Kampuni ya Viwanda vya Kemikali ya kimisri Kima... Ni Kiini cha mji wa Misri wa Viwanda vya Kemikali na Mbolea

 Imefasiriwa na / Esraa ElSaid Abdel Hamid

Karibu na mradi mkubwa zaidi wa uhandisi wa karne ya 20 (Bwawa la Juu) na kutumia nguvu za umeme zinazozalishwa kutoka kwake, na mtaji wa paundi milioni 16 uligawanywa zaidi ya hisa milioni nane, thamani ya hisa moja  ni paundi 2 za Misri,Viwanda vya Kima na mahali pake maalum vilianzishwa kwenye eneo la ekari 946 kusini-mashariki kutoka mji wa Aswan, karibu kilomita nne, kwa amri ya Rais Gamal Abdel Nasser mnamo Machi 22,1956 , kwa lengo la kutengeneza Kemikali na Mbolea.

Na uzalishaji halisi kwa kiwanda cha Kima ulianza mnamo Mei 1960 , kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea za nitrojeni na nitrati ya amonia, na Kiwanda hicho kinajumuisha sehemu kadhaa za uzalishaji nazo ni kama:

Sehemu ya uzalishaji wa hidrojeni, ambayo hutoa takriban mita za ujazo 37,000 /saa na elektroniki ya maji.

Sehemu ya uzalishaji wa nitrojeni ambayo hutoa takribani mita za ujazo 13,000/ saa kwa kutoa hewa .

Sehemu ya uzalishaji wa amonia hutoa tani 400 / siku ya mchanganyiko wa nitrojeni na hidrojeni.

Sehemu ya uzalishaji wa asidi ya nitriki hutoa takriban tani 1,422 kwa siku, kwa kiwango cha 53%, kwa kuchoma nusu ya amonia inayozalishwa na hewa na kisha kuifuta ndani ya maji.

Sehemu za Uzalishaji wa Mbolea inazalisha takriban tani 665 za mbolea 33.5% ya nitrojeni + tani 30 za nitrati ya ammoniamu 34.8% ya nitrojeni ya chini na ya juu kwa siku.

Sehemu ya ufungaji (kwa ajili ya kufunga mbolea na nitrati), na sehemu ya baridi na vifaa (vifaa vya baridi na maji katika mzunguko uliofungwa ili kurekebisha matumizi ya maji).

Sehemu za umeme.

Sehemu ya majipu.

Mbali  na maabara kuu, maduka, warsha, mafunzo na kompyuta, warsha za vifaa vya usahihi, maduka ya mbolea na nitrate, huduma za kijamii, zahanati ya matibabu, machimbo ya Kom Ombo, na bandari ya Mto. 

Na mji wa makazi unaojumuisha nyumba za mitindo mingi, msikiti, ushirika wa watumiaji, kilabu na bwawa la kuogelea, ukumbi wa harusi, mkate, shule ya msingi, shule ya maandalizi, shule ya sekondari, kitalu, . Chama cha Ushirika wa Nyumba.

Tena Kiwanda cha Kima kinasafirisha  bidhaa zake kuelekea nchi zipatazo ishirini Duniani kote kati ya Amerika Kusini, Ulaya, Asia na Afrika, kama vile nitrati ya ammonium nitrate ya kiwango cha chini, aloi ya ferrosilicon, mbolea ya ammoniamu ya nitrati ya kioevu,Mbolea ya ammonium nitrate ya punjepunje, mbolea ya Nitrochema Fort yenye microelements , mafusho ya silikaGesi ya nitrojeni ya hali ya juu,, oksijeni Gesi, amonia ya kioevu, maji ya amonia, asidi ya nitriki, asidi hidrokloriki, vumbi la silika, nitrojeni.