Mpango wa Afro-Media ni Mshiriki wa vyombo vya Habari kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Mpango wa Afro-Media ni Mshiriki wa vyombo vya Habari kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Mpango wa Afro-Media ulionesha furaha yake kubwa kwa kuchaguliwa kuwa mshirika wa vyombo vya habari kwa Udhamini huo, kutokana na jitihada za Afro-Media kuwa daraja la vyombo vya habari kati ya watu wa Misri na watu wengine wa Afrika, kwa kutambulisha juhudi za kitaifa za Misri kuelekea maendeleo ya bara la Afrika, ambapo Udhamini wa Nasser ni mojawapo ya jitihada muhimu zaidi kwa wakati huu, tena sambamba na wakati wa tukio hilo, tuko pamoja nanyi daima  ili kufuatilia  magazeti muhimu zaidi na chaneli za televisheni zinazohusika na utangazaji wa vyombo vya habari vya tukio hilo, ili kuratibu juhudi zinazohusika na kuandaa ujumbe wa vyombo vya habari, na tutakupa habari nyingine zote moja kwa moja.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa uko katika toleo lake la pili pamoja na ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, na kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", unaolenga viongozi watendaji wa vijana wenye taaluma na watendaji mbalimbali ndani ya jamii zao katika ngazi ya mabara matatu ya Afrika, Asia na Amerika Kusini.