Mapinduzi ya Julai 23

Mapinduzi ya Julai 23

Imeandikwa na: Basmala Ayman Mohamed 

Inawezekana kuna mapinduzi na matatizo mengi kwenye nchi nyingi kwa sababu ya uovu wa utawala, utofauti wa mitazamo ya watu, au kwa sababu nyingine. Hiyo ni jambo la kawaida kwenye nchi zote, lakini nchi zilizoendelea zinaweza kutatua matatizo hayo bila hasara nyingi na zinahakikisha umoja wa watu, na serikali za nchi hizi zibadilishe mfumo ili serikali ijirekebishe na isidhoofishwe na kukaliwa na wengine. Pia kuna mapinduzi yaliyofanyika nchini Misri mnamo tarehe Julai 23, 1952 na yalikuwa na sababu nyingi, malengo na matokeo.

Mapinduzi ya 23 Julai yalikuwa Mapinduzi ya Kijeshi yaliyoongozwa na maafisa wa kijeshi chini ya uongozi wa Gamal Abdel Nasser. Kulikuwa na sababu nyingi za kuanzisha mapinduzi hayo:

1. Ukoloni wa Uingereza na uingiliaji wa kigeni

Kuendelea kwa ukoloni wa Uingereza nchini Misri na kuingiliwa kwao katika mambo ya ndani kulikuwa chanzo cha mvutano mkubwa, hasa baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati shinikizo maarufu la ukombozi kutoka kwa ukoloni liliongezeka. Hii ilibidi iondolewe ili nguvu zao nchini zisiongezeke na kuikalia milele na wananchi hawakuwa na haki hiyo. 

2- Uovu na utawala mbaya: uovu umeenea ndani ya mfumo wa kifalme na utawala mbaya wa mfalme Farouk Al-Aoul, jambo linalozidisha hasira ya watu na kuwalazimisha maafisa kuzungumza dhidi ya mfumo wa sasa. Mfalme Farouk Al-Aoul hakufuata maoni ya wengi, bali anafuata maoni ya wachache, na hakuna haki.

3- Matatizo ya kiuchumi na kijamii: matatizo ya kiuchumi na kijamii yaliongezeka nchini Misri, na hiyo ilisababisha kuongezeka kwa umaskini na kutoweka kwa haki ya kijamii, jambo ambalo liliwalazimisha watu kubadilisha mfumo.

4- Mapambano ya kitaifa na harakati za kisiasa: harakati za kitaifa na kisiasa zinazoomba uhuru zinaongezeka, na umuhimu wake na athari yake viliongezeka na hivyo kuathiri mivutano ya ndani na kuzidisha shinikizo kwa maafisa juu ya mfumo wa sasa.

Kutokana na sababu hizo, maafisa wa jeshi, Gamal Abdel Nasser na Mohamed Naguib waliongoza mapinduzi ya kijeshi mnamo Julai 23, 1952 ili kumaliza utawala wa kifalme na kuanzisha jamhuri mpya nchini Misri.

Kiongozi wa harakati iliyoitisha mapinduzi alikuwa Mohamed Naguib, aliyechaguliwa na maafisa huru kutokana na umaarufu wake mzuri ndani ya jeshi. Alikuwa kiongozi pekee katika kupanga na aliwahamasisha maafisa wengi wa jeshi kujiunga na maafisa huru, na hivyo alikuwa miongoni mwa sababu za mafanikio ya mapinduzi hayo. Maafisa walikuwa na malengo mengi kutoka mapinduzi hayo, kama vile kumaliza mfumo wa kifalme, kugawa ardhi ya kilimo kati ya watawala na matajiri, kumaliza ukoloni wa Kiingereza kwa sababu ya kuingilia kwao mambo ya ndani, kuanzisha jeshi la kitaifa lenye nguvu, kuanzisha haki ya kijamii, na kuanzisha maisha ya kidemokrasia yenye kufuata maoni ya wengi na malengo ya watu.

Mpango wa kutekeleza:

Maafisa huru walifanya mikutano mingi ili kujadili msimamo kwa uangalifu, mwisho wao ukiwa ni mkutano uliofanywa Julai 22, 1952 ili kupitia mpango wa mwisho wa kutekeleza. Yaliyomo ndani ya mpango yalikuwa sababu ya mafanikio ya mpango huu kwa urahisi wake na kuleta udhibiti kamili juu ya vikosi vya silaha na kuteka utawala wa nchi.

Mwanzo ulikuwa ni kudhibiti vikosi vya silaha juu ya jengo la uongozi wa kijeshi katika eneo la daraja la Alquba na kulivamia kwa kundi la Maafisa Huru, huku kundi lingine likiwakamata baadhi ya wakuu wa nchi kutoka nyumba zao ili kuhakikisha kutokuwepo kwa vikosi vya kijeshi dhidi ya mapinduzi. Kisha walidhibiti kikosi cha serikali ya kitaifa na kupeleka vikosi barabarani ili kudhibiti baadhi ya maeneo muhimu ya kitaifa.

Watu walionesha haraka ukubali wao kwa jeshi na walitoka kwa wingi kutangaza msaada wao kwa kundi hilo la kitaifa la maafisa huru. Ukubali huu ulikuwa muhimu kwa viongozi wa harakati ili kuendelea. Kwa hiyo, Mapinduzi ya Julai yalipata urasmi wake kutoka kwa watu baada ya watu kuyakubali, na yalionesha matarajio ya watu ya kupata uhuru.

Kuna mafanikio mengi na matokeo mazuri yaliyosababishwa na mapinduzi hayo, kama:

Athari ya kwanza ya mapinduzi ni kwamba Wamisri waliweza kuchukua haki yao rasmi katika kuchagua watawala wao, na kiongozi Mohamed Naguib alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri, na Gamal Abdel Nasser alichaguliwa kuwa Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Ndani.

Mnamo tarehe Juni 18, 1953, kituo cha uongozi wa mapinduzi kilitoa uamuzi wa kumaliza mfumo wa kifalme na kutangaza Jamhuri.

Mapinduzi yalilazimisha mfalme kuacha utawala na kuondoka Misri na kwenda Italia, na kusababisha kumalizika kwa mfumo wa kifalme na kuanzishwa kwa mfumo wa jamhuri. Ndani ya nchi, mapinduzi ya Julai yalileta miradi mikubwa na mafanikio ya kitaifa kama kuongeza eneo la kulima kupitia kuimarisha na kutunza miundombinu ya kilimo. Pia yalichangia maendeleo ya viwanda, yaliyokuwa njia ya kufanikisha maendeleo.

Mapinduzi yalileta maendeleo katika huduma za kijamii, afya, na kitamaduni kwa watu wa mashambani na kujenga vituo vingi mashambani. Aidha, Mapinduzi yalipatia elimu kipaumbele, na kuanzisha mfumo wa elimu bure ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa watu wote. Kujenga Bwawa la Juu ni mojawapo ya mafanikio muhimu zaidi ya Mapinduzi ya Julai 23, kwani lilisaidia kudhibiti mtiririko wa maji na kupunguza athari za mafuriko.