Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Vijana huko Guinea Conakry asifu  Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana katika kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake 

Katika muktadha wa sherehe ya kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana,na iliyoambatana na sherehe za watu huru Kuadhimisha miaka sabini ya Mapinduzi matukufu ya Julai, iliyokuwa ni uzinduzi wa kwanza wa harakati za ukombozi wa Afrika, na nchi za ulimwengu wa tatu, sifa za dhati za Mkuu wa Baraza la Taifa la Vijana huko Guinea Conakry,"Mamadou Barry", zilitokea kando ya kongamano la kwanza la kila mwaka la mashauriano kwa viongozi wa vijana wa Afrika, lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Afrika, katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, Julai 2022.

Mkuu wa Baraza la Taifa la Vijana,Mamadou Barry,  alisema kuwa harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana ni mojawapo ya mifumo muhimu ya kufufua kanuni za ushirikiano na mshikamano wa kiutu Duniani, na haswa Barani Afrika zile zilizoungwa mkono na waasisi wa Umoja wa Afrika, akionesha msaada wake, shukrani na imani katika juhudi za Harakati ya  Nasser kwa Vijana katika kutumia ujuzi na nguvu za vijana, kusaidia uwezeshaji wao na kuimarisha ushiriki wao katika vituo vya maamuzi, pia alitathmini jukumu la kimaendeleo la Harakati ya Nasser kwenye Jumuiya za Kiafrika za mbali na maskini zaidi kupitia mijadala jumuishi na kufanya kazi ili kuboresha ujuzi wa rasilimali watu waafrika, kupitia vyombo vya habari vingi vya teknolojia.

Barry aliendelea akisisitiza kuwa Harakati hiyo ya Nasser inaweza kuunda Raia wa ulimwengu mzima, na mwenye ushawishi kupitia uanzishaji wake wa masharti ya Mkataba wa Vijana wa Afrika na Mwenendo wa Umoja wa Afrika kwa Uwekezaji kwa Vijana, kama marejeleo ya msingi, ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, akiongeza kuwa inazingatiwa kama moja ya njia za kuanzisha ajenda za maendeleo, mikataba ya kikanda na kimataifa katika ngazi ya chini, kama vile (Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika) na Mkakati wa Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa (Kusini - Kusini).

Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana,"Ghazaly", alithibitisha kuwa harakati hiyo lilizinduliwa Julai 2019, Barani Afrika, katika nchi zipatazo 23 na kisha kupanuliwa katika miaka minne iliyopita na kufikia takriban nchi 65 ulimwenguni,kwa hivyo, kufikia ushawishi na kuenea katika mabara matano ya Asia, Afrika, Ulaya, Amerika ya Kusini na Australia, ili kuimarisha mahusiano ya kihistoria na kuunga mkono uhusiano wa pande mbili kati ya Misri na nchi zingine za kidugu na kirafiki,na uimarishaji wa kanuni za ushirikiano wa Kusini-Kusini, kama jukwaa la vijana kwa viongozi wenye ushawishi mkubwa zaidi ulimwenguni ili kuzidisha kanuni za Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na mshikamano wa Afro-Asia.

Ghazaly alihitimisha, akibainisha undani wa mahusiano ya pande mbili na viunganishi vya kihistoria kati ya Misri na Jamhuri ya Guinea Conakry, akiashiria misimamo ya pamoja ya kihistoria iliyochukuliwa na viongozi wa nchi hizo mbili kuhusu masuala ya bara hilo, iliyotukuza muungano wa watu wawili, alieleza kuwa Marehemu Kiongozi "Ahmed Sekou Toure" na Marehemu Kiongozi wa Misri "Gamal Abdel Nasser" walikuwa na mahusiano mazuri, moja ya dalili zake ni kwamba Rais Abdel Nasser alimpa yule wa kwanza"Mkufu wa Nile" wakati wa ziara yake nchini Misri mnamo 1961, na kama tathmini ya jukumu na mapambano yake dhidi ya mkoloni Barani Afrika, kwa upande mwingine, chuo kikuu kikubwa zaidi cha Guinea Conakry kiliitwa (Chuo Kikuu cha Gamal Abdel Nasser) kama Tathmini ya jukumu la kila wakati la Kiongozi wa Misri.