Kampuni ya Al-Nasr ya Utengenezaji na kupakia Samaki

Kampuni ya Al-Nasr ya Utengenezaji na kupakia Samaki
Kampuni ya Al-Nasr ya Utengenezaji na kupakia Samaki
Kampuni ya Al-Nasr ya Utengenezaji na kupakia Samaki
Kampuni ya Al-Nasr ya Utengenezaji na kupakia Samaki
Kampuni ya Al-Nasr ya Utengenezaji na kupakia Samaki

Hadithi hii ilianzia miaka ya hamsini ya karne iliyopita,pamoja na kushikilia madaraka ya Misri kwa  Marehemu Kiongozi Rais "Gamal Abdel Nasser" baada ya mapinduzi ya Julai 23,1952. ambapo wazo la kuanzisha makampuni ya kitaifa, ambayo yanamilikiwa na kuendeshwa kikamilifu na serikali ni jambo kuu mnamo wakati huo, Sekta ya chakula na vinywaji ilikuwa na umuhimu mkubwa, kwa hivyo Uamuzi ulitolewa kwa kuanzisha Kampuni ya Edfina ya vyakula vilivyohifadhiwa mnamo Mei 1956 , na Kiwanda cha Edfina Damietta kilijengwa mnamo 1960,kama kiwanda cha kwanza cha kampuni hiyo katika mji wa" Ezbet El-Borg " wa Mkoa wa Damietta, kwa kuwa inamiliki theluthi mbili ya ukubwa wa meli ya wavuvi wa Misri,  kwa ajili ya upatikanaji wa samaki waliovuliwa kutoka maji ya Mediterania na Bahari nyekundu, ili kuwatayarisha na kuwapakia ,na iliitwa Kampuni ya Al-Nasr ya utengenezaji na kupakia samaki, ina ukubwa wa mita za mraba 11,000, ambapo kiwanda cha bati kinajengwa, na kiwanda kingine cha barafu, na kuchakata tena taka za samaki, na kuchimba mafuta ya samaki na kuzalisha unga wa samaki na chakula cha mifugo. 

Mwanzoni,takriban wafanyakazi 1,800 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho kupitia misogeo mitatu. Na kinategemea zaidi samaki wa tuna (Albacore) na dagaa, na kinajumuisha jokofu saba za kuhifadhi bidhaa za chakula, kwa kiwango cha tani 500 kwa kila jokofu, na Matengenezo yake yanategemea kuwepo kwa vyombo vya baridi vinavyogharimu Paundi milioni moja kwa kila chombo cha baridi. 

Kiwanda cha" Edfina Damietta" kilipata umaarufu mkubwa ndani na nje, kwa ubora wake katika utayarishaji  wa samaki aina ya tuna, pamoja na uzalishaji na kufunga  maharagwe , pamoja na kuhifadhi na kufunika mboga. Uzalishaji wa kiwanda hicho ulikuwa takriban tani nne kwa siku, na  husafirishwa kwa nchi nyingi za Kiarabu na kizungu, zikiwemo Marekani, Italia na Canada, pamoja na Libya, Saudi Arabia, Emirates, Sudan na Syria.