"Ahmed Bin bella " ..... Ambaye ni mafuta ya mapinduzi ya Ukombozi

"Ahmed Bin bella " ..... Ambaye ni mafuta ya mapinduzi ya Ukombozi



Kauli yake inayohusu Misri: amesema" natamani kuzungumzia pamoja na yeyote anayekutana nami ili kumweleza kisa cha mchango wa Misri katika mapinduzi ya Algeria, basi kwamba, Misri imo moyoni mwangu na Abd Elnaser yumo moyoni mwangu, na bila ya Misri Mapinduzi ya Algeria hayatakuwepo, na mapinduzi mengine pia, Misri ilikuwa kila kitu, siku ninapokuja Misri na sikuwa na chochote, nilisimama mbele ya bakuli ya maharage nayo ilinilisha, nasi tulichukua silaha, vyakula, na pesa ili kukomboa nchi zetu, natamani kukamilisha Masiku yangu hapa katika nchi hii, haki ya Mwenyezi Mungu, haya ni matumaini naomba Mwenyezi Mungu ayahakikishe.

Bwana Bin Bella ameulizwa kuhusu Abd Elnaser, amesema " Mimi ni mwaminifu mkubwa kwa Mawazo ya Abd Elnaser, namzingatia kama mtu adhimu, amechangia kusisitiza Mapinduzi ya Algeria zaidi ya yeyote, naye alikuwa alama ya Uaminifu wa mapinduzi ya Algeria mnamo awamu zake tofauti, na waigeria wana deni kwa mtu huyu.

Bin Bella Plu alimwambia bwana Ahmed Said "mtangazaji mmisri maarufu na rais wa idhaa ya sauti ya waarabu aliyepita " kwamba, kakangu Said, Abd Elnaser ni alama muhimu katika eneo, bila ya Misri hayatakuwepo Mapinduzi ya Algeria, bila ya Nasser haitakuwepo misaada kwa mapinduzi. Natamani kuhitimisha maisha yangu nchini Misri.

Ahmed Bin Bella, anazingatiwa kiongozi mmoja muhimu katika historia ya Algeria, basi kwamba yeye aliyepambana ili kukomboa Algeria toka Ufaransa, naye alikuwa rais wa kwanza kwa Algeria baada ya Ukombozi.

Ahmed Bin Bella alizaliwa katika mji wa Maghania wa Algeria, tarehe ya 25 mwezi wa 12 mwaka wa 1916, familia yake ilikuwa ndogo sana yenye mizizi ya kimagharibi, na alijiunga shule ya kifaransa nchini Algeria, na alilazimishwa kujiunga jeshi la kifaransa mnamo kipindi cha ( toka1937 hadi 1940), na alishiriki katika vitu vikuu vya pili vya kimataifa kwa cheo cha afisa wa kijeshi la kifaransa, na baadaye kumaliza vita, alibeba bendera ya Ukombozi dhidi ya Ukoloni wa kifaransa.

Alianza njia ya mapambano ya kitaifa na ametawala tawala za taasisi khasa (toka 1947 hadi 1950). Nayo inazingatiwa kama ubawa unaofanana na kiaskari, kwa chama cha nchi ya Algeria, uliobeba nembo ya "Hakuna Ushirikiano ", " Hakuna Utenganisho", bali Ukombozi, na taasisi hiyo ilihusiana na kupanga maandamano dhidi ya Ukoloni wa kifaransa, hata ilikuwa kama Ala ya kijeshi linalosababisha mapinduzi yenye silaha, ingawa ilikuwa harakati yenye siri lakini, ilijulisha katika "Machi 1950", na wanachama wake walifukuzwa, walikamatwa gerezani mpaka ilimalizisha mwishoni.

Yeye alikamatwa mwaka wa 1950, lakini yeye aliweza kukimbia baada ya miaka miwili gerezani, alielekea Kairo, ambapo Misri, Abd Elnaser walimkumbatia, na bwana Ahmed Said " ambaye alikuwa rais wa kwanza wa idhaa ya sauti ya waarabu " alimpokea na alimfikisha kwa afisa wa upelelezi mmisri ili kuanza safari ya mapinduzi ya kweli, kutokana na mji mkuu wa Misri, Kairo, basi Misri ilimpa Bin Plu njia zote za msaada wa kifedha, kijeshi, kisiasa, na kupitia vyombo vya habari; ili kuunga mkono suala la kialgeria, na hayo yote kupitia siasa ya Misri inayoungana na Uhuru wa nchi za kiarabu na kiafrika zinazokuwepo chini ya Utawala wa Ukoloni, na kwa kweli Bin Plu ameanza kupanga mapinduzi kwa ajili ya; Ukombozi wa kitaifa na mrengo wake wa kijeshi ( jeshi la Ukombozi wa kitaifa).

katika mwezi wa Novemba, mwaka wa 1954 cheche ya kwanza ya mapinduzi ilianza, na kauli ya kwanza kwa mapinduzi ilitolewa na bwana Ahmed Bin Plu, kupitia idhaa ya sauti ya Waarabu katika Kairo - ambayo imeweka Programu nyingi sana kwa ajili ya kunusuru suala la kialgeria -
Kwa hivyo, bwana Bin Bella aliieleza kwamba" sauti ya waarabu ni sauti ya Mapinduzi ya kialgeria", basi harakati ya kupambana kwa silaha kutokana na Waandamanaji dhidi ya Ukoloni wa kifaransa iliendelea, na majadiliano kati ya chanzo cha ukombozi na serikali ya Kifaransa yalianza mwaka wa 1956, na katika tarehe ya 20 mwezi wa Oktoba, mwaka wa 1956, Bin Plu alikuwa akielekea Tunisia kwenye ndege Morocco, na jeshi la kifaransa liliteka nyara ndege ile, jambo linaloeleza mchakato wa kwanza wa uharamia wa kianga katika historia, uliosababisha kukamatwa kwa Bin Plu pamoja na viongozi wa mapinduzi ya kialgeria.

Naye aliachiwa baada ya kutia saini mikataba ya IVAN pamoja na Ufaransa mwaka wa 1962, na kupata Uhuru kwa Algeria, tarehe ya 5 mwezi wa Juli mwaka wa 1962, baada ya Mapinduzi ya Shahidi milioni , yaliyoendelea kwa miaka minane ili kumaliza Ukoloni ulioendelea kwa miaka Mia moja na thalathini na mbili 132.

Ahmed Bin Bella alitawala cheo cha Urais wa kwanza kwa Algeria baada ya Ukombozi katika tarehe ya 15 mwezi wa Oktoba mwaka wa 1963, naye alitamani kujenga taifa lenye nguvu linalofuatia yanayohusu mataifa ya kiarabu, lakini katika tarehe ya 19, mwezi wa Juni, mwaka wa 1965, waziri wa Ulinzi wa Algeria Bwana Alhawari Bumedin, alipinga Bin Plu na amejiweka nafsi yake rais, amekamata Bin Plu kwa miaka 14.na baada ya kifo chake 1978, yeye aliachiwa tarehe ya 30 mwezi wa Oktoba mwaka wa 1980, na alielekea Uswisi na Ufaransa kwa miaka kumi "10", na alirudi Algeria mwaka wa 1990 ili kufanya kazi yake ya kisiasa tena, ambapo aliongoza chama cha " Harakati kwa ajili ya Demokrasia nchini Algeria " nacho ni chama cha Upinzani alikiunda mwaka wa 1984, mnamo kuwepo kwake katika Uhamisho, lakini chama kilishindwa katika Uchaguzi wa Bunge 1991, na tawala za Algeria zilikivunja katika 1997.

Bin Bella aliishi kama mwanaharakati na alijitoa maisha yake kwa kuhudumu nchi yake ndani na nje, na aliunga mkono kwa nguvu masuala ya Ukombozi wa kitaifa, na alisisitiza suala la kipalestina, na alikuwa mwananchi, mwarabu, mpenzi wa Afrika, aliendelea kama hivyo mpaka kifo chake tarehe ya 11 mwezi wa Aprili mwaka wa 2012, akiacha nyuma yake historia yenye mafanikio iliyoendelea kwa miaka 96.

Haki ya Mwenyezi Mungu hatutapata mwanamume kama Gamal Abd Elnaser, hili lililosemwa na Bin Plu kuhusu Abd Elnaser.