na Huda Shaarawy mkononi mwake kuponya majeraha yake na hiyo ilikuwa mwaka 1936, mara tu baada ya kusainiwa kwa mkataba wa 1936.

 Rawya alicheza jukumu la kuongoza kati ya wanafunzi wenzake katika Shule ya Sekondari ya Princess Fawzia, na kutoka hapa alianza kuunda Utu wa kisiasa wa "Rawya", akikataa dhuluma na kudai haki za wanawake. Alipata diploma ya shule ya sekondari na kisha kujiunga na Kitivo cha Elimu, Chuo Kikuu cha Kairo, Idara ya Historia, alifanya kazi baada ya kuhitimu Uandishi wa habari kwa miaka sita, na alifundishwa na waandishi wawili wakubwa, marehemu Mustafa na Ali Amin, na baada ya kazi yake katika Uandishi wa habari, alipata diploma kutoka Kitivo cha Elimu mwaka 1947, diploma ya saikolojia mwaka 1949, kisha diploma katika Uandishi wa habari mwaka 1951, na diploma kwenye masomo ya Kiislamu.

Katika kipindi hiki (miaka ya 1990), Chama cha Wanawake wa Misri, kinachoongozwa na Hoda Shaarawy, kilitengeneza kijitabu kilichojumuisha baadhi ya matakwa ya wanawake, muhimu zaidi ni haja ya kurekebisha sheria ya Uchaguzi kwa kuwashirikisha wanawake wenye haki ya kupiga kura, pamoja na kuwapa wanawake haki zote za kisiasa na Uanachama katika mabaraza ya mitaa na bunge kwa msingi sawa na wanaume.

Wakati mapinduzi ya Julai 23, 1952, watu walikombolewa kutoka kwa Udhalimu na kazi, na wanawake walipewa haki zao kamili za kijamii na kisiasa, na katiba ya kwanza ilitolewa nchini Misri mnamo Januari 1956, na ilijumuisha kanuni ya Usawa kati ya wanaume na wanawake kwenye haki za kisiasa, na wanawake walikuwa na haki ya kuteua na kupiga kura, kama Uchaguzi wa kwanza wa bunge kwa wanawake ulifanyika mnamo 1957, na waliingia kwenye Uchaguzi na kura nusu milioni za wanawake kwa mara ya kwanza.

Wanawake kwenye Uchaguzi huu walikabiliwa na makabiliano magumu ambayo lazima yashinde, ikiwa ni pamoja na mila za Mashariki katika jamii ya Misri, bado inayozuia harakati za wanawake kwa kiwango kikubwa katika ngazi ya Umma, hasa katika mazingira ya kisiasa, na bado Uamuzi ulitolewa hivi karibuni nchini Misri kuongeza "kiwango cha bunge" kwa wanawake katika bunge la Misri. Kwa Uamuzi wa Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser, chini ya Katiba ya 1956, mlango wa Uteuzi ulifunguliwa na wanawake 8 waliomba Uteuzi, na bodi ya wahariri ya shirika la kisiasa la mapinduzi ililazimika kuidhinisha Uteuzi huu, na Uteuzi wa Rawya Attia uliidhinishwa, na kuwa mwanamke wa kwanza kuingia katika bunge la Misri.

Mwaka 1956, Rawia alichukua cheo cha nahodha katika kitengo cha makomando wa katika jeshi na kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia cheo cha kijeshi katika jeshi, ambapo alicheza jukumu muhimu katika Vita vya Suez (Uchokozi wa Utatu "Tripartite Aggression") wakati alipowafundisha wanawake  4000 juu ya huduma ya kwanza na Uuguzi, na kupokea askari waliojeruhiwa na maafisa kuponya majeraha yao katika 1967, na Rais Gamal Abdel Nasser alisema juu yake katika mkusanyiko wa wanaume wa vyombo vya habari, aliamini katika mapambano ya wanawake wa Misri kutoka kwa mapambano ya Bi.Rawya Attia.

Tarehe Julai 14, 1957 ilirekodiwa kama tarehe ya kuingia kwa mwanamke wa kwanza wa Misri bungeni baada ya vita vikali, na Rawia alianza safari ya kazi ya kisiasa, akidai haki ya kisiasa ya wanawake ya Uchaguzi.

Rawya Attia aliongoza Chama cha Familia za Mashahidi na Mashujaa wakati wa Vita vya Sita vya Oktoba mwaka 1973, na kwa sababu hii aliitwa "Mama wa Wapiganaji wa Mashahidi", na alikuwa akitembelea askari mbele kila siku, na alipokea Medali ya Jeshi la Tatu kwa Vita vya Oktoba, Ngao ya Jeshi na Ngao ya Jeshi la Tatu, na alichaguliwa kama mama bora kwa mwaka 1967, na pia alipokea Medali ya Wajibu kutoka kwa darasa la kwanza kutoka kwa Rais Anwar Sadat.

Rawya aligombea Ubunge wa wananchi kwenye Uchaguzi wa mwaka 1984 na kufanikiwa kupata tena kiti chake chini ya dome, kuanza majukumu yake ya ubunge maarufu, yaliyoanza kupanuka kwa kuijadili wakati wa vikao, ambapo alishiriki kujadili taarifa ya Waziri wa Masuala ya Jamii kuhusu matatizo ya kifamilia, na kumtaka waziri kutekeleza mradi huo kwa ajili ya Uanzishwaji wa ofisi za mwongozo wa familia na Ushauri wa ndoa kote Jamhuri, na pia alitaka Ushirikiano wa Kamati ya Forodha na Mila ya Wizara na Wizara ya Mwongozo wa Taifa, kuondoa mila na desturi zinazoharibu sifa ya Misri nje ya nchi, na pia kuwasilisha pendekezo la mradi Sheria ya Uzazi wa mpango.

Rawya hakusahau jukumu lake la kibinadamu, ambalo daima lilifanana na jukumu lake la bunge, kwa hivyo alikuwa na jukumu kubwa katika vita vya Iraq na Kuwait, na kusimamia Utoaji wa kozi za ambulensi, Uuguzi na Ulinzi wa raia kwa wanawake wa Kuwait waliotoka Kuwait.

Baada ya kazi yake kubwa katika kutoa, kuinua jina la wanawake wa Misri, haikuwa ajabu kwamba alichaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Taifa la Familia na Idadi ya Watu mnamo 1993, na kushikilia nafasi hiyo hadi kifo chake mnamo Mei 9 1997.

Vyanzo:

Tovuti ya Mkoa wa Giza.

Tovuti ya Gazeti la Dar Al-Hilal.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy