Taasisi ya Mafunzo ya Diplomasia kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri yafungua kozi ya kujenga uwezo wa wanadiplomasia wa Afrika wanaozungumza Kifaransa

Taasisi ya Mafunzo ya Diplomasia kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri yafungua kozi ya kujenga uwezo wa wanadiplomasia wa Afrika wanaozungumza Kifaransa

Imetafsiriwa na: Noran Ahmed Mohammad 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia, kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Misri, inafanya kozi ya mafunzo ya wiki mbili Januari hii, ambapo wanadiplomasia 23 na maafisa waandamizi kutoka nchi 11 za Afrika watashiriki: Mauritania, Togo, Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Komori, Chad, Mali, Gabon, Burkina Faso na Kameruni.
Hii inakuja katika muktadha wa nia ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ya kubadilishana uzoefu na nchi za kindugu za Afrika na makada wao wa kidiplomasia katika uwanja wa kuendeleza ujuzi wa kidiplomasia, mazungumzo na usimamizi wa mgogoro, pamoja na kuanzisha masuala muhimu zaidi ya kipaumbele kwa bara la Afrika kwenye uwanja wa kimataifa.