Bustani ya Taifa ya Msitu wa Nyungwe nchini Rwanda , na shughuli muhimu zaidi zinazoweza kufanywa huko
Imefasiriwa na / Zeinab Mekky
Msitu wa Nyungwe ni miongoni mwa misitu mikongwe na mizuri zaidi Barani Afrika, una mandhari nzuri na ya kuvutia, rangi yake ya kijani yenye ukungu baridi wakati wa asubuhi huifanya kufifisha macho na kufanya akili kwenda mbali na uzuri wake.
Msitu wa Nyungwe unapatikana kusini magharibi mwa Rwanda, kwenye mpaka na Burundi.
Uko na nafasi ya eneo la takriban kilomita za mraba 1,019 za msitu wa mvua, mianzi, nyasi na vinamasi.
Bustani ya Msitu Nyungwe ilianzishwa mwaka 1933 na serikali ya kikoloni ya Ubelgiji, Baada ya Rwanda kupata uhuru wake mwaka 1962, hifadhi za misitu nchini humo zilisimamishwa kwa Wizara ya Kilimo, na mwaka 2005 serikali ya Rwanda iliifanya Nyungwe iwe hifadhi rasmi na kuipa hadhi ya kulindwa , kiwango cha juu zaidi cha ulinzi nchini.
Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ilitia saini makubaliano na "African Parks" kuchukua usimamizi wa bustani ya Kitaifa ya Nyungwe kwa miaka 20 ya awali.
Mwonekano wa kuvutia wa Jua katika Msitu wa Nyungwe
Msitu huo una takriban aina kuu 13 za wanyama, ni kundi la wanyama lenye takriban aina 275 za ndege, aina 1068 za mimea, aina 75 za mamalia, aina 32 za amfibia na aina 38 za reptilia, pamoja na vipepeo na hii ndiyo iliyoifanya kuwa ya Kipaumbele kipekee sana, cha uhifadhi Barani Afrika na kuwa hifadhi ya asili.
Bustani hiyo sio tu kwako kuona, lakini unaweza kufanya shughuli nyingi tofauti na za kuvutia ndani yake, pamoja na:
Kutembea kwa miguu: - Na hii katika bustani ya Kitaifa ya Nyungwe, kwa kuwa ni paradiso kwa wapanda kutembekea, Pia kuna njia 13 za kupanda mlima ambazo zinachukua zaidi ya kilomita 130 kutoka sakafu ya msitu, kwa hivyo unaweza kutumia wiki nzuri kutembea njia nyingi na kuchunguza wanyamapori, ndani ya msitu wa zamani wa mvua, ambayo itakushangaza kwa mwonekano wake na maisha ya porini iliyomo, kutia ndani ndege, nyani, mimea, maua, na vipepeo maridadi wanaoruka karibu nawe, pamoja na miti ya zamani.
Pia kuna fursa ya kutembea umbali mfupi, kwani shughuli hii hudumu kutoka saa moja hadi nane, katika fursa nzuri kwa wale ambao hawawezi kutumia shughuli ya kupanda mlima.
Kupanda kwa parachuti: Kufurahia Kupanda kwa parachuti ni sehemu ya ratiba ya safari katika urefu wa mita 50 kutoka ardhini na ni urefu wa ajabu kwa sababu utakuwa na uzoefu wa kipekee, utaona nyani wakitembea kwenye vilele vya miti, ndege wakiruka juu na chini, wewe na mtazamo mzuri wa msitu mkubwa wa Nyungwe
safari za sokwe
Ni shughuli ambayo hufanyikwa asubuhi, takriban saa 11 asubuhi, katika kundi la watu wanane upeo, na sokwe hucheza kwenye miti na pia hunyonyesha, kulisha na kuoana, sokwe wamezoea sana uwepo wa wageni.
Safari za nyanya: Bustani hiyo ina aina zaidi ya 30 za nyani, wakiwemo nyani wa bluu, nyani weusi na mweupe, nyani wenye mkia mwekundu, nyani wa manjano na wengineo. Inajulikana kuwa nyani ni watu wa kuchezea sana, hivyo unaweza kupiga picha za ajabu pamoja nao.
Utazamaji wa ndege
Msitu huo unajulikana kama paradiso ya ndege, kwa kuwa ni nyumbani mwa zaidi ya aina 300 za ndege wenye makazi takriban 29 katika Bonde la Ufa la Albertine. Kwa wapenzi wa ndege, tunakuhakikishia utazamaji bora zaidi wa ndege pamoja na upatikanaji wa waelekezi, waongozi ambao watakusaidia kueleza na kutambua aina mbalimbali za ndege msituni.
Matembezi ya Shamba la Chai cha Jesakura: Ni tofauti na inasisimua kwa kweli, ni shughuli mpya kwa sababu utatembelea shamba la chai cha Jesakura ambacho kipo pembezoni mwa bustani ya Taifa ya Msitu wa Nyungwe, hapa utachanganya ziara ya shamba la chai na shughuli nyinginezo, kama vile kujifunza jinsi ya kupanda chai, kuivuna na kuichakata hadi hatua ya mwisho ili kuwa tayari kunywa, Kwa hivyo unaweza kuifanya jioni.
kukaa katika bustani ya msitu: - Ni shughuli nzuri kwa wapenzi wa kupiga kambi ndani ya hifadhi, hutahisi upweke kwa sababu malazi katika hifadhi hukupa mahitaji na ulinzi wote.
Kuonesha baadhi ya shughuli zinazoweza kufanywa katika bustani ya Taifa ya Msitu wa Nyungwe, tunakuhakikishia uzoefu mzuri kwa kutembelea hifadhi hiyo na kufanya shughuli yoyote kutoka humo.
Vyanzo
_nyungweforest.com
_visitrwanda
_African Parks.org
_Uganda safaristours.com