The Egyptian Gazet ni mshirika mkuu kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

The Egyptian Gazet ni mshirika mkuu kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud

Miaka 141 imepita tangu kutolewa kwa toleo la kwanza la Gazeti la Egyptian Gazet, lililoanzishwa mnamo Januari 26, 1880 huko Alexandria kabla ya kuhamia Kairo, na Gazeti hilo tangu kuanzishwa kwake na waandishi wa habari waingereza watano  wakiongozwa na Andrew Philip, mhariri wake mkuu wa kwanza, akisaidiwa na Moberly.Bill, ambaye baadaye alifanya kazi kama mhariri mkuu wa "Times" ya Uingereza, - licha ya kuzingatia sera ya kutetea maslahi ya Jumuiya ya Uingereza nchini Misri na kuunga mkono sera ya Uingereza  katika Mashariki ya Kati, ila baada ya mapinduzi ya 1952 na kuhamishiwa umiliki wake kwa taasisi ya uhariri kwa uchapishaji na utangazaji , likawa kutetea maswala ya kiaarabu na likawa pia  kama msemaji rasmi wa kitaifa kwa  Lugha  hai  nyingi zinazoenea zaidi ulimwenguni katika awamu ya mageuzi ya kimapinduzi.

Vichwa vyake vya habari  na karatasi zake za  kwanza  zilionesha matukio makubwa na ya  hatari  ulimwenguni wakati wa mazungumzo ya uokoaji, mazungumzo ya ufadhili wa Bwawa Kuu, mgogoro wa Mfereji wa Suez, na Vita vya 1956, 1967, na 1973, Al-Gazet limekuwa chanzo, chimbuko la habari na uchambuzi kwa kile kinachohusiana na Misri katika viwanja viwili vya kikanda na ndani na hili ni jukumu hilo hilo ambalo linalotoa sasa hivi,kama kuonyesha wazi lililofanywa na    uongozi wa kisiasa  katika nyanja za ndani na nje ya nchi na njama inazozikabiliana nazo , na kurekebisha habari zozote za uongo zinazoilenga Misri mbele ya Jumuiya za kigeni na mabalozi nchini Misi  ,bali  Duniani kote .

Katika historia yake yote, Gazeti hili lilikuwa chanzo cha habari halisi, liliripoti matukio ya Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia na Kabla ya hivyo, lilishuhudia mradi wa kuchimba Mfereji wa Suez, mapinduzi ya kiaarabu, na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Gazeti limekuwa maarufu mwanzoni na hata hadi leo kwa makala  zake za uhariri zenye hekima ,  zinazohusika kwa maoni, uchambuzi na ufafanuzi  masuala mengi ya kimataifa, kikanda na ya ndani. Miongoni mwa makala hizo maarufu zaidi ambazo hazikubeba majina ya waandishi wake kwa sababu zinaelezea mtazamo wa gazeti kwa ujumla (tahariri),  zile zilizozungumzia Vita vya Korea na athari zake , Vita Baridi, makubaliano ya kuhamisha majeshi ya Uingereza kutoka Misri, matatizo ya chama cha Ikhwan  cha kigaidi, na Vita vya Kiarabu na Israel.

Katika uwanja wa ndani, makala za Gazeti zinashughulikia hali ya uchumi na miradi ya kitaifa, kijamii na kiutamaduni. na kile Kinachothibitisha nguvu na msimamo wa uadilifu  wa makala za Gazeti ni  yaliyoripotiwa na idadi kubwa ya mashirika ya habari  na kuitaja  katika magazeti ya kigeni.

Tafiti na uchunguzi zilizofanywa katika miaka ya hivi karibuni zimeonesha kuwa wasomaji wa Gazeti  wamejikita katika makundi yafuatayo,  na kuyataja kwa nafasi mfululizo wake : jumuiya za kigeni, mabalozi, watalii wanaosafiri kwa treni, ndege na bahari, wageni wa hoteli za kigeni, wafanyakazi wa makampuni ya kigeni , wafanyabiashara katika nyanja mbalimbali, na wanafunzi wa Sehemu za Kiingereza katika vyuo vikuu. Na maafisa wakuu wa serikali ambao kazi zao zinahitaji kufuatilia kile kinachochapishwa kwenye magazeti ya umma na yale yanayochapishwa kwa lugha za kigeni. gazeti hilo limefikia mikoa yote ya Misri, pamoja na tovuti yake, ambayo watumiaji wake wameorodheshwa baada ya Misri kwa mfululizo, Marekani, Ujerumani, Uingereza, nchi ya Falme za Kiarabu, Uchina, Saudi Arabia na Uholanzi. Mohamed Fahmy  anaongoza uhariri wake kwa sasa , na anasaidiwa na kundi fulani .