Tunaadhimisha siku hii maarufu sana katika historia kwa wakati wa Ukombozi wa Kiarabu

Tunaadhimisha siku hii maarufu sana katika historia kwa wakati wa Ukombozi wa Kiarabu

Imefasiriwa na / Raeed Dahy Mohamed

Enyi Wananchi: 

Katika siku hizi za milele katika historia ya Waarabu, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwani  zama za utawala wa kigeni zimeisha kabisa; Zama za ukoloni, zama za udhibiti na zama za wavamizi zimeishia kabisa kwa mujibu wa azma ya watu waarabu katika Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu.

Leo, tunapoadhimisha kuanzishwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, kila mmoja wetu anahisi kwamba Jamhuri hiyo mpya inawakilisha utashi wetu; matakwa ya kila mmoja wenu, akiwa pale kaskazini huko Syria au kusini huko Misri, si utashi wa mkoloni, wala si mapenzi ya mnyang'anyi, wala ya mvamizi, wala si mapenzi ya wale wanaotaka kufanya hivyo na kutudhibiti .. Utashi wa watu halisi wa Kiarabu
Leo – ndugu zangu – kila mmoja wetu na kila mtu katika ulimwengu wa Kiarabu na katika taifa la Kiarabu ana haki ya kujisikia fahari kweli; Kwani kabla ya hapo mwaka wa 17 waligawanya ulimwengu wa Kiarabu. waligawanya kwa penseli kwenye ramani katika nchi na majimbo ili waweze kutudhibiti, walituwekea masharti na kukubaliana na Wayahudi mnamo mwaka wa 17 kuwapa Palestina. Ila Leo sisi ndio tunaoamua, hakuna mgeni anayeamua..

Leo ndugu zangu.. Leo ndugu zangu.. Utashi wetu ni sisi tu - sisi Waarabu – ndio wenye ukuu, ndio wenye madaraka, ndio wenye maamuzi, ndio wenye mamlaka, walioamua kuanzishwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu.

 Leo – ndugu zangu – tunapoadhimisha siku hii maarufu zaidi katika historia; Alfajiri ya ukombozi wa Waarabu, mapambazuko ya kuondokana na utawala wa kigeni, na tunaposherehekea siku hii, tunaangalia zamani na majaribio ya kigeni ya kutudhibiti, na maneno waliyokuwa wakisema: kwamba kuna kasoro wanataka kujaza eneo hili, na kwamba eneo hili lazima lijumuishwe na kukidhi.

Leo, tunaposherehekea, kila mmoja wetu anahisi moyoni mwake kwamba utashi wake umeshinda, imani yake imeshinda, malengo yake yameshinda, ule utaifa wa Kiarabu, ambao ulikuwa ndoto kwa kila mmoja wetu, utaifa wa Kiarabu ambao tulikuwa tunaita kwa hotuba, utaifa wa kiarabu ambao walikuwa wakiusoma miaka nenda miaka rudi katika mashairi.Ni muda mrefu…miongo kadhaa.Leo tukiwa tunasherehekea tunahisi utaifa huo wa kiarabu umeanza kutimia. na kuwa nyenzo. Leo, tunapoangalia kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, ambayo iliibuka kutoka kwa mapenzi yako na kutoka kwa dhamiri yako, tunahisi kuwa huu ni mwanzo.

Huu -Enyi Ndugu- ndio mwanzo wa ukombozi na mwanzo wa kuondokana na utawala wa kigeni na kuondokana na ukoloni.Huu ndio mwisho wa udhaifu na mwanzo wa nguvu.Huu ndio mwisho wa kutojali na mwisho wa mawakala wanaofanya kazi. Pamoja na wageni kuuza nchi yao, na mwanzo wa utawala wa watu huru; Utawala wa watu.. watu wazalendo.. watu halisi.

Leo – Ndugu zangu – ninapozungumzia maneno haya, nazungumzia Taifa la Kiarabu kama Taifa la Kiarabu linalojitegemea; Kila mtu ndani yake anamhurumia mwenzake, kila mmoja ndani yake anamuunga mkono mwenzake, kila mmoja ndani yake yuko katika mshikamano na mwenzake, kila mmoja ndani yake - katika nchi yoyote Ile na katika nchi yoyote ya Kiarabu ambayo waliiunda baada ya Vita vya Kwanza vya Kidunia. – anahisi kuwa nchi yake inajumuisha nchi zote za Kiarabu.

Leo – Ndugu zangu – tunapoadhimisha kuzaliwa kwa Jamhuri hii, tunatumai Mungu atatujaalia mafanikio, na tunatumai kuwa Mungu atatuunga mkono kwa nguvu zake, na tunatumai kuwa Mungu atatuongoza kwa dhamira na imani, na tumaini kwamba Mungu atatutia nguvu ili tuweze kufikia ndoto ambazo tulikuwa tunaziita, na ili tuweze kuanzisha katika eneo hili la Dunia kuna uhuru wa kweli, na kwamba hakuna nafasi ya nyanja za ushawishi, na kwamba tunajaza. Utupu ambao wanauzungumzia sisi wenyewe, na kwamba tunaweza kuwa msaada kwa Waarabu wote katika kila nchi ya nchi zao, na katika kila nchi ya nchi yao.

Leo-ndugu zangu tunaposherehekea kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu, iliyotokana na utashi wetu, iliibuka kutoka kwa dhamiri zetu, na Ikawa matokeo ya dhamira yetu.Tunaelekea siku za usoni, tukiamini kuwa tuko mwanzoni mwa njia; Njia ya uhuru, njia ya utendaji, njia ya umoja, na njia ya mshikamano. Mwenyezi Mungu awabariki. 

Al Salaam Alaykum Warahmat Allah.

---------------------------------------

Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kutoka kwa Ikulu kwa Wananchi na Taasisi za Kimisri na Kisyria; kumpongeza kwa kushika madaraka ya nchi.


Kwa tarehe ya Februari 23,1958.