Ubelgiji Yaahidi Euro Milioni 25 ili Kuimarisha Elimu Tanzania

Ubelgiji Yaahidi Euro Milioni 25 ili Kuimarisha Elimu Tanzania

Imetafsiriwa na: Abdel Rahaman Mohamed 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Koinrad Guikkenent, Mwakilishi wa Nchi wa Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABE), alitangaza ahadi ya serikali ya Ubelgiji ya kuipatia Tanzania Euro milioni 25 kutekeleza mpango mpya wa maendeleo ya elimu wa miaka mitano katika mkoa wa Kijuma.

Jochenin, alipozungumza na Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, alieleza kuwa programu hiyo, itakayotekelezwa kwa kipindi cha 2023 - 2027, itajikita katika kuendeleza sekta ya elimu kwa kuboresha ujuzi wa ajira na mafunzo ya ufundi kwa vijana kwa lengo la kuunda fursa za ajira. Pamoja na kukuza usawa wa kijinsia kwa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake, Tutuba alisisitiza kuwa mpango huo utakuwa na matokeo chanya kwa maisha ya Watanzania kwa kuchangia maendeleo na kuongeza: "Mpango huu utashughulikia vipaumbele mahususi katika mpango wa tatu wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano (2021/22 - 2025/26), unaolenga kuboresha huduma za kijamii, maisha ya wananchi na elimu."

Tutuba alipendekeza serikali ya Ubelgiji kuzingatia wazo la kuongeza sekta nyingine muhimu ili kuboresha maisha ya watu, kama vile huduma za afya na maji, kwa sababu wanawake ndio walengwa wakuu na ndio walioathirika zaidi na uhaba wa maji.

Tutuba pia aliiomba serikali ya Ubelgiji kuanzisha mpango kama huo katika visiwa vya Zanzibar ili wananchi wa visiwa vya India vyenye uhuru wa nusu wafaidike na matokeo chanya ya mahusiano kati ya Tanzania na Ubelgiji.

Ziara hiyo kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Gestas Nyamanga, ni matokeo chanya ya ziara ya kikazi ya Rais Samia Suluhu nchini Ubelgiji mnamo tarehe Februari 2022, ambapo ilikubaliwa kubuni mbinu za kujadili utengenezaji wa programu na kuhakikisha mchakato huo unakamilika kwa ratiba.