Mpango wa Wajitolea wa Umoja wa Afrika

Mpango wa Wajitolea wa Umoja wa Afrika

Imefasiriwa na / Osama Mostafa Mahmoud

Ni mpango wa maendeleo ya vijana Barani Afrika, unalenga vijana wenye uzoefu wa kujitolea na uzoefu wa kazi na unahimiza vijana kama washiriki wakuu katika kufanikisha Maendeleo, Amani na Ustawi wa bara hilo, tena mpango huo unakusanya vijana na kuwafundisha katika mafunzo ya msingi yaliyojikita katika kukuza roho ya kutoa huduma na kujitolea kwa Vijana wa Afrika wanaoshiriki.

Maeneo ambayo mpango unayalenga yanatofautiana na yanajumuisha Afya, Amani na Usalama, pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Ujasiriamali wa Vijana, pamoja na Kilimo na Mazingira, na mpango unahitaji kusambaza vijana washiriki kwa Taasisi za Umoja wa Afrika na mashirika husika pia kwa mwaka mmoja katika maeneo mbalimbali ya bara la Afrika.

Ikumbukwe kuwa Mpango wa Wajitolea wa Umoja wa Afrika (AU-YVC) ni mpango mkubwa zaidi wa kujitolea Barani Afrika, ulizinduliwa mwaka 2010, kwa lengo la kuwekeza katika nguvu za vijana, kushiriki maadili yao, na kukuza kazi yao kati ya jamii zao za mitaa, mashirika yasiyo ya kiserikali, mamlaka za serikali, na sekta binafsi, na hufanya kazi kwa msaada wa Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063, inayolenga Afrika linaloongozwa na Vijana wake, kupitia  kufanya kazi kwa mwaka mmoja mzima katika mojawapo ya nchi za Afrika, tena mpango huo unalenga kuwajengea uwezo vijana na kuwawezesha kupitia uzoefu wa kitaaluma, kufanya kazi katika maeneo ya maendeleo ya huduma kwa nchi zote za bara hilo katika maeneo mengi ya sekta na taasisi, pamoja na kukuza mwelekeo wa Vijana katika mashirika ya Afrika, na kuimarisha Umoja na Ushirikiano wa Afrika kupitia kubadilishana.