Baraza Kuu la Utamaduni lapokea wana wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika

Baraza Kuu la Utamaduni lapokea wana wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika
Baraza Kuu la Utamaduni lapokea wana wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika
Baraza Kuu la Utamaduni lapokea wana wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika
Baraza Kuu la Utamaduni lapokea wana wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika

Vijana waafrika wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi walikutana na Dkt. Hisham Azmy, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Utamaduni, na Dkt. Amany Al-Taweel, Mkurugenzi wa Programu ya Afrika katika Kituo cha Al-Ahram cha Mafunzo ya Siasa na Mikakati, kama sehemu ya shughuli za siku ya kumi ya "Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika".

Dkt. Amany Al-Taweel alisifu jukumu la Ofisi ya Afrika kwenye Wizara ya Vijana na Michezo inayoongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy na juhudi zake katika kuimarisha mawasiliano kati ya vijana wa Bara la Afrika ili kubadilishana Tamaduni, Uzoefu na Mitazamo kati ya Vijana Waafrika kuhusu masuala na mada zinazohusu nchi zao za Afrika, akisisitiza kuwa Bara la Afrika ni Mahali pamoja pasipogawanyika, haswa wanawe walijitahidi sana kuunda Taasisi moja kwa bara la Afrika.

Al-Taweel alielezea dhana ya mawazo ya kiafrika yanayokabili Ukoloni na Utumwa Barani Afrika kutokana na nchi za Magharibi, akionesha kuwa mawazo hayo yalitolewa kwa ufafanuzi katika mikutano mitano kati ya London na Paris pia Waafrika nje ya nchi, yote yaliyolenga haja ya watu wa Afrika ya kufahamiana, na hiyo ndiyo ni jukwaa ambalo viongozi wa Ukombozi walitegemea Barani Afrika.

Al-Taweel alisisitiza kuwa Uhuru wa kitaifa wa nchi za kiafrika unakabiliwa na changamoto zile zile zinazoikabili Afrika mnamo enzi tofauti, akibainisha mapungufu ya nchi za Afrika kati yao katika ngazi ya kiuchumi, licha ya kuwa na mali nyingi na nguvu za kibinadamu.

Huko Al-Taweel aliashiria umuhimu wa kuangalia maslahi ya bara la Afrika na Vijana wake ili kujenga mustakabali wake na ufufuo wake kati ya Mataifa, akisisitiza haja ya Ushirikiano wa Afrika-Afrika katika nyanja zote.

Al-Taweel pia aligusia sera ya Misri kuhusu bara la Afrika, akisisitiza nia ya uongozi wa kisiasa wa Misri katika kuwakusanya watu wa bara la Afrika, ikiamini jukumu la nchi za Afrika katika kujenga mustakbali na kukabiliana na changamoto zinazolikabili bara la Afrika.

Kwa upande wake, Dkt. Hisham Azmy alieleza jukumu la Baraza Kuu la Utamaduni katika kuongeza mawasiliano ya kiutamaduni na Afrika na kuimarisha uhusiano kati ya Misri na nchi zote za Afrika, kwa kuzingatia Utambulisho wa Misri wa Afrika.

Azmy alieleza mchango wa Kiongozi Marehemu Gamal Abd El Nasser katika Ukombozi wa Bara la Afrika na Harakati ya Nchi zisizofungamana kwa upande wowote za Afrika, Kiarabu na Kiislamu na akibainisha kuwa sera ya Misri inaonesha wazi uungaji mkono kamili wa harakati za ukombozi Barani Afrika, akifafanua juhudi kubwa zaidi za Misri katika uwanja huo pamoja na kueleza jukumu la kikanda ya Misri wakati wa enzi ya Marehemu Rais Gamal Abd El Nasser, ambaye mwelekeo wa kiutamaduni wa Misri Barani Afrika uliongezeka naye.

Azmy alisisitiza kuwa hivi karibuni  Bara la Afrika  linatazamia kwa matumaini ya maoni na msisitizo wa Rais Abd El Fatah El-Sisi ya kulivuka Bara la Afrika hadi katika enzi za mwamko na maendeleo wakati wa Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo ulishughulikia kuwatambulisha washiriki katika Baraza Kuu la Utamaduni na kufafanua matukio muhimu zaidi ya kiutamaduni kuhusiana na upande wa Afrika, pamoja na kusisitiza juhudi za Baraza katika uungaji mkono wa Mshikamano wa Utamaduni wa Afrika, ukigusia matukio muhimu zaidi yaliyoandaliwa na Baraza hilo mnamo kipindi kijacho, yanayohusu Bara la Afrika.